Ustaarabu na unyenyekevu utakusaidia siku ambayo akili yako imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo lako

Ustaarabu na unyenyekevu utakusaidia siku ambayo akili yako imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo lako

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Nimekumbuka vitu kadhaa leo ngoja nijitahidi kuandika japo sio mwandishi mzuri sana.

Kunawakati tunapitia vitu vingi na tunakutana na watu wengi tofauti tofauti kwenye maisha wenye kutufurahisha na kutukwaza lakini tujitahidi kujifunza ustaarabu na unyenyekevu hasa tunapokwazika inawezekana ukatulipa vizuri bila kujua ni wakatigani na katika mazingira gani.

Tujitahidi Kuishi kwa wema hata kama unaona ni watu wa chini sana kukuzidi, tusidharauliane.

Nimekumbuka tukio lililonifundisha kuwa ustaarabu unalipa;

Nilikuwa nasafiri mkoa fulani, kipindi hiki stendi ni Ubungo Terminal sikukata tiketi na nilichelewa sana. Nikafika Dar saa nne usiku, hadi nafika Ubungo ni saa tano. Nikashuka kwenye daladala lengo nielekee ndani kukata tiketi.

Sikuwa mwenyeji maeneo yale wale, wabeba mizigo wakaanza kunigombaniia huku mmoja akivuta begi langu nikafanikiwa kumnyang'anya lakini bahati mbaya likakatika mkono. Nilichukia sana aisee, nikimuangalia kwa hasira lakini nikaishia kumwambia aache, sikumtusi wala sikumtolea kauli chafu.

Wakat natoka kuna kaka akanifata kunielekeza kuwa kuna njia ya shortcut, akanionesha upande wa kupita, Ilikuwa usiku nikiwa sielewi nipite wapi. Nikiangalia upande wa pili wa barabara nikamuona yule kaka aliyeniharibia begi akinitazama sana nikawa namuangalia kiwizi wizi.

Akanionyesha ishara nisipite na yule kaka bali ninyooshe barabara kubwa. Kwakweli nilikuwa nishakubali kupita kule kwenye giza nilikoambiwa kuwa ni shortcut, nikafata maelekezo mwingine nikanyoosha nikakuta geti nikaingia nikiwa salama.

Sijui ingekuwaje ningepita kule kichochoroni, aliniokoa sana pengine lingenikuta jambo baya. Nikajiuliza ingekuwaje ningemjibu vibaya au kumtukana kwa makosa yake ya kunikatia mkanda wa begi?!

Nafikiri sote hatujakamilika lakini huenda haya madogo madogo yakatubeba. Unayemdharau leo huenda ndio akakusaidia kesho na kuwa mnyenyekevu na mstaarabu siyo kukosa akili bali ni jambo la kiungwana sana 🙏🙏🙏.

Sio lazima ukitukanwa ujibu au ukichukizwa ulipize, tuishi humo wapendwa.

Screenshot_2023_0220_210436.png
 
Aaarghh!!! Mimi ukinikwaza majibu utayapata Kwa haraka sana.
Inawezekana ndo kinachokupa amani Bora tu useme yaishe au nyie ndo mkikwazwa ukianza kuongea asubuhi hadi jua linazama 😂😂😂kesho unaamka nalo Tena asubuhi
 
Jamaa mmoja alikuwa anawahi kwenye usaili alioitwa kwa ajili ya kazi aliyoomba. Akiwa katika harakati na purukushani za usafiri wa daladala, kwa bahati mbaya mama mmoja wa makamo alimkanyaga kidogo kwenye kiatu chake kilichong'arishwa vizuri, ili aonekane 'smart' na kumuongezea 'credit' kwenye usaili.

Jamaa alimgeukia yule mama na kumshambulia kwa maneno makali yenye kejeli na matusi mbele ya umati wa watu ndani ya daladala ile!

Mama wa watu akajitetea na kusema kuwa hakukusudia kumkanyaga na kumwomba amsamehe, lakini wapi, jamaa akaendelea kusema maneno mabovu juu ya yule mama. Baadhi ya watu wakamuonea huruma mama yule, hivyo wakamsihi jamaa anyamaze, yaishe.

Ndio jamaa akatulia. Jamaa alipofika akasubiri na wenzake kwa ajili ya kuitwa kwenye chumba cha usaili. Ilipofika zamu yake, alipoingia kwenye chumba cha usaili, alimkuta yule mama aliyemtukana kule barabarani ndio mkuu wa usaili! Jasho lilimtoka!
 
Jamaa mmoja alikuwa anawahi kwenye usaili alioitwa kwa ajili ya kazi aliyoomba. Akiwa katika harakati na purukushani za usafiri wa daladala, kwa bahati mbaya mama...
Inasikitisha sana kunawakati tutakosa kusaidiwa sababu ya maneno mabaya
 
Jamaa mmoja alikuwa anawahi kwenye usaili alioitwa kwa ajili ya kazi aliyoomba. Akiwa katika harakati na purukushani za usafiri wa daladala, kwa bahati mbaya...
Motivational speaker umeanza Tena?
 
Back
Top Bottom