Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Hivi tatizo la wajinga wengi tanzania waliosoma na walioko maofisini ni tatizo la waalimu waliowafundisha au tatizo la mfumo wa elimu tuliourithi kutoka kwa wakoloni?
Watu walitabiri wajinga watakuja 1979
 
Mleta mada Ameuliza kama hiyo ndoto imetimia? Mi naona imetimia kwa yanayoendelea. Hii ni mada pana sana
 
Hiii mada ningewapa tips za kutosha sema wengi humu ni zao la UPE mtaanza kunishambulia tu bora nikae Kimya!
 
Kusoma ni jambo moja na akili nzuri ni jingine.
Tatizo kubwa ni jinsi ya kupata watu wenye akili nzuri,ili watumike kusaidia taifa lisonge mbele kwa ujumla.
Elimu haimuongezei mtu akili bali hunoa Ile iliyopo. Akili ni ya kuzaliwa/kurithi kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Inakuwa Bora zaidi sana kama mtu mwenye akili akapata elimu na ni afadhali pia kama asiye nayo akaenda shule.
Sasa, cha kufanya ni kuwatambua wenye akili miongoni mwa waliosoma kwa mustakabali mwema wa taifa.
Hata hivyo, kuna changamoto kubwa ya kupambana na wasio na akili ambao wameshatangulia kushika mpini wa panga lenye makali hatari.
 
Acha uzwazwa newton, Einstein ,bronsted wanajua kuandika huo upuuzi
 
Tafiti ni rahisi sana. Tatizo wanafunzi hawafundishi kufikiri mwalimu wao wa UPE anawakalilisha imetoka hiyo. Ndio maana wanafunzi wanashindwa kukariri wanafeli
Sasa wanafeli vipi wakati matokeo ya advance zaidi ya wanafunzi 50000 wamepata daraja la kwanza!?
 
Sasa wanafeli vipi wakati matokeo ya advance zaidi ya wanafunzi 50000 wamepata daraja la kwanza!?
Sasa si wanasahihishwa na wajinga wajinga waliyotabiriwa. Zamani kufaulu ilikuwa kugumu sana
 
Vigezo vya kuwachukua walimu toka kenya lilipigwa na kina Dr Gama KWA kigezo cha ujasusi wa kenya KWA tanzania uingereza walikubaliwa chini ya mpango wa VSO.
 
Hivi mwalimu ambae hajui logarithm anaweza kumfundisha mwanafunzi ajue vizuri kabisa.
Kwa mtazamo wako huyu mwalimu akifahamu logarithm ataweza kuwafaulisha wanafunzi wake wote????? (Shule ya kata iwe mfano)


Mfano wewe huo ufaulu wako unahisi unaweza ukawaambukiza wanafunzi wako wote???????

Usiendeshwe na hisia, papara,mhemko,hasira n.k unapojibu!!!!!!!!!!!!! Picha pana inatakiwa.
 
Nlifundishwa na walimu wa UPE baonana naye 1 saiz ni mkuu wa shulu ya msingi nawakumbuka2 mmoja alishastaaf na meingine still ni mwalimu. Aliyestaf alinifundisha chekechea na darasa la kwanza na la pili.
Huyu alikuwa ni best teacher sijawahiona katika maisha yangu. Na katika walimu nlifurahi kufundisha nao toka nimeanza kusoma ni huyu mwalimu.
Wa 2 huyu bado inservice huyu yeye alinifundisha darasa la 3 hadi la 7 hesabu huyu naye ni kati ya walimu wazuri kupata kutokea katika maisha yangu.
Wapo wengine wa UPE walinifundisha ila siwezi wasemea kwa sababu walikuwa wa kawaida sana.
Walimu wa sasa hivi tunawaona wanatoa hadi vijanaa hawajui kusoma na kuandika wanafika hadi form4 ila zaman hueziona kitu kama hicho
 
Kuna muda wa form four failure walienda kufundisha wenzao pia wa form six walienda kufundisha wenzao
 
Je Taifa la Sasa ni la watu wenye akili au wajinga
 
Tatizo halikuwa failures wa darasa la saba tu. Ualimu ni profession kama profession nyingine yoyote ile. Hao walimu wa UPE hawakupata training hata sekunde moja. Mbaya zaidi wengi wao wakapewa kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza which was worse. Kibaya zaidi idadi
ya wanafunzi kwenye darasa haikuzingatiwa. Standard class size ya shule za msingi ni wanafunzi 45. Hii ilizidi kwa hata mara mbili sababu hakukuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa. Kwa kifupi hakukuwa ba maandalizi ya kutosha kabla ya kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza. Ndiyo maana watu waliipa UPE maana yake halisi- Ualimu Pasipo Elimu. Hii yote ilisababishwa na ukweli kwamba wakati ule , lakini nafikiri mpaka sasa, ilkuwa ni one man show. Rais ndiyo anajua kila kitu. Hawezi kukosea. Lakini kinachosikitisha sana mpaka leo watu wanaamini hivyo. Ndiyo maana raus akikisolewa wapambe wake wanadai anatukanwa. Posts nyingi humu zinaonyesha hivyo.
 
Duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…