Kuna vitu muungano umewasaidia sana hamvijui na hatuvisemi!, waliofanya yale Mapinduzi Matukufu ni wenyewe wenye Zanzibar yao, japo walivunja ghala la silaha na kuziiba bunduki, umagwaji mkubwa wa damu kwenye mapinduzi yale, haukufanywa kwa bunduki, bali kwa mapanga na majambia kwa kuchinjana!, najua unawajua waliochinjwa na walikufaje!, madhila makubwa na mabaya zaidi yaliyowakuta waliopinduliwa sio usiku ule wa mapinduzi bali the aftermath ya mapinduzi, najua unakijua walichokifanya waliopindua kwa waliopinduliwa!, mshukuruni sana Mwalimu Nyerere na Muungano, kuna wengine mnapiga kelele humu kulaani na kuubeza muungano. bila kujua kuwa bila muungano, kuna baadhi yenu msingezaliwa, maana hao watu wa kuwazaa wote wangemalizika, kama Juliasi asingemdhibiti Okello, amini nakuambia, hata Karume mwenyewe angefyekwa kwa sababu ameoa mke kutoka jamii inayopaswa kufyekwa!, na Okello angawafyeka wote kabisa wa jamii ile!, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo!, alikuwa anakwenda kufanya kufanya genocide.
P