Utabiri: Kagame kuchukua Eastern Congo, Kabale, Burundi, Kagera na Kigoma miaka ijayo

pole sana, nakuonea huruma kwasababu hauifahamu vizuri Tanzania, kagame mwenyewe anaielewa hata akipatwa na ukichaa hili ninaouhakika hawezi kulifanya
 

PK anamiaka mingapi sasa?

Unafikiri Mtu hazeeki?

Kama ameshindwa sasa akiwa na nguvu unategemea ataweza miaka mitaji ijayo ambayo nguvu zinazidi kufifia?
 
Namtakia kila laheri kwenye huo upanuzi wa himaya yake.
 
Pk akilianzisha hatupotezi muda kutumia majeshi yetu panya road tu wanaiteka mpk ikulu na Rwanda yote.
 
Kwa hiyo umemtabiria kwamba umri wake utakiwa miaka 1000 pia!
 
jf siku hizi haina taarifa zenye uhalisia bali imejaa watabiri walioshiba maandazi na chai halafu wanakuja kutupotezea bundle na just imagine sasahivi gharama za internet zimepanda ukigusa kidogo unashangaa kuambiwa bundle lako limeisha.
 
Kama sud Kivu tu ina mshinda atawezaje kuchukuwa eneo lote hilo

Wakongo hatujaamua kwenda kufanya upumbavu uko kwenu
 
Shida vijana wanakariri tu hawana uwezo wa kuchunguza mambo kwa kina, kwa ufupi Rwanda ni Taifa ambalo hawana uwezo wa kuanzisha vita dhidi ya Tanzania, unapaswa ujue taifa la Rwanda hadi kesho halina amani wala utulivu, kilichomo ndani ya Rwanda ni utiifu kwa Kagame kwani wapinzani wake amekuwa akiwaminya hadi kuwanyima haki ya kuishi. Rwanda inao maadui wakubwa sana ambao ni raia wake chini ya utawala wa Kagame wanyarwanda hawaaminiani kamwe. Lakini kwa taarifa zaidi unapaswa ujue nje na KIGALI maisha ya Rwanda Ni magumu mnoo. Msipende kuishia vijiweni na kuishia mijini bali zama ndani mpate uhalisia wa maisha.
 
Soma kitabu cha alfu lela humo kuna hadithi nyingi za kufurahisha sana.Mojawapo ni ndoto ya mchana naamini utaipenda hiyo simulizi.
 
Atachukua yote uliyosema Ila hatochukua mawili ya mwisho
 
Mbona Kagera kachelewa sana kuichukua. Wale si wenzetu Iddy Amini alibughi kidogo, vinginevyo watu wake angewatwaa.
Sio wenzenu kivipi. Kambi ya jeshi ya Kaboya inatosha kuisambaratisha Rwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…