Ustaarabu wa ikolojia wa China ni mfano wa kuigwa wa maendeleo ya kijani barani Afrika

Ustaarabu wa ikolojia wa China ni mfano wa kuigwa wa maendeleo ya kijani barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111447318085.jpg


China, ikiwa ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, ustaarabu wake wa ikolojia una mifano mingi ya kuigwa na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, hususan zile za Kusini.

Ustaarabu huu wa ikolojia wa China unaweza kutendeka, una faida, na ni endelevu katika kuleta usasa, na hasa kupitia sera bora za kiuchumi na mikakati inayochangia maisha ya masikilizano kati ya binadamu na asili. Katika muongo mmoja uliopita, maendeleo endelevu ya ubora wa juu ya China yameendelea kujengwa chini ya misingi mitano imara, ambayo ni uvumbuzi, uratibu wa pamona, kijani, ufunguaji mlango na mabadilishano.

Wakati China na Afrika zikipanua maeneo ya ushirikiano wao wa kiuchumi, bara la Afrika limechukua nafasi ya mbele katika kutambua thamani ya ikolojia ni kichocheo, ama injini, na sio kikwazo cha ukuaji wa uchumi. China imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya mageuzi ya misitu, na nchi nyingi za Afrika nazo zimeanza kufanya hivyo. Tukichukulia mfano wa mradi wa kurejesha hadhi ya maeneo ya misitu na miti iliyoharibiwa ambao umezinduliwa hivi karibuni katika kaunti ya Kwale, ambao umehusisha wakulima 65,000 katika maeneo ya Lungalunga, Msambweni, Matuga na Kinango. Mradi huu unalenga kuwaletea wakulima hao kipato kwa njia ya kuuza hewa ya kaboni, kutokana na wakulima hao kupanda miti ya kiasili na ya matunda. Hatua hii sio tu kwamba itawaongezea kipato wakulima hao, bali pia ni njia mojawapo ya kuboresha ikolojia, na hivyo kusaidia katika kuondokana na kuongezeka kwa jangwa na ukame.

Bara la Afrika lina eneo kubwa la misitu na miti, na linaweza kutumia maliasili hiyo kunwa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.

Katika ujenzi wa njia ya maendeleo ambapo asili na uchumi wa jamii haviwezi kuchukuliwa kama maeneo tofauti ya ukuaji wa uchumi bali ni pande mbili zinazotegemeana, China inalionyesha bara la Afrika kuwa maendeleo ya uchumi sio lazima yaendane na uharibifu wa ikolojia.

Kwa miaka mingi, nchi za Afrika zimekuwa na hofu na wasiwasi kuwa kuongeza kasi ya uchumi na kuwa za kisasa kunawezekana tu kupitia uharibifu mkubwa wa mazingira. Lakini leo, China inaonyesha mfano wa maendeleo kwa nchi za Dunia ya Kusini ambazo kuwa nyuma kiuchumi na matishio ya kimazingira hayapaswi kuwa kikwazo cha ukuaji wa uchumi.

Mageuzi ya kijani sio tu kwamba yanawezekana, bali yanapaswa kuwa njia pekee kwa nchi za bara la Afrika lenye utajiri mkubwa wa ardhi na misitu ya asili. Pia, kwa kushirikiana na China, mchakato huo hautakuwa tena wa majaribio, bali ni jambo lenye uhakika wa kufanikiwa, kwani China inaendelea kutoa ushauri bora kwa Afrika na nchi nyingine zinazoendelea ili kusaidia katika mageuzi ya kijani ya viwanda.

China kwa sasa ni nchi inayoongoza katika sekta ya kijani ya uchukuzi, na tayari imezisaidia nchi za Afrika kama Nigeria kuanza mabadiliko katika sekta hiyo na kutumia aina ya magari yasiyotoa uchafuzi mwingi. Tukichukulia mfano wa Kenya, nchi hiyo imezindua mradi wa mabasi ya usafiri wa umma yanayotumia umeme, na hivyo kusaidia kupunguza uchafuzi wa hewa. Pia nchini Nigeria, mwanzoni mwa mwaka huu, ulizinduliwa mradi wa reli nyepesi ya umeme inayojengwa na China katika mji wa Lagos, ikiwa ni awamu ya kwanza ya mradi huo unaotekelezwa chini ya Pendekezo la Ukanda mmoja, Njia Moja (BRI).

Tukirudi nyuma na kuangalia kiini cha nguvu ya uchumi wa nchi hii, tunaona kuwa ni utambuzi na heshima kubwa kwa maliasili, na hii inatokana na kutunga na kutekeleza sera za kitaifa zinazolinda na kuhifadhi maliasili, huku wakati huohuo, zikilinda mazingira. Ulinzi wa ikolojia ni zana muhimu inayoweza kusaidia pakubwa katika ustaarabu wa ikolojia ambao umejikita katika maendeleo ya uchumi na jamii.

Wakati China na Afrika zikiendelea kuimarisha urafiki wao uliodumu kwa miongo kadhaa, kuna mafunzo mengi ambayo nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutoka China kuhusu njia ya maendeleo ya uchumi na ikolojia, ambayo China imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuifuata, kutokana na kutunga na kutekeleza sera za kitaifa zinazolenga kuchochea ulinzi wa mazingira. Sera za kijani za China zinasaidia katika kudhibiti majanga ya kimaumbile, kulinda dunia yetu, na wakati huohuo, kuchochea ukuaji wa uchumi ambao haujawahi kushuhudiwa duniani.
 
Back
Top Bottom