Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Wewe ni mjinga

Nasema hivyo kwa sababu wewe unaitwa ndege ilihali mtu aliyelimika anajua moja kati ya siya ya ndege ni kujongea kwa mabawa na wewe mabawa huna, hivyo kujiita ndege wakati wewe sio ndege ni justification ya ujinga wako
Je,kama katumia taswira?
 
Je hili ndio Taifa la wajinga lililotabiriwa mwaka 1977 wakati walipoanzisha sera ya Elimu ya Universal Primary Education UPE?

Katika sera ya nchi ya kutoa elimu kwa wote. Serikali ilipanga kutoa elimu kwa watanzania wote bila ubaguzi wowote. Serikali ilikuja na mpango elimu ya msingi iwe ni lazima kwa kila mtanzania.

Katika Bunge la wakati ule viligubikwa na wasomi wachache sana.
Wapinzani wa sera kipindi kile walionekana mwiba sana kwa Serikali.
Wasomi wengi walishauri kuajiri waalimu kutoka nchi ya Kenya na nchi kama uingereza na mataifa mengine Walikuwa tayari kutoa waalimu. Ili kufanikisha mpango huu.

Hatimaye Bunge likaja na mpango wa UPE (Universal Primary Education) yaani wahitimu failure wa elimu ya msingi kwenda kuwafundisha wenzao.
Wasomi chuo kikuu cha Dar es salaam waligomea huu mpango kabisa. Sababu ilikuwa Tanzania inatengeneza Taifa la watu wajinga sana.

Sasa hivi wale walioanza kufundishwa na walimu wa UPE wanamiaka 50 mpaka 55. Je Taifa letu ni la watu wenye akili ama wajinga kama ilivyotabiriwa?
Tumeanza tena kuwasingizia waalimu hebu tuwapumzishe. Hao Walimu tunaowabeza wengi tunawakumbuka hadi Leo.
 
Je Taifa la Sasa ni la watu wenye akili au wajinga
Ukiwemo na wewe mkuu usijisahau. Walimu wa zaman walikuwa wanaheshimika s ana hebu linganisha na wa sasa waliokopa hadi wanapokea negative balance kwenye mshahara
 
Tatizo halikuwa failures wa darasa la saba tu. Ualimu ni profession kama profession nyingine yoyote ile. Hao walimu wa UPE hawakupata training hata sekunde moja. Mbaya zaidi wengi wao wakapewa kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza which was worse. Kibaya zaidi idadi
ya wanafunzi kwenye darasa haikuzingatiwa. Standard class size ya shule za msingi ni wanafunzi 45. Hii ilizidi kwa hata mara mbili sababu hakukuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa. Kwa kifupi hakukuwa ba maandalizi ya kutosha kabla ya kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza. Ndiyo maana watu waliipa UPE maana yake halisi- Ualimu Pasipo Elimu. Hii yote ilisababishwa na ukweli kwamba wakati ule , lakini nafikiri mpaka sasa, ilkuwa ni one man show. Rais ndiyo anajua kila kitu. Hawezi kukosea. Lakini kinachosikitisha sana mpaka leo watu wanaamini hivyo. Ndiyo maana raus akikisolewa wapambe wake wanadai anatukanwa. Posts nyingi humu zinaonyesha hivyo.
Unayeongea wewe sio mwalimu. Hakuna mwalimu asiye mzoef hufundisha la 1 hadi la 3 madarasa yote haya hufundishwa na walimu nguli wenye uzoef na kazi sababu elimu yote iliyobakia hadi phd hutegemea msingi wa KKK.
 
Ndugu, unaweza kuthibitisha hiki???? Usifuate mkumbo, kama hujui kitu jaribu kuuliza,kudadisi na kujifunza!!!!!!!!!!!!!!
Bado mtoto mkuu mwache tu. Hao wa upe kuna wengine ni maprofessor kwa sasa
 
Walifundisha,unadhani waliofeli mitihani ya la Saba 1970s-90s walikua hawawezi masomo!?..palikua na msemo 'kafaulu lakini hakuchaguliwa'..na Mara nyingi waliofaulu siyo wale waliokua na uwezo,palijaa ukiritimba,lakini hao walimu wa upe wanafunzi wao walikua imara kimasomo,hakuna aliyetoka darasa la pili kwenda la tatu na hajui kusoma,kuandika,kuhesabu,kujumlisha na kutoa,unasema wenye advance diploma/degrees wakafundishe primary...unadharau Sana level za elimu,hao wanatakiwa kufundisha a level na certificates vyuoni
Okay mkuu tusibishane sana maana kuna gap kubwa kati yetu ya ufahamu, soma hili, huwezi kufundisha hizi private primary schools hapa Tanzania kama una level ya certificate, let's agree to disagree, thanks
 
Okay mkuu tusibishane sana maana kuna gap kubwa kati yetu ya ufahamu, soma hili, huwezi kufundisha hizi private primary schools hapa Tanzania kama una level ya certificate, let's agree to disagree, thanks
Hao wafanyabiashara,elimu ya msingi ya tz haihitaji mtu mwenye degree kufundisha,hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali,Kuna elimu gani msingi!?
 
Mimi naona tatizo sio waalimu .Tatizo ni mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana.Hata hao waalimu Bora mnaowataka wangeeda kufundisha nn? Wakafundishe panzi ana miguu mingapi? Wakafundishe miji mikuu? Wakafundishe hesabu za umri?.Tukubali mtaala wetu hauna msaada Kwa watoto.Mtaala wetu unafundisha utambuka tu. Jua elimu mtambuka ni elimu ambayo mtu yeyote anawezapata hata km hajaenda shule.Ni elimu inaypatikana Kwa kupitia warsha ,vyombo vya habari na pia usomaji was vitabu na mitandao.Tunawapotezea watoto muda fikiri moto anasoma miaka 2,7,4,2.jumla miaka 15 yupo tu darasani na hajui anasoma nn zaidi yakukariri. Mtoto kaingia miaka 7 +15=22 ni mateso Kwa mzazi na pia Kwa mtoto.Hapo hatoki na ujuzi.Ndio kwanza akasomee ujuzi. Kwaumri huo ameshaanza mambo ya utu uzima tamaaza kuwa na maisha mazuri imeshamfikia .Matokeo yake ule ubunifu tuliotegemea kwake unafifia.Mtoto mdogo hupenda kujifinza ujuzi sio mambo mtambuka.Leo hii wenye Hela hupeleka watoto wao wakasomee mtaala was nje huu wa ndani hawaitaki maama ni mzigo.Je hapo alaumiwe nani? Madarasa yenyewe yapo full watoto zaidi ya 70 darasani Vitenda KAZI km zana na vitabu hakuna.Madawti hakuna watoto wanakaa chini ,wanafunzi 800 waalimu 6 Unafundishaje? Mishahara duni .Kila siku kilio.Leo unataka aliepata div 1$2 wawe waalimu watakubali kweli Kwa mazingara km haya ya mishara duni na mazingira magumu ambayo hayana maji ,umeme na hata nyumba Bora za kuishi.Ni wakati Sasa kupaza sauti mtaala ufumuliwe uletwe mtaala ambayo unakidhi Kwa walengwa.Tusiwalaumu waalimu wanafanya KAZI nzuri.
 
Sababu za elimu yetu kuwa duni ni nyingi sana. Hao waalimu wa UPE siwezi kuwalaumu hata kidogo kwa kuwa 1977 bado nchi ilikuwa changa. Kuna hii crash program ya mwaka 2006 na 2007 ndo ilikuwa ya hovyo zaidi. Wahitimu wa kidato cha sita walienda kozi ya mwezi mmoja na kudaka ajira.
 
Walifundisha,unadhani waliofeli mitihani ya la Saba 1970s-90s walikua hawawezi masomo!?..palikua na msemo 'kafaulu lakini hakuchaguliwa'..na Mara nyingi waliofaulu siyo wale waliokua na uwezo,palijaa ukiritimba,lakini hao walimu wa upe wanafunzi wao walikua imara kimasomo,hakuna aliyetoka darasa la pili kwenda la tatu na hajui kusoma,kuandika,kuhesabu,kujumlisha na kutoa,unasema wenye advance diploma/degrees wakafundishe primary...unadharau Sana level za elimu,hao wanatakiwa kufundisha a level na certificates vyuoni
Je lile Taifa la wajinga limekuwa?
 
Back
Top Bottom