Kwa miaka 15 Dr Slaa alipokuwa Bungeni hakuna aliyeuliza elimu yake. Si Kingwangalla wala mwajiri wake Kingwangalla. Sasa wakubwa wa Kingwangalla wameshikwa pabaya wananza kulia na elimu ya Dr Slaa. Walianza na mke wake, wakenda kwenye mshahara na sasa Kingwangalla anajiona amekuja na silaha mpya - elimu ya Dr Slaa.
Sijui Kingwangalla ana uelewa kiasi gani kuhusu mfumo wa elimu ndani ya kanisa Katoliki. Lakini angejishushulisha Kingwangalla angedundua kwamba hata elimu tunayoiita elimu dunia ina elements za mfumo wa elimu unaotumiwa na kanisa. Akumbuke Catholism imekuwepo kwa zaidi ya karne na hiyo elimu tunayoipata imekopa sana kutoka kwenye mfumo wa elimu ndani ya kanisa katolioki. Hivi anajua hivi number i, ii, iii, iv, v, vi, ............etc. Huko Seminary wanasoma psychology, economics, thoelogy, law etc. na sio kama wanasoma catholism peke yake, ni mchanganyiko wa catholism na elimu ya kawaida.
Dr. Slaa anaongea lugha 7! narudia lugha 7. Dr Slaa ameweza kuwamulika mafisadi na ufisadi ndani ya mfumo wetu kiutawala Tanzania. Dr. Slaa ameanika uchafu wa kutisha ndani ya ccm na sasa wanajivuwa magamba. Dr. Slaa amejenga chama kikuu cha upinzani - sio zile kachumbari za CDM+CUF+UDP etc. Tuna chama kimoja kimeshika dola kuna kingine ni official opposition and the rest can sort out themselves. Na tayari tumeona faida ya kuwa na chama kimoja kikuu cha upinzani. Kingwangalla ame-achieve nini? hata kwenye mchakato wa ubunge ndani ya ccm he came 3rd!!! Kingwangalla is a classic example of everything wrong in our governance system hapa Tanzania. Inakuwaje No 3 ndio atangazwe mshindi!
Anaonekana kukerwa na udokta Slaa na kaenda mbele zaidi na kusema Dr Slaa hana Degree. Pale magogoni kuna mheshimiwa mmoja ana doctorate 3 huku hana hata Masters na mbaya zaidi haijulikani udokta wake ni wa nini ana aliandika paper gani. Even worse moja ya chuo kilichompa udaktari hakina hadhi ya ky-issue doctorate. Kwenye cabinet na hata bungeni wapo madokta fake kibati. Kingwangalla haoni hayo yeye amekazana na Dr Slaa. In his view Kingwangalla anataka nini hasa kifanyike - Dr Slaa atolewe CDM? avuliwe uraia kama Bashe au iwaje?
Yeye aseme wazi, wamemshindwa Dr Slaa kwa hoja sasa wamewekeza kwenye siasa maji taka! Haitalipa!