UTABIRI: Kuna uwezekano mechi ya Simba na Yanga ikaahirishwa

UTABIRI: Kuna uwezekano mechi ya Simba na Yanga ikaahirishwa

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau

Tukumbuke tarehe 25/07/2021 kutakuwa na mechi kati ya Simba na Yanga utabiri wangu unanambia hii mechi inaweza isichezwe.

Sababu ni hali ya Corona nchini iwapo serikali kupitia wizara itaamua kuchukua tahadhari zaidi kuzuia maambukizo, ukizingatia mechi itapigwa Kigoma ambako rate ya maambukizi kandokando ya nchi ipo juu kuliko maeneo ambayo hayapo mipakani.

Kiashiria: Ugomvi wa Manara na viongozi wake na maboss wake wa Simba pia kutakuwa na hoja kubwa itakayo ibuka itakayopelekea timu moja kutoingia uwanjani kwa sababu za kudai kuwa wanahujumiwa.
 
Hiyo mechi iarishwe tu, maana italeta vurugu kwenye club ya simba endapo itafungwa, yule msemaji wao kajiweka pabaya kwa ku-react negativelly kwenye mzozo wao. Suluhu ni simba kushinda tu hiyo mechi itatuliza mambo klabuni.
 
Hiyo mechi iarishwe tu, maana italeta vurugu kwenye club ya simba endapo itafungwa, yule msemaji wao kajiweka pabaya kwa ku react negativelly kwenye mzozo wao. Suluhu ni simba kushinda tu hiyo mechi itatuliza mambo klabuni.
Nakukatalia mapema kabisa, Simba tukufungwa hiyo mechi haiwezi kuleta vurugu abadan. Haji ni mjinga hata wanasimba washamjua kuwa anatumika, mechi ikiisha anashughulikiwa na Simba kama club itaendelea na malengo yake, kumbuka Simba ya sasa inauongozi makini na mashabiki wa Simba pia wameshapevuka.
 
Wakuu kwa kinachoendelea kuhusu Covid 19, chonde chonde naiomba serikali yetu sikivu iufute huu mchezo au kama unachezwa uchezwe kusiwe na mshabiki hata mmoja uwanjani

Naandika huku naogopa kwa kinachoendelea kuhusu covid 19 nchini hali ni Mbaya mnooo

Uhai ni bora kuliko huu mchezo wana kigoma wanaenda kuumia kama ilivyo Mwanza sasa hivi

Serikali futeni huu mchezo hali sio nzuri na kingine watu hawavai barakoa

Asante
 
Team zicheze bila mashabiki tuangalie kwenye tv tu na sio kufuta mchezo kabisa
Tumeshakata tiketi Tangu Jumatano na Zinaendelea kuuzwa.. Nina tiketi yangu ya TSH 30,000 unadhani ni rahisi kurudisha pesa?
JPEG_20210723_123726_2306680629824792970.jpg
 
Wakuu kwa kinachoendelea kuhusu Covid 19 ,chonde chonde naiomba serikali yetu sikivu iufute huu mchezo au kama unachezwa uchezwe kusiwe na mshabiki hata mmoja uwanjani...
Mkuu embu tuambie kuna ndugu yako yeyote ndani ya ukoo wenu umesikia amefariki kwa virus vya covid 19 Au tu kuumwa? Au kuna rafiki yako yeyote umesikia kakutwa na hiyo covid 19?

Tusiseme hali ni mbaya halafu hatuoni hali yoyote utafikiri hao wagonjwa tunaoaminishwa wapo hawapatikani uraiani mwetu. Watu wanaenda kariakoo na misongamano kila siku na tunawaona wanadunda tu.

Embu wewe uwe wa kwanza kutuambia mgonjwa uliyemsikia katika eneo lako
 
Serikali imefanya vizuri sana kuzuia misongamano.

Hata hii mechi izuiwe ili kuwakinga watu wasipate corona maana hali huko duniani ni mbaya sana na nadhani ni wakati wa serikali kuchukua hatu dhidi ya hii mikusanyiko ya namna hii
 
Back
Top Bottom