Usomi wa Slaa una maswali kuliko majibu! Doctarate yake ni ya Kupewa - Kigwangala

Usomi wa Slaa una maswali kuliko majibu! Doctarate yake ni ya Kupewa - Kigwangala

Kwa miaka 15 Dr Slaa alipokuwa Bungeni hakuna aliyeuliza elimu yake. Si Kingwangalla wala mwajiri wake Kingwangalla. Sasa wakubwa wa Kingwangalla wameshikwa pabaya wananza kulia na elimu ya Dr Slaa. Walianza na mke wake, wakenda kwenye mshahara na sasa Kingwangalla anajiona amekuja na silaha mpya - elimu ya Dr Slaa.

Sijui Kingwangalla ana uelewa kiasi gani kuhusu mfumo wa elimu ndani ya kanisa Katoliki. Lakini angejishushulisha Kingwangalla angedundua kwamba hata elimu tunayoiita elimu dunia ina elements za mfumo wa elimu unaotumiwa na kanisa. Akumbuke Catholism imekuwepo kwa zaidi ya karne na hiyo elimu tunayoipata imekopa sana kutoka kwenye mfumo wa elimu ndani ya kanisa katolioki. Hivi anajua hivi number i, ii, iii, iv, v, vi, ............etc. Huko Seminary wanasoma psychology, economics, thoelogy, law etc. na sio kama wanasoma catholism peke yake, ni mchanganyiko wa catholism na elimu ya kawaida.

Dr. Slaa anaongea lugha 7! narudia lugha 7. Dr Slaa ameweza kuwamulika mafisadi na ufisadi ndani ya mfumo wetu kiutawala Tanzania. Dr. Slaa ameanika uchafu wa kutisha ndani ya ccm na sasa wanajivuwa magamba. Dr. Slaa amejenga chama kikuu cha upinzani - sio zile kachumbari za CDM+CUF+UDP etc. Tuna chama kimoja kimeshika dola kuna kingine ni official opposition and the rest can sort out themselves. Na tayari tumeona faida ya kuwa na chama kimoja kikuu cha upinzani. Kingwangalla ame-achieve nini? hata kwenye mchakato wa ubunge ndani ya ccm he came 3rd!!! Kingwangalla is a classic example of everything wrong in our governance system hapa Tanzania. Inakuwaje No 3 ndio atangazwe mshindi!

Anaonekana kukerwa na udokta Slaa na kaenda mbele zaidi na kusema Dr Slaa hana Degree. Pale magogoni kuna mheshimiwa mmoja ana doctorate 3 huku hana hata Masters na mbaya zaidi haijulikani udokta wake ni wa nini ana aliandika paper gani. Even worse moja ya chuo kilichompa udaktari hakina hadhi ya ky-issue doctorate. Kwenye cabinet na hata bungeni wapo madokta fake kibati. Kingwangalla haoni hayo yeye amekazana na Dr Slaa. In his view Kingwangalla anataka nini hasa kifanyike - Dr Slaa atolewe CDM? avuliwe uraia kama Bashe au iwaje?

Yeye aseme wazi, wamemshindwa Dr Slaa kwa hoja sasa wamewekeza kwenye siasa maji taka! Haitalipa!
 
Yani ilianza "CCM ni mafisadi".Ikajibiwa "Slah na Mbowe pia mafisadi".
Ikaja "UDAKTARI wa JK ni sawa na wa dokta MANYAUNYAU.Imejibiwa "Slah pia".
CCM MUST BE BRAIN DAMAGED.
 
Slaa bonge la bomu! :hatari: :hatari:

Huna aibu kama si slaa ccm ingejuvua gamba lini pili tangu tupaye uhuru hatujawahi kuwa na mbunge aliyeweza kutoa hoja nzito na zenye mantiki kama Slaa pili wewe binafsi inasemekana umesoma kwa kutumiavjina la mtu tatu sijawahi kusikia kutoka kwako issue yoyote ambayo sisi kama vijana tunaweza kukuqote kwenye maongeze ya mustakabali wa taifa hili kama dimosei Slaa has proved beyond doubt that he is a truly patriotic leader.nne huone viongozi kama lyatongo wamejibandika udk ili wajaribu kuona kama wanaweza kupata umaarufu kama wa Slaa lakini wapi.mwisho naona kama.umesukumwa ni uwivu zaidi na haipendezi kijana wa makamo yako kuwa na uwivu
 
Almost kila msomi ana proffession moja anayosomea, ndo maana kuna wengine madaktari wa kutibu, wengine wanasheria, wengine watawala and so on na wengine wa dini ila wote ni wasomi. Waliingia darasani na kufuata taratibu zote za kisomi. Mtazamo wangu elimu ya dini na ya dunia yote ni usomi, the issue ni civilization au tuseme badiliko la mtu(toal change) of behaviour, attitude na mengine mengi. Haya na aje aseme huyu Kingwangala udakatari wake anauaplai wapi bungeni?
 
This is why I said yesterday that CHADEMA IS BELOW PAR. Look what we have from Slaa!! What about Freeman? Same sht.
 
Slaa bonge la bomu! :hatari: :hatari:
Watakucheka watu. Elimu itolewayo na kanisa katoliki inaheshimika duniani kote. Tazama shule zao tz. Mwulize mh. JK. Ukweli haubatilishwi na uongo.
 
Kigwa mwenyewe alifeli hata standard seven akatumia jina la mtu kwenda secondary leo anajifanya anaponda PhD za watu walozisotea, sijui hata huo udaktari ameupataje. Kigwa anaweweseka kwa kuwa anajua alibebwa, na ile mbeleko ilombeba ya mama salma imechanika, kwa hiyo hana kipindi kingine tena cha ubunge, tuone huu utumbo wake na ujinga wake atausemea wapi. Na Bashe ameshapewa uraia wake alopokwa mwanzo jiandae kumkabidhi jimbo no kulikabidhi jimbo chadema.

Hivi yale maandamano ulokuja nayo kwa mbwembwe yaliishia wapi Kigwa, yako unayashindwa unaanza kudandia ya watu, be careful kijana, Slaa ni mziki mnene huuwezi wewe mzee wa kubebwa.
 
Sijaambulia kitu hapa naona manyokanyoka tuuu!
Hebu kwanza,
Hoja ni nini? Dr Slaa hakusoma URBANIANA? hana PhD? Hakusoma? au nini basi? Tukianza kupekuana hivi hata huyo bingwa wa SHAHADA ZA UZAMIVU WA UCHAKACHUAJI hatobaki salama!
Kigwangala awe wazi, Hoja yake nini??? au ni CHUKI tu? anataka wote tuwe na digrii za Madrasa? Anapaswa kuelewa taratibu za udahili haziko uniform kama yeye na vilaza wenzake wanavyotaka tuamini!!!
 
Mjadala huu hauna faida hata kidogo . Ujinga mwingi uko kule CCM wanaodhani kwamba kuwa na title kama Prof , Dr nk inamsaidia kuwadanya wananchi na kupewa Ubunge . Huu ni upumbavu kujadili elimu ya Slaa .Huyu mtu kama ni mwana CCM yeye aje atueleze inako elekea maana kuna hali ya hatari hadi polisi sasa wanaua hadharani . Slaa ana PhD ambayo haina ubishi na hana haja ya kuja kupoteza muda wake hapa badala ya kujenga Chama .
 
Tujiulize swali ni nini chanzo cha elimu? ni kweli wasio na degree hawana akili? hawawezi kuongoza? hii notion sio kweli kabisa! wasomi wa nchi hii wameifanyia nini tanzania zaidi ya kuinua mabega na kujitapa na kuwa wezi! ni nini cha maana wamefanya? hadi leo barabara zetu zinajengwa na watu toka nje, embu niambie nyie mnaojiita wasomi mliokosa uzalendo mmelifanyia nini taifa hili zaidi ya kuwasaliti maskini waliowasomesha kwa kodi zao! Uzalendo haumo mioyoni mwenu, wala rushwa wakubwa! Embu nenda kwenye library za nchini kwetu niambieni ni vitabu vingapi vimeandikwa na watanzania? wanaojiita wasomi? enyi receptive mind msiofikiria! tunahitaji kiongozi mwenye busara na mwenye uwezo mkubwa wa kutafakari, wasomi ni watu wa kutumiwa tuuu, ni lazima wawe chini mwenye kutafakari.
UKILETA VIGEZO HIVYO UTATAKA KUNIAMBIA MAPROFESA NDIO VIONGOZI WAZURI! NAQ HIYO SIO KWELI ENHE KIGWANGALA ULIEANZISHA MGOMO MUHIMBILI!

Huyu jamaa anachemka sana, sijui anawaza nini, kumbe na migomo alikuwa anaogoza, ubunge kapewa hebu anyamaze na vikao vya bajeti vinaanza ngoja tumwona na hiyo Doctor yake atakuwa anapambana vipi.... upeo mdogo wa kufikiri
 
Mike Tyson pia ana PhD....so?
Hivi usomi maana yake nini? Naona tunachanganya mambo.certificates zoote,diploma zoote na phd bado tunahoji usomi wa mtu? Au mpaka tuone neno degree ndio turidhike.usomi wa kweli ni kupita vyuo halali,je Dr slaa kafoji? Hivi mnajua shughuli ya phd ya canon law au mnaongea tu! Usomi ni pamoja na content ya vitu ulivyosoma fatilieni phd za canon law alafu mlinganishe na phd za kawaida.alafu acheni kukariri mifumo ya elimu kuna vyuo vina asses content ya vyeti vyako kupitisha kusoma elimu ya juu zaidi na sio neno degree kwenye certificates! Mfano kuna degree za uhasibu za miaka 3 vyuo vya nje na halali lakini content zake ni diploma ya CBE! Tujadili ya msingi kama Dr slaa amefoji vyeti uwekwe ushahidi lakini si ku compromise usomi wake.kuna wasomi wazuri tu na wana deliver vizuri tu maofisini wakiwa na masters bila undergraduate degree! Usomi si mpangilio wa formal academic wakuu.hizi siasa tunazipeleka kusiko leteni mjadala wa maendeleo mnayotuletea wananchi nyinyi kama chama tawala na si longo longo.huyo Kigwangala ambae ni Dr na zitto mwenye masters nani zaidi kihoja? Upupu mtupu!
 
Niliwahi kuleta thread ikihoji elimu ya Slaa, wanamgambo wakaitia kapuni! Tatizo ni jinsi nyinyi wanamgambo mnavyoipaisha hiyo elimu ya Slaa, wakati kimsingi ina kasoro nyingi na magumashi kibao! Kama mngeichukulia kawaida hakuna mtu ange-scrutinize, ila label mnazompa Slaa ndizo zinawaponza! Dr Ph D wa ukweli...............wapi!
 
Mjadala huu hauna faida hata kidogo . Ujinga mwingi uko kule CCM wanaodhani kwamba kuwa na title kama Prof , Dr nk inamsaidia kuwadanya wananchi na kupewa Ubunge . Huu ni upumbavu kujadili elimu ya Slaa .Huyu mtu kama ni mwana CCM yeye aje atueleze inako elekea maana kuna hali ya hatari hadi polisi sasa wanaua hadharani . Slaa ana PhD ambayo haina ubishi na hana haja ya kuja kupoteza muda wake hapa badala ya kujenga Chama .

Hapoo kwenye red hapo, ndo iko maneno ya ukweli.
 
Tanzania tuna matatizo sana, nadhani ni inferiority complex. Asha Migiro kule UN hakuna anayetaja cheo cha cheti chake DR. UN hawaruhusu hiyo only kama wewe ni Doctor wa kutibu watu. basi.

Kwa mtu mwenye akili timamu na anayejiamini basi hana haja ya kujitafutia uhalali kutia vyeo vya njia za mkato.

Koffi Annani - ni Professa,
Condelesa Rice- assistant Professa
Hata huyu bwana mkubwa wa IMF alipatwa na madhira New York Dominique Kahn ni Professa
Wote hawa wako poa hakuna majigambo
 
Inaonekana kabisa mwandikaji ni mshamba wa elimu elimu inaenda kwa credit Hours na kama hujui hii ni nini basi usirukie mambo.

Cha kujiuliza ni miaka mingapi Dr Slaa kasoma baada ya kidato cha sita? kwani ukifanya hivyo ndiyo utaelewa maana kila Darasa unalochukua ni credit Hrs na kuchukua Degree za juu inaelekea elimu yako ya kabla ni kubwa kiasi gani. Mfano mimi nilivyokuja kusoma Marekani nilipewa Credit Hrs 29 za History, Economics na Geology kwasababu nilichukua HGE A-Level. Hivyo kwenye Degree program yangu ya Credi Hrs 134 nilipewa 29 Hrs kabla hata ya kuanza chuo!. Dr Slaa alikuwa na Credit Hrs nyingi wakati anasoma kwenye Vyuo vya Theology hivyo alikuwa kashachukua masaa mengi yanayohitajika kwa PHD. Kwenye PHD za miaka minne miaka mitatu ni ya Darasani na unachukua madarasa na mwaka mmoja ni wa Research ambayo kwa watu wengine wanashidwa research na wanachukua madarasa tu. Hivyo Dr slaa alikuwa tayari na madarasa mengi hivyo hakuwa ha haja ya kusoma miaka mitatu hivyo kasoma kidogo na kufanya Research ya PHD. Lakini ukiangalia miaka mingapi katumia kusoma kuanzia Form 6 ni sawa na bongo tu. Bongo (3-Chuo, 1- Master na 4 PHD) Dr Slaa katumia miaka zaidi ya 8 iliyopo hapa.
 
Back
Top Bottom