Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Hivi tatizo la wajinga wengi tanzania waliosoma na walioko maofisini ni tatizo la waalimu waliowafundisha au tatizo la mfumo wa elimu tuliourithi kutoka kwa wakoloni?
Watu walitabiri wajinga watakuja 1979
 
Umetoa mada nzuri sana mkuu, tatizo itakua diluted na vihiyo ambao ndio wengi humu, yes UPE ulikua mpango maalum ili wajinga na wapumbavu wawe wengi, royal families watoto wao hakusoma chini ya sera hii ya UPE, miaka michache iliyopita kukaletwa shule za sekondari za kata, hizi nazo zimetuletea wapumbavu zaidi, aliyeanzisha hili hata kitukuu chake hakijasoma huko, President Mugabe pamoja na ushenzi wake ulioua uchumi wa Zimbabwe, education systems aliyoirithi hakuigusa ndio maana hadi leo wazimbabwe ni hot cake kielimu, President Kagame kafuata waalimu Zimbabwe katuluka sisi, UK hadi leo wazimbabwe (nurse's)wanapewa working visa kirahisi, hapa tuna Doctors wapo mitaani!wanakimbiza viajira uchwara
Mleta mada Ameuliza kama hiyo ndoto imetimia? Mi naona imetimia kwa yanayoendelea. Hii ni mada pana sana
 
Hiii mada ningewapa tips za kutosha sema wengi humu ni zao la UPE mtaanza kunishambulia tu bora nikae Kimya!
 
Je hili ndio Taifa la wajinga lililotabiriwa mwaka 1977 wakati walipoanzisha sera ya Elimu ya Universal Primary Education UPE?

Katika sera ya nchi ya kutoa elimu kwa wote. Serikali ilipanga kutoa elimu kwa watanzania wote bila ubaguzi wowote. Serikali ilikuja na mpango elimu ya msingi iwe ni razima kwa kila mtanzania.

Katika Bunge la wakati ule viligubikwa na wasomi wachache sana.
Wapinzani wa sera kipindi kile walionekana mwiba sana kwa Serikali.
Wasomi wengi walishauri kuajiri waalimu kutoka nchi ya Kenya na nchi kama uingereza na mataifa mengine Walikuwa tayari kutoa waalimu. Ili kufanikisha mpango huu.

Hatimaye Bunge likaja na mpango wa UPE (Universal Primary Education) yaani wahitimu failure wa elimu ya msingi kwenda kuwafundisha wenzao.
Wasomi chuo kikuu cha Dar es salaam waligomea huu mpango kabisa. Sababu ilikuwa Tanzania inatengeneza Taifa la watu wajinga sana.

Sasa hivi wale walioanza kufundishwa na walimu wa UPE wanamiaka 50 mpaka 55. Je Taifa letu ni la watu wenye akili ama wajinga kama ilivyotabiriwa?
Kusoma ni jambo moja na akili nzuri ni jingine.
Tatizo kubwa ni jinsi ya kupata watu wenye akili nzuri,ili watumike kusaidia taifa lisonge mbele kwa ujumla.
Elimu haimuongezei mtu akili bali hunoa Ile iliyopo. Akili ni ya kuzaliwa/kurithi kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Inakuwa Bora zaidi sana kama mtu mwenye akili akapata elimu na ni afadhali pia kama asiye nayo akaenda shule.
Sasa, cha kufanya ni kuwatambua wenye akili miongoni mwa waliosoma kwa mustakabali mwema wa taifa.
Hata hivyo, kuna changamoto kubwa ya kupambana na wasio na akili ambao wameshatangulia kushika mpini wa panga lenye makali hatari.
 
Ukitaka kuharibu future ya taifa lolote duniani huna haja ya kutumia bunduki au mabomu ya maangamizi Cha kufanya chezea mfumo wa elimu na mwisho utakuja kuona matokeo yake miongo kadhaa ni ajabu unakutana na kijana kahitimu kidato Cha Nne na kupata Cheti alafu hajui kuandika Insha sasa unajiuliza alifaulu vipi?
Acha uzwazwa newton, Einstein ,bronsted wanajua kuandika huo upuuzi
 
Tafiti ni rahisi sana. Tatizo wanafunzi hawafundishi kufikiri mwalimu wao wa UPE anawakalilisha imetoka hiyo. Ndio maana wanafunzi wanashindwa kukariri wanafeli
Sasa wanafeli vipi wakati matokeo ya advance zaidi ya wanafunzi 50000 wamepata daraja la kwanza!?
 
Sasa wanafeli vipi wakati matokeo ya advance zaidi ya wanafunzi 50000 wamepata daraja la kwanza!?
Sasa si wanasahihishwa na wajinga wajinga waliyotabiriwa. Zamani kufaulu ilikuwa kugumu sana
 
Vigezo vya kuwachukua walimu toka kenya lilipigwa na kina Dr Gama KWA kigezo cha ujasusi wa kenya KWA tanzania uingereza walikubaliwa chini ya mpango wa VSO.
 
Hivi mwalimu ambae hajui logarithm anaweza kumfundisha mwanafunzi ajue vizuri kabisa.
Kwa mtazamo wako huyu mwalimu akifahamu logarithm ataweza kuwafaulisha wanafunzi wake wote????? (Shule ya kata iwe mfano)

Mfano wewe huo ufaulu wako unahisi unaweza ukawaambukiza wanafunzi wako wote???????

Usiendeshwe na hisia, papara,mhemko,hasira n.k unapojibu!!!!!!!!!!!!! Picha pana inatakiwa.
 
Nlifundishwa na walimu wa UPE baonana naye 1 saiz ni mkuu wa shulu ya msingi nawakumbuka2 mmoja alishastaaf na meingine still ni mwalimu. Aliyestaf alinifundisha chekechea na darasa la kwanza na la pili.
Huyu alikuwa ni best teacher sijawahiona katika maisha yangu. Na katika walimu nlifurahi kufundisha nao toka nimeanza kusoma ni huyu mwalimu.
Wa 2 huyu bado inservice huyu yeye alinifundisha darasa la 3 hadi la 7 hesabu huyu naye ni kati ya walimu wazuri kupata kutokea katika maisha yangu.
Wapo wengine wa UPE walinifundisha ila siwezi wasemea kwa sababu walikuwa wa kawaida sana.
Walimu wa sasa hivi tunawaona wanatoa hadi vijanaa hawajui kusoma na kuandika wanafika hadi form4 ila zaman hueziona kitu kama hicho
 
Kuna muda wa form four failure walienda kufundisha wenzao pia wa form six walienda kufundisha wenzao
 
Nlifundishwa na walimu wa UPE baonana naye 1 saiz ni mkuu wa shulu ya msingi nawakumbuka2 mmoja alishastaaf na meingine still ni mwalimu. Aliyestaf alinifundisha chekechea na darasa la kwanza na la pili.
Huyu alikuwa ni best teacher sijawahiona katika maisha yangu. Na katika walimu nlifurahi kufundisha nao toka nimeanza kusoma ni huyu mwalimu.
Wa 2 huyu bado inservice huyu yeye alinifundisha darasa la 3 hadi la 7 hesabu huyu naye ni kati ya walimu wazuri kupata kutokea katika maisha yangu.
Wapo wengine wa UPE walinifundisha ila siwezi wasemea kwa sababu walikuwa wa kawaida sana.
Walimu wa sasa hivi tunawaona wanatoa hadi vijanaa hawajui kusoma na kuandika wanafika hadi form4 ila zaman hueziona kitu kama hicho
Je Taifa la Sasa ni la watu wenye akili au wajinga
 
Kwa mtazamo wako huyu mwalimu akifahamu logarithm ataweza kuwafaulisha wanafunzi wake wote????? (Shule ya kata iwe mfano)

Mfano wewe huo ufaulu wako unahisi unaweza ukawaambukiza wanafunzi wako wote???????

Usiendeshwe na hisia, papara,mhemko,hasira n.k unapojibu!!!!!!!!!!!!! Picha pana inatakiwa.
Tatizo halikuwa failures wa darasa la saba tu. Ualimu ni profession kama profession nyingine yoyote ile. Hao walimu wa UPE hawakupata training hata sekunde moja. Mbaya zaidi wengi wao wakapewa kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza which was worse. Kibaya zaidi idadi
ya wanafunzi kwenye darasa haikuzingatiwa. Standard class size ya shule za msingi ni wanafunzi 45. Hii ilizidi kwa hata mara mbili sababu hakukuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa. Kwa kifupi hakukuwa ba maandalizi ya kutosha kabla ya kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza. Ndiyo maana watu waliipa UPE maana yake halisi- Ualimu Pasipo Elimu. Hii yote ilisababishwa na ukweli kwamba wakati ule , lakini nafikiri mpaka sasa, ilkuwa ni one man show. Rais ndiyo anajua kila kitu. Hawezi kukosea. Lakini kinachosikitisha sana mpaka leo watu wanaamini hivyo. Ndiyo maana raus akikisolewa wapambe wake wanadai anatukanwa. Posts nyingi humu zinaonyesha hivyo.
 
Samahani mleta mada, naomba unipe uhusiano wa wewe kufaulu na uhusiano wa kumfaulisha mwingine kwa kiwango kilekile. Namaanisha hivi:

Wewe umepata daraja la kwanza, kwa maana hiyo ukiwa mwalimu utakuja kuwafaulisha wanafunzi wako kwa kiwango kama chako!!!!!!!!!!

Namaanisha hivi tena:

Walimu wanaoajiriwa wawe wamepata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza (mtazamo wenu) hivyo wanafunzi wao wote (shule za kata) watafaulu kama wao.

UDSM, SUA, MZUMBE na UDOM kwa Tanzania hivi ni vyuo vikubwa, kuna shahada mbalimbali za elimu zinatolewa huko. Katika vigezo vyao vya udahili unadhani walimu kutoka hivi vyuo wanaufaulu mdogo??? (mtazamo wenu)

Jibu kwa kutumia picha pana na siyo mhemko, papara na hasira!!!!!!!!!!!!!!

Nb: Walimu ni sehemu ndogo sana ya tatizo, nashangaa wanavyotupiwa mzigo wa lawama pamoja na kujitahidi kwao katika mazingira magumu ya kazi!!!!!!!!!!!

Eti wamefeli!!!!!!!!!!!Halafu ukipata watoto unampelekea akufundishie!!!!!!!!!!!!!!!!!Iwe shule binafsi au ya umma bado utawakuta!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ahsanteni sana walimu kwa mchango wenu!!!!!!!!!!!!
Duh
 
Back
Top Bottom