Uspika wa Bunge 2022: Sababu za Kisheria na Kikatiba Dkt. Tulia kukosa sifa za kugombea

Kwa kuwa kanuni za bunge zinamtaja kuwa endapo spika atajiuzuru yeye anakuwa kaimu spika,hivyo basi zuio hilo linamuhusu bila chenga.
 
Hapana, usianze na absence ya Tulia. Anza na absence ya Ndugai. Kifungu kinachotumika hapa mahsusi (specifically) ni - Kf. 41 (1) (a) tayari nafasi ya Spika ni Vacant - automatically Tulia amekalia kiti cha Spika kwa muda (Amekaimu) akisubiri nafasi hiyo ijazwe. Hivyo kwa sasa yeye ana mamlaka ya Spika (Tulia amekuwa Kaimu Spika). Kwa nafasi yake ya uKaimu spika tayari inamkosesha vigezo vya kugombea uspika kwa kuwa Katiba imekataza mtu mwenye madaraka kugombea nafasi hiyo.
 
Tanzania hatuna katiba tuna maoni ya raisi,hivyo ni vyema angeulizwa Samia kuwa anachukuliaje Hilo swala
 

Bila kupepesa macho Mtemi Andrew Chenge ndiye anayefaa kuwa Spika wa bunge
 
Afadhali kuna kitu kama hiki..japo hakupenda kabisa kijulikane kwa wengine
 
Kwa sasa Tulia ni Deputy Speaker (naibu Spika) na acting Speaker (kaimu Spika), wala sio Speaker. Angekuwa Speaker kusingekuwapo zoezi la kumtafuta Speaker tena !
 
Napata shida na hiki watu walichokikomalia kwa Tulia,

Huu mchakato unaoendelea ni wa kichama (Maccm) yanapambana kupata mgombea watakaye mdhamini. Kwa vyovyote mpaka muda huu Tulia anazo sifa kama mwanachama yeyote lakini ikitokea ccm wameteua jina la Tulia awe mgombea wao wa kiti Cha Uspika ni lazima Tulia ajiuzulu unaibu Spika ndipo apate sifa ya kuchukua fomu ya kuwa mgombea rasmi.

Sijui kinachowaumiza watu kuhusu Tulia mpaka hapo.
 
Naona wapinzani wa Tulia wanahangaika kwa kila sarakasi.

Kwani mnaogopa nini? Kamatia hapo hapo Tulia.

Nani anamuogopa huyo wa kubebwabebwa. Watu wanajadili kuhusu kukiukwa kwa sheria wewe unaleta Mambo ya kuogopwa. Yeye kwa Sasa ni kaimu speaker lakini bado anataka unaibu speaker. Yani viti vyote vya kwake.
 

Watu wanataka mtu mpya. Sio damu ya zamani ya kunguni.
 
Watu hawatak kufuata katiba
Huu ujinga ulianzishwa na mtu fulan sasa wengine wanaiga
Watanzania tusikubali huu uhuni
 
Watu wanataka mtu mpya. Sio damu ya zamani ya kunguni.
Issue kubwa iliyopo ni kama Tulia ana sifa ya kutia Nia kwenye Uspika ndani ya Chama au Hana. Hili ndilo linatusumbua wengi.

Kuhusu damu Mpya mbona wengi washatia Nia....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…