Ustaarabu wa kurudisha miamala iliyokosewa

Ustaarabu wa kurudisha miamala iliyokosewa

Happy Saturday viongozi,

Kwanza tuweke swala moja bayana hali ni ngumuuu, aisee maisha ni tight naona sio kwa muajiriwa au mfanya biashara ila nisiongelee wengine sema kwa cycle yangu kila mtu analia noki nimegundua nina cycle ya ajabu ata nikitaka laki 5 ya chap sina wa kuniazima dah.

Twende kwenye mada, hivi na hali hii wazee umekaa zako unakuna P weekend hii mara msg:
View attachment 3083338

Hiyo pesa imetumwa kimakosa, baada ya dakika simu inaita kuombwa kurudisha muamala.

Ukweli kutoka moyoni, utarudisha? Au kutafutiana lawama?

Kalaga Baho Nongwa mzee wa micro finance apo vp?
kama ni siku ya marejesho, toa kiasi cha marejesho ya mkopo wako, then kua muungwana kinachobaki mrudishie mwambie kiasi kingine kimekatwa juu kwa juu na mtandao husika na kwamba ulikua unadaiwa, na haukua na namna nyingine ya kuzuia hilo 🐒
 
ku bargain na mtu utafikiri chako 😂, mstaarabu atakata hela ya kutuma tu kabda elf 10 ila njaa kali sisi ss
 
Mungu ananjia nyingi za kumpa mja wake. Nitashukuru Mungu kwa rizki kisha hela nahamishia laini nyingine, nafuta usajili wa laini na kuivunja kisha nafanya mambo yangu taratibu
 
Mimi Kuna pesa ilitumwa kimakosa ya mama mmoja wa lindi huko anatumia mtoto wake wa kike (mwanafunzi) Hela ya michango fln ya shule.

Hadi siku2 sijapigiwa simu na badae Nami nikatumiwa Hela kama 7000 Hivi nauli kutoka hapo nilipo niende mjini Bahati mbaya kipindi natoa sikuangalia Makato ikawa imekatwa Hela ya mama kama 200+ Hivi hivo ikawa imepungua Nami kipindi hicho Sina Hela hata mia mbovu ndo nimetoka veta somewhere..

Kwenyesaa12 nimefika mjini nikapigiwa simu na yule mama akajieleza sana nikamwambia nikweli niliona mama na Hela Yako ipo japo itapelea kidogo maana Nami nilitumiwa na mtu katika kutoa nikawa nimetoa na Hela Yako inapelea 200 na seti kadhaa.

Yule mama alifurahi sana ukumbuke kipindi kile anapiga alikuwa anataka kulia ananiomba kajieleza mnokuwa ni mjane na yule anamsomesha yeye....

Tukakubaliana nae kuwa nirudishe iliyopo nikamuomba naomba hiyo no nitume Moja Kwa Moja Kwa mhusika maana ikirudi itazidi kupungua.

Mama akanitajia Ile no nikaituma nilituma Moja Kwa Moja Kwa mwalimu yule bint alikuwa andvance.

Yule ticha akaniambia ubarikiwe sana kijana nayajua maisha ya huyu mama na binti huyu Yani umefanya kitu Cha maana mno!!

Badae mama ane nikampigia kumwambia Tyr na binti nimeongea nae ameipata yule mama alifurahi sana huwezi amini yule binti nilipewa😆😆

Japo sikuwahi hata kuja kuonana nae Hadi Leo. Tuliendelea kuwa na mawasiliano na mama Hadi binti yake aliporudi ndipo nikamwambia mama ameniambia nikuone asee hajakuambia huko?

Akacheka akasema Tena anasema Kila siku nikamwambia soma ipi siku tutaonana.

Mwisho wa yte jiwe ndo alinisababishia nikakoswa mke Kwa kufungia laini yangu kisa sikuwa na nida!!! Ila mwisho wa mawasiliano yetu.

Nilichojifunza hata iku Moja usile Hela ya kukoswa kutumwa acha hata kama una njaa kiasi Gani!!

Kuna ingine crdb walijichanganya badala ya kuniwekea m8 na laki1 wakaweka m81 pesa iliingia saa4 Hadi saa9 nikaendapo kuwaambia nikamkuta mhusika wamembana.
Bahati nzuri hata hiyo saa9 nilienda kuweka Hela cash maana nilikuwa wakala Tena nime ajiriwa tu kusimamia.

Baada ya kufika tu nikamwambia Hela mmeiwela kwangu kimakosa irudisheni haijatumika.

Nikawambia Mimi boss wangu Huwa ananiwekea Hela zake badae anazitoa pia (kuzipoza kabla ya kuanza kuweka float) hivyo nilijua ni yeye na sikumpigia simu nilikuwa busy.

Demu alinirukia kama mwehu akiwa na furaha kuu mnoo

Yule demu alikuwa anasema alikagua Kila slp lakni hakuona kosa alilolifanya ..
Tena wanasema hela ya mama ntilie ndo laana kali mtu anakukuruka sa 10 kuanza kupika unakimbia na buku jero yake
 
Mungu ananjia nyingi za kumpa mja wake. Nitashukuru Mungu kwa rizki kisha hela nahamishia laini nyingine, nafuta usajili wa laini na kuivunja kisha nafanya mambo yangu taratibu
Jambazi kubuhu 😂
 
Hapo Mimi nitamwambia anipe 10k akikubali sichukui. Akikataa nachukua kimabavu
Mkuu hauwezi kuichukua😄😄🤣🤣
Kuna siku manzi mmoja nilimwelewa, nikampa 'dokezo', akanambia haamini naonekana mjanja mjanja sana hivyo nimdhihirishie kwa kiapo, nikaapa.

Akanambia haamini hicho kiapo, vinginevyo niambatanishe na fedha mbichi, nikarusha 50k!

Akanijibu kuwa kiasi nilichorusha na muonekano wangu ni vitu viwili tofauti.. 'hela gani hiyo haitoshi hata kununua nyanya?...

Dah, kauli hiyo ilinijaza upepo nikazuia muamala dakika sifuri.

Aliendelea kuona hiko kivuli cha 50k kwa muda mrefu kila aangaliapo salio hadi siku alotaka kuitoa ndoakajiona mpumbafu!

Eti Oooh, ...'hautaniwagwi na wewe?'...
 
Hata aniombe simpi ng'ooo.

Tena ntamfurumusha kama PAKA MWIZI atajutRRa.

Naitoa hela naenda kula BIA na KUKU huku nakata uno kweRikweRi.

Uno la shangwe. Uno la PAKA-CHONGO.
Wizooo km Wizooo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo Mimi nitamwambia anipe 10k akikubali sichukui. Akikataa nachukua kimabavu
Mkuu hauwezi kuichukua😄😄🤣🤣
Kuna siku manzi mmoja nilimwelewa, nikampa 'dokezo', akanambia haamini naonekana mjanja mjanja sana hivyo nimdhihirishie kwa kiapo, nikaapa.

Akanambia haamini hicho kiapo, vinginevyo niambatanishe na fedha mbichi, nikarusha 50k!

Akanijibu kuwa kiasi nilichorusha na muonekano wangu ni vitu viwili tofauti.. 'hela gani hiyo haitoshi hata kununua nyanya?...

Dah, kauli hiyo ilinijaza upepo nikazuia muamala dakika sifuri.

Aliendelea kuona hiko kivuli cha 50k kwa muda mrefu kila aangaliapo salio hadi siku alotaka kuitoa ndoakajiona mpumbafu!

Eti Oooh, ...'hautaniwagwi na wewe?'...
 
Mie sijui sasa, na uzuri ilishawahi nitokeaa, 670k ziliingia kwenye Halopesa angu kimakosaa,

Niliacha km ilivyo, zikapita week 2 kimyaa, nkaunga bundle la 30k, ikabaki 640k.

Siku ya 2 yake, eti mtu ananipigia kunieleza kuna hela imeingia kwangu kimakosa, nkakubali na nlimuambia nimetumia 30k, akasema iliyobaki hiyo nirudishie, nkamrudishiaaa.
Kwa nilivyo na shida na pesa kwa sasa hivi hahaha itakuwa ndoto kumrudishia hata mia Tano hata hivyo hongera una moyo mzuri.
 
🤣🤣🤣 Leo naona hata wale wanaokimbia na hela za MGODI sijui NIVUSHE nao watasema wanarudisha hio milioni.
NIvushe na mgodi labda ukimbie kwa kuachana na line uitupe mbali huko.
Nakopa, nalipa, nakopa tena.
Hiyo riba inavyoongezeka usipolipa kwa wakati ni balaa
 
Back
Top Bottom