Dogo kataa usikatae,pamoja na kwamba Real Madrid haiko vizuri sana,lakini ikifika hatua kama hizi huwa inalitolea macho kombe hatari. Na kama ulivyosema,akiingia tu final hesabu maumivu kwa PSG. Sijui kuuchambua mpira ila najua kabisa Madrid wakifika hatua kama hizi usiwaguseHabari.
Hadi sasa zimebaki timu nne ambazo zitacheza hatua ya nusu fainali na ratiba:
Leg 1.
27 April 2021 Tuesday
Paris Saint Germain Vs Manchester City
Real Madrid Vs Chelsea
Leg 2.
04 May 2021 Tuesday
Manchester City Vs Paris Saint-Germain
Chelsea Vs Real Madrid
Hapo bila kupepesa macho mpira anaocheza Paris Saint Germain dhidi ya kocha wao Pochettino umekuwa na nidhamu ya kutafuta matokeo tu hakuna kingine.
Hivyo basiasi ubishe usibishe Paris Saint Germain atakuwa Champion wa ligi ya mabingwa ulaya.
Final itachezwa 29 May 2021 Ataturk Olympics Stadium.
Final itakuwa ni Paris Saint Germain Vs Real Madrid na bingwa atakuwa Paris Saint Germain.
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
Cc: Kichwa Kichafu
Kwa sasa Real Madrid huo uwezo umekwisha kiongozi ukimlinganisha kwa PSG.Utabiri wako ni kama nauelewa japo moyo unauma natamani Real Madrid wabebe
Kama ulimuangalia vizuri mwaka jana Man city wakati anatoka ungesema alikosa nini hasa?Mkuu man city ndio bingwa
Hahahah nakumbuka vyema sana ilikuwa ni quarter final.Mtabiri umekumbuka uefa nusu final spurs na city ,hahaaaa
Cr 7 alikuwa na mchango mkubwa kwa kipindi chote hicho ulichokisema boss.Real Madrid asingekuwepo sawa, Yaani hao jamaa wakifika hatua hiyo wanakuwa hatari kuliko stage za awali.....wanasenior players ambao hawahitaji motivation, wanajiongoza wenyewe na watabeba ndoo
Huyo anaongea kwa sababu mapenzi ya timu yamezidi uhalisia wake.Kwenye soka lolote linaweza kutokea na hutakiwi kubeza.
Kuna mwana kakomaa kabisa anakwambia piga uwa Chealsea anabeba ubingwa,na ukimbishia anakwambia minaweka laki moja wewe weka kishkizo cha shati.
Tuchel alikuwa PSG pia. Pia angalia upo wa timu yako na PSG.Msiichukulie poa Chelsea ya Tuchel. Yule Tactician na yeye ni mzee wa kutafuta matokeo.
Si ya sasa.Madrid ni Madrid tu mkuu
Huyo Tuchel alikuwa na PSG yenye kikosi bora zaidi ya hicho alichonacho.Chelsea anakwenda kama DARK HORSE,Big Ears inakwenda Stamford Bridge msimu huu!!
Mwaka huu upepo upo upande wa PSG.Utabiri mzuri lakin PSG wazidi kuombea njaa kikosi cha madrid kiendelee kuwakosa nyota wake muhimu kama watakutana fainali.
Ogopa team yenye uwezo wa kutengeneza chance nyingi pia.PSG hii inayopata chansi 15 za wazi wanafunga moja?
Si rahisi ila ndicho kinachoenda kutokea kiongozi.Si rahisi
Huyo Tuchel alikuwa na PSG yenye kikosi bora zaidi ya hicho alichonacho.
Hakikuwa bora sana kama cha Bayern Munich. Hata kwenye final match kama uliangalia Bayern alishinda kwa mbinde sana.Huyo Tuchel alikuwa na PSG yenye kikosi bora zaidi ya hicho alichonacho.
Cr 7 alikuwa na mchango mkubwa kwa kipindi chote hicho ulichokisema boss.
Ila mpira dk 90.
Hiyo hiyo iliyopitia tundu la sindano mpaka kufikia hapo ilipoSi ya sasa.
Chelsea itawashangaz wengi msimu huu. Kaeni hivyo msubiri maajabu.Kwa mara ya kwanza kabisa nafanana mtazamo na mbumbumbu fc!!
Naunga mkono hoja.
Natamani sana chama langu la Chelsea libebe ndoo mwaka huu! Ika tatizo lake lina watoto wengi wa chekechea na ina washambuliaji butu ukilinganisha na wakongwe wa Real Madrid, PSG na Man City.
Alikosa bahatiKama ulimuangalia vizuri mwaka jana Man city wakati anatoka ungesema alikosa nini hasa?
Huyo PSG mwaka jana tu alicheza fainali na kikosi chake ila uzoefu na pressure iliwakwamisha japo walicheza vizuri sana na Bayern Munich alishinda kwa mbinde tunaweza sema.Alikosa bahati
Na alikosa uzoefu wa kimashindano
Kwa mwaka huu naona anahamu ya kombe