Utabiri: Odinga anaenda kushinda Urais

Utabiri: Odinga anaenda kushinda Urais

Truths

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
1,494
Reaction score
1,504
Sikuzote watu wanaweza wakamkataa mtu fulani, lakini wako watakao shawishika na watu wengine kulingana na mazingira yanavyojionyesha.

Swali wanalojiuliza ni kwanini watu wengi wamemkubali Odinga? Hapa dalili za Odinga kuthaminishwa huanza kujitokeza.

Mfano hapa Tanzania, kuna watu walimkataa Lowasa na Upinzani mwanzoni, wakijiaminisha kua wao wanaiunga mkono CCM chama cha Nyerere.

Hata hivyo baada ya Ngoma yake kulia na kuchezwa sana kila mahali, watu wale wakajikuta wanaanza kumthaminisha na wanamuimba kuliko wimbo wa [HASHTAG]#Seduce[/HASHTAG] me wa ali kiba.

Tukirudi Kenya:-
Kwa hapa utaona Odinga amejenga mvuto na Ngoma yake inachezeka zaidi kwasababu Mahakama imeamua positive juu yake.
Mamuzi ya mahakama yanatoa Picha kwa wakenya kua Odinga ndiye anayependwa na ndiye alieshinda Uchaguzi na si Kenyatta.

Na hapa utaona, hata waliomkataa wataanza kumfikiria kua anafaa. Kwavile tu Mahakama ilimpa ushindi.

Watamchukulia Odinga kama mtenda Haki kwasababu mahakama ilimpa Haki. Na kinyume chake kwa Kenyatta ambaye alipoteza.

Hii ni dalili kua Odinga anakwenda kushinda U-Raisi ndani ya siku 60 zijazo

Hata hivyo wako wanaopingana na nadharia hii wakidai wakenya wana ukabila sana, hivyo zamu hii yale Makabila Tawala watahakikisha Odinga hashindi.

Jibu langu:- Nadhani sikuzote wako watu wasiofungamana na upande wowote hata ndani ya makabila Tawala. Hawa ni wale "swing". Wana sway anywhere..kulingana na wanachokifikiri wao.
Hawa wana uwezekano wakakaa upande wa Odinga zaidi.


2. Na rekodi za wananchi wa kenya zinaonyesha hawana Tabia ya kumtaka mtu aongoze Awamu 2 za Uraisi.mfano walimkataa Mwai kibaki dhidi ya Odinga kwenye uchaguzi wa Pili.

3. Inawezekana ikawa Ni kweli kua, Kenyatta aliashindwa Uraisi. Kama asingeiba asingeibuka mshindi..mnakumbuka yule jamaa aliekufa ghafla.


Zipo dalili kua wameshamkataa Kenyatta na jubilee yake.

4. Matokeo ya wabunge Jubelee inaongoza dhidi ya NASA ya Odinga, hata hivyo kama ni kweli wakina Kenyatta walichakachua matokeo kwa mujibu wa mahakama. Hii ina maana kua wingi wa wabunge wa Kenyatta hauwezi kumsaidia.

Nawasiliasha...


Updated

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tehe tehe tehe sitaki ushahidi ila kutoka source inayoaminika wamemtoa roho ili watumie kiganja chake kwenye acess zake ICT
Hata tukisema kweli walimuua bwana Msando,je,tunafahamu ni upande upi uliomuua? Je,Msando alikuwa na upande katika wagombea? Maadili ya kazi yake yanamruhusu kulalia upande? Kama jibu ni hapana,je,ni nani waliomuua bwana msando ? Hii damu yake itamtokea nani puani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama figisu hazitatatumika naungana na wewe kuwa Odinga atashinda. Odinga ababebwa na yafuatayo;-
-unga crisis
-unemployment crisis (japo siyo kosa la Uhuru)
-na sasa maamuzi ya mahakama (kama ulivyogusia)

Lkn Uhuru kwa namna alivyombwatukia jaji mkuu ndg Maraga. Sijui..!!!
 
Kama figisu hazitatatumika naungana na wewe kuwa Odinga atashinda. Odinga ababebwa na yafuatayo;-
-unga crisis
-unemployment crisis (japo siyo kosa la Uhuru)
-na sasa maamuzi ya mahakama (kama ulivyogusia)

Lkn Uhuru kwa namna alivyombwatukia jaji mkuu ndg Maraga. Sijui..!!!
Kwani jaji Maraga ndo mpiga kura mkuu? Kwani jaji Maraga ndo IEBC? Odinga hashindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Urasi wa kenya nadhani ni vita ya System kati ya Kenya na jirani yake so System ya Kenya haitakubali kuona Raila ameshinda maana itakuwa kama wamekuwa uchi kwa System ya Jirani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona maalim seif hamshauri kenyetta agomee uchaguzi?
 
Hii ni dalili kua Odinga anakwenda kushinda U-Raisi ndani ya siku 60 zijazo

Hata hivyo wako wanaopingana na nadharia hii wakidai wakenya wana ukabila sana, hivyo zamu hii yale Makabila Tawala watahakikisha Odinga hashindi.

Jibu langu:- Nadhani sikuzote wako watu wasiofungamana na upande wowote hata ndani ya makabila Tawala. Hawa ni wale "swing". Wana sway anywhere..kulingana na wanachokifikiri wao.
Hawa wana uwezekano wakakaa upande wa Odinga zaidi.
Kwa ukabila wa Kenya, hakuna swing kwenye ukabila huo bali kinachofanyika ni kitu kinachoitwa diffusion, kwa kila kambi kuwaweka watu wa dominant tribes with solid promises za kuja kushika madaraka fulani iwapo fulani atashinda.
Hii maana yake ili Odinga apate kura ya Mkikuyu, ni lazima kwenye line up awe na Mkikuyu mwenye ahadi ya kuwa PM, Spika, CJ au waziri wwizara muhimu.

Huu ukabila wa Kenya huko tuendako sisi Tanzania pia ndio tunauanza, na mimi niliuzungumzia sana humu
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! | Page 4 ...
Makabila makubwa vs Makabila madogo | JamiiForums | The Home of ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...


Tumeishaanza kidogo kidogo, determinant ya nani anashinda urais wa Tanzania, inaamuliwa na Kanda ya Ziwa, hivyo tumeishaanza anza kupiga chapuo
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana ...

Udini, Ukanda na Uksabila ni sumu mbaya sana, hatuwezi kuipiga vita kwa denial kuwa haipo Tanzania, ipo, dawa ni kui contain na kui diffuse!.
Paskali




 
Back
Top Bottom