Ustaarabu wa kurudisha miamala iliyokosewa

Kuto rudisha hela ya watu ni level ya kuto kua mstaarabu yani ni mwizi, ndio mana hii nchi asilimia 90 watu ni wezi ila tu hawajapata fursa ya kuiba, maendeleo kama nchi kupata ni ndoto labda maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
 
Kuto rudisha hela ya watu ni level ya kuto kua mstaarabu yani ni mwizi, ndio mana hii nchi asilimia 90 watu ni wezi ila tu hawajapata fursa ya kuiba, maendeleo kama nchi kupata ni ndoto labda maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Una point mkuu
 
Wapare bana😁

Na atanishukuru Sana.

Nakumbuka nilikuwa na biashara ya Duka lenye biashara ya muamala pia ndàni yake.

Akaja mteja, akasema nimuwekee 14k Sasa Mimi sijui ilikuwaje nikaweka 140k. Sikujua.

Jioni kwèñye mahesabu nashangaa kûna upungufu kama WA 126k.
Tafuta Wapi, fungua droo wapi. Nikasema labda nimeziweka kwèñye shelves ambako nafichaga maana Pesa zingine nazoachaga dukani nafichaga Nyuma ya shelves. Hollaaa!

Nikasema labda niliziacha nyumbani. Narudia nyumbani sehemu napo fichaga. Hollah. Duuh!

Nikakata tamaa, nikahesabu nimepata Hasara ambayo kuifidia ingenichukua Siku tisa au Kumi kwani kipindi kile kwèñye miamala tuu Kwa Siku wastani nilikuwa napata 10k mpaka 12k nje y biashara zingine.

Kesho yake naenda Dukani, nikiwa nafanya Usafi nikatafuta tenà na tena 126 yàngu. Wapi. Nikakata tamaa.

Baadaye jioni hivi akaja Dada mmoja anayeendesha Harrier Tako la Nyani akiwa na miwani Yake. Akashuka Kwa gari akaja pale Dukani.
Sikuwa namjua Sana yàani siô mteja wàngu wa mara Kwa mara.

Akanisalimu nami Kwa uchangamfu sijambo, Basi akawa anacheka mwenyewe.

Akaniuliza swali, kîla kitu kiko Sawa.
Nikamjibu, Yeah! Huku Akili yàngu ikijaribu kuhusianisha kauli hiyo na Mada zilizopita.
Akaniuliza, unahakika?
Hapo Akili yàngu Kwa upesi ikakumbuka Ile Pesa 126k. Hapo akaniona uchangamfu umepotea.

Nikamwambia ndîo, Kisha nikamuuliza why kuniuliza swali hilo. Akaniambia kama Hakuna tatizo Basi.
Nikatulia wewe.

Mwisho akafunguka kuwa,
Jana alituma mdada wa Kazi kuja kuweka Pesa Hapa kwangu. Na yeye humtumia huyo mdada, akawa anajaribu kunielekeza huyu Dada alivyo, pia huku akijaribu kuonyesha kuwa yeye NI mteja wàngu wa Muda mrefu. Nikamkumbuka Yule Binti.

Akasema alimuagiza niweke 14k kwèñye Namba Yake(boss aliyemtuma), akashangaa imeingia 140. Akajua nitakuwa nimekosea.

Akasema yeye NI mfanyabiashara Kariakoo anajua jinsi ilivyokuwa Kazi kupata hiyo faîda hasa Kwa biashara kama yàngu àmbayo mtaji ulikuwa Milioni tatu Mpaka tano.

Akaniambia, Moja ya mambo yaliyomfanya aje kunirudishia hiyo Pesa NI tàbia yàngu ya kuwahi kufungua Saa Moja na kuchelewa kufunga Saa nne maduka ya Eneo Hilo mengi yamekuwa yamefungwa.

Ati hicho ndicho Kilimpa Imani na kuingiwa na huruma ya Kurejesha hizô Pesa.

Nilimshukuru Sana. Tukawa marafiki na baadhi ya Mizigo nikawa nachukulia kwàke.
 
Kabisa mkuu uaminifu una tabia ya kufungua milango mingi ya neema , sitokaa nimdhulumu mtu hata mia mbovu .
 
Shida sio wewe maana hamna aliyeumbwa na roho mbaya, ni malezi, umasikini na matendo uliyotendewa na jamii ndio vimekushape hivyo
 
Na utakuta lijitu lilikula hela ya watu iliyotumwa kimakosa na akatafutwa ili airudishe kagoma kesho yake anaona mwizi kaiba anajifanya na yeye anahisira anaokata mawe anamrushia mwizi.
Sema wizi kuepuka kabisa?? makazini watu wanajiongeza sana na bado ni wizi, serikalini?

Maisha magumu hela haijawahi kutosha kama una moyo wa kukinai ni wachache sana
 
😁😁😁😁😁 wew ni nouma
kuna siku mwenzangu alitumiwa hela kimakosa bahat nzuri alikua anaezima sim ile kuwasha muamala unasoma ametumiwa laki na thrlathini na sita yan mm nilikua namwambia tuitoe tuile mwenzangu hapana sio vizur mpaka muamala ukarudishwa yan nikamwambia angekua n mm agekua hana bahati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…