Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Dr Mwinyi sio Mzanzibari,haijui Zanzibar,hajawahi kuishi Zanzibar,hajui matatizo ya Wazanzibari

Tunataka Mzanzibari mzalendo ambae anaweaza kuwaongoza Wazanzibari kwa maslahi ya Zanzibar

Naona Seif anafaa,wengine wote ni wachumia tumbo tu,vibaraka wa Tanganyika
Kabisa mkuu hawa mbuzi wa Tanganyika mwaka huu lazima tuwaonyeshe kuwa tumewachoka
 
Yaani waifanye hii nchi Kaka ya kwao atoke mwinyi aje mwinyi acheni huo upumbavu ss watanganyika wenye mlengo ule tutapigwa na butwaa
It's normal kwa watoto waliokulia Ikulu, kuja kuwa marais, hivyo ikitokea baada ya Mwinyi akaja Mwinyi, tulikuwa na Karume, akaja Karume, jirani tuna Kenyatta na Kenyatta, DRC Kabila na Kabila, . Kati ya nchi 54 za bara la Africa, nepotism kwenye urais nimetokea mara 38! Na sio Africa tuu,hata US kulikuwa Adams na Adam's, na Bush na Bush, India Gandhi na Gadhi, Pakistani Bhutto etc.

2015 Makongoro aligombea.
Hivyo hakuna cha ajabu.
P
 
Mkuu, katiba inasema Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri kwa nafasi yake chini ya uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Haitaji kuwa waziri au waziri asiyena wizara.

Wengine ni makamu wa rais, waziri mkuu na mawaziri wake isipokuwa manaibu waziri hawana sifa ya kuingia kwenye cabinet
Yes hivyo ndivyo ilivyosema katiba, watu pekee wanaoingia cabinet na sio mawaziri ni watatu tuu, Rais, Makamo na Katibu Mkuu Kiongozi, Rais wa Zanzibar haingi cabinet kama rais wa Zanzibar kwasababu ndani ya cabinet ya JMT, Zanzibar doesn't exist,hivyo lazima ateuliwe kama Waziri asiye na wizara maalum, aapishwe ndio aingie!.

Tusubiri safari hii kama yule jamaa yetu alishinda, atapewa uone kama atateuliwa na ataingia cabinet meeting!.
P
 
Kabisa mkuu hawa mbuzi wa Tanganyika mwaka huu lazima tuwaonyeshe kuwa tumewachoka
Mkuu Natafuta Kiki, wewe endelea tuu kutafuta Kiki, mwisho wenu mtakufa na vihoro na vijeba vya roho kuuhusu huu muungano wetu adhimu, uliosababishwa na yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hao mnaowaita mbuzi ndio walikufadhilini na kuwasetiri na bado wanakufadhilini na kuwasitiri!. Ama kweli, shukrani ya punda...fadhila mfadhili mbuzi, utauonja mchuzi, lakini binaadamu...
P
 
Yes hivyo ndivyo ilivyosema katiba, watu pekee wanaoingia cabinet na sio mawaziri ni watatu tuu, Rais, Makamo na Katibu Mkuu Kiongozi, Rais wa Zanzibar haingi cabinet kama rais wa Zanzibar kwasababu ndani ya cabinet ya JMT, Zanzibar doesn't exist,hivyo lazima ateuliwe kama Waziri asiye na wizara maalum, aapishwe ndio aingie!.

Tusubiri safari hii kama yule jamaa yetu alishinda, atapewa uone kama atateuliwa na ataingia cabinet meeting!.
P
Yule jamaa ana "laana" ya JKN; Kama alishindwa kupata nomination visiwani 1985 ili we sehemu ya cabinet; basi kama ambavyo EL na Mzee Malecela walikosa sifa za kupenya 5bora; ndiyo same principle inayomfanya huyo "kipenzi cha wapiga kura wa kisiwa chake" kukosa sifa. Bahati mbaya mtoa laana alishatangulia mbele za haki
 
Hapo kwa mama samia ndio kabisaa hataki kusikia tena hayo mambo kwanza mpaka hapo alipo saa hivi ni vike basii anatamani hata kesho mda wake ufike apumzike zake
 
Mtakufa na vihoro!, hao mnaowaita mbuzi ndio wanakufadhilini na kuwasitiri!. Ama kweli, fadhila mfadhili mbuzi, utauonja mchuzi.
P
Usipanik P,hayo ni mawazo yake,Tanganyika haifadhili Zanzibar isipokuwa inaitia Zanzibar katika majonzi na umasikini

Wanasiasa wa Zanzibar ni wachumia tumbo wako kimaslahi binafsi kuliko maslahi ya Wazanzibari..

Tanganyika itafanya kila njama na fitna za kuwagombanisha Wazanzibari wasitambuane, kwavile nayo inaing'ang'ania Zanzibar kimaslahi,

ref Lukuvi,Hotuba yake Ile aliyoitoa Kanisani kuhusu Zanzibar na Wazanzibari na kwanini Tanganyika inaing'ang'ania Zanzibar,hotuba iko YouTube,kaisikilize

Kila Kitu kina mwisho,let's wait and see, time alone time will tell
 
Pazia la kuichukua fomu za kugombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi huenda likafunguliwa Rasmi muda wowote kuanzia mwezi Juni 2020.

Sina hakika na ndoto yangu, Ila haya ndio niliyoyaona ndotoni.

Nawaona wanaume wawili wakichuana vikali sana, kiasi kwamba wanarandama kwa sifa na haiba inayorandana Kila pahala. Wasomi Hawa wawili wa kiwango cha juu wanazidiana sifa moja tu.
Mmoja ameishi na kukulia Zanzibar na mwingine ameishi na kukulia Dar es Salaam.

Wanaume hao Ni Profesa Makame Mbarawa Mnyaa na Dkt. Hussein Mwinyi.

Naona ukungu mzito watu wengi wanabishana hapana huyu hajakulia na kuishi huku iweje tumkabidhi jukumu zito hivi wakati ana kila nasaba na watu wa bara. Safari hii hatukubali lazima tufanye tutakavyo sisi na sio wao.

Naiona busara kubwa ikitumika kumaliza mgogoro huu kwa turufu ya jinsia. Unazuka mjadala kama ndio hivyo basi wakose wote na akae mwanamke ili kuondoa dhana ya upendeleo na visa vya nani ni nani.

Namuona mwanamke mwenye sauti ya mamlaka na akitokea kwenye kiti chenye maamuzi mazito akikubali kubeba gharama za kuinusuru chama na mpasuko. Namfananisha na Samia Suluhu Hassan. Nyota yake Ni Kali sana na ndiye anayewatuliza wanaume hawa wawili kwa kuvaa kiatu cha kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM huko visiwani Zanzibar.

Ndoto yangu haiishii hapa, namuona Mwenyekiti na kamati yake wanajifungia kwa muda na hawa wanaume wawili Kisha wanakubaliana kitu.

Siku chache baadaye nawaona wanaume hawa wanaongozana hadi Dodoma.

Namuona Mwenyekiti wa wa CCM anapitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa ndiye mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Nawaona wajumbe wa CCM wanaenda chemba kunong'onezana na kisha Mwenyekiti wa muda anamtangaza Dr. Hussein Mwinyi kubeba bendera ya Chama kama Mgombea mwenza wa Magufuli.

Ndoto inaendelea nawaona wajumbe wakimtaja Profesa kama Makamu Rais wa Zanzibar.

Nawaona wakitoka na nyuso za furaha Kila mmoja.

Usingizi unakatika nashtuka najiuliza ni kweli au ni mawaa ya ndoto.

Ngoja tusubiri media confirmation, mimi nishamaliza ndoto yangu.
naona ndoto yako haijakamilika na vipi mara hii pia mutaufuta uchaguzi au mutamtangaza tu na hamutatowa form za matokeo ebu lala tena utupe jibu
 
Kwa siasa na "mfumo wa kijamii" wa Zanzibar kamwe Mwanamke hawezi kuhimili vishindo katika nafasi ya urais, ni lazima Rais awe kidume.

Ndoto yako imekosa kuzingatia jambo muhimu la " mfumo wa kijamii wa wazanzibar" ambao hata hao wanawake wanauheshimu.
hakuna mfumo wa kijamii wala baba ake wakikubali wabara ndio yupi awe rais ndie anayetangazwa
 
Mkuu kuwa na shukrani ni jambo jema sana. Muungano ni sacrifices, sasa mtu ana ji sacrifice hadi kulifuta jina lake la Tanganyika, kwa ajili ya muungano, huku Zanzibar ikiachwa na jina lake, utaifa wake,umeme bure, ajira za JMT bwelele, wanasomea elimu ya juu JMT bila kuchangia senti tano, asilimia 4.5% ya fedha za misaada ni zao, fedha zote ni za JMT, Mabalozi, Jeshi, Polisi, Uhamiaji, Mawasiliano, Bahari kuu Anga, ulinzi na usalama, vyote ni bure!. Kumuita mkoloni ni shukrani ya punda!.

P
Bora umemwambia brother..... Kuna watu ni mazezeta wa akili Sanaa.... Wanadhani ss hatuipendi tanganyika yetu
 
Hivi kati ya Makamu wa Rais wa Tanzania na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nani ni mkubwa kimadaraka?
Naomba ushauri, kisiasa makamu wa raisi TZ na raisi wa Zanzibar nani zaidi?
Henri na Jose, ki ukuu, Makamu wa rais wa JMT ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar, ila ki mamlaka na madaraka, rais wa Zanzibar ni mkubwa zaidi kwasababu yule ni rais, ndani ya muungano, rais wa Zanzibar ana mamlaka na madaraka kama rais wa Tanzania bara, lakini makamo wa rais hana malaka yoyote wala madaraka bali ni ceremonial akisubiria just in case something happens to rais.
Dr. Shein alikuwa VC kwa miaka 10 ndio akaenda kuwa rais wa Zanzibar.
P
 
Ipo siku wazanzibar watafanya tena mapinduzi matukufu zaidi
Hili haliwezekani tena, kwasababu kwa sasa status ya Zanzibar kimataifa sio nchi!, ni sehemu ya JMT, huwezi kufanya mapinduzi sehemu tuu ya nchi. Zanzibar ni sehemu tuu ya JMT yenye utawala wake wa ndani, Zanzibar sio dola, hivyo haiwezi kupinduliwa!, hao wanajeshi na polisi na uhamiaji, wote ni ni JMT!, wale JKU, KMKM na vikosi vya SMZ, ni migambo tuu, hivyo usitegemee migambo wafanye mapinduzi na tuna JWTZ, polisi na UWT wetu wa JMT hapo Zanzibar!.
Kiukweli kuna watu wana akili fupi kama...

Mwaka 1964 mapinduzi yalifanywa na jeshi lipi ?
 
Henri na Jose, ki ukuu, Makamu wa rais wa JMT ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar, ila ki mamlaka na madaraka, rais wa Zanzibar ni mkubwa zaidi kwasababu yule ni rais, ndani ya muungano, rais wa Zanzibar ana mamlaka na madaraka kama rais wa Tanzania bara, lakini makamo wa rais hana malaka yoyote wala madaraka bali ni ceremonial akisubiria just in case something happens to rais.
Dr. Shein alikuwa VC kwa miaka 10 ndio akaenda kuwa rais wa Zanzibar.
P
Rais wa Tanzania bara ni nani ?
 
Usipanik P,hayo ni mawazo yake,Tanganyika haifadhili Zanzibar isipokuwa inaitia Zanzibar katika majonzi na umasikini

Wanasiasa wa Zanzibar ni wachumia tumbo wako kimaslahi binafsi kuliko maslahi ya Wazanzibari..

Tanganyika itafanya kila njama na fitna za kuwagombanisha Wazanzibari wasitambuane, kwavile nayo inaing'ang'ania Zanzibar kimaslahi,

ref Lukuvi,Hotuba yake Ile aliyoitoa Kanisani kuhusu Zanzibar na Wazanzibari na kwanini Tanganyika inaing'ang'ania Zanzibar,hotuba iko YouTube,kaisikilize

Kila Kitu kina mwisho,let's wait and see, time alone time will tell
Nahisi elimu ya Lukuvi ina shida kidogo maana hata wakati wa bunge la Katiba wakati wa Jk aliwahi kuongea vitu kuhsu zanzibar ambavyo hatukutarajiwa kiongozi kama yeye kuviongea.
 
Henri na Jose, ki ukuu, Makamu wa rais wa JMT ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar, ila ki mamlaka na madaraka, rais wa Zanzibar ni mkubwa zaidi kwasababu yule ni rais, ndani ya muungano, rais wa Zanzibar ana mamlaka na madaraka kama rais wa Tanzania bara, lakini makamo wa rais hana malaka yoyote wala madaraka bali ni ceremonial akisubiria just in case something happens to rais.
Dr. Shein alikuwa VC kwa miaka 10 ndio akaenda kuwa rais wa Zanzibar.
P
Mkuu Pascal kwa kumbukumbu Dr Shein hakufikisha miaka 10,alikuwa VC baada ya Dr Omar Ali Juma kufariki hyo mwaka 2001,akamaliza na Mkapa term yake iliyobaki,akaanza pia na JK mpka 2010 alivyoenda kugombea urais wa Zanzibar
 
Wezi wa fadhila wantufikicha kisha wanataka tuwashukuru.
We Acha tuu .
Kuna vitu muungano umewasaidia sana hamvijui na hatuvisemi!, waliofanya yale Mapinduzi Matukufu ni wenyewe wenye Zanzibar yao, japo walivunja ghala la silaha na kuziiba bunduki, umagwaji mkubwa wa damu kwenye mapinduzi yale, haukufanywa kwa bunduki, bali kwa mapanga na majambia kwa kuchinjana!, najua unawajua waliochinjwa na walikufaje!, madhila makubwa na mabaya zaidi yaliyowakuta waliopinduliwa sio usiku ule wa mapinduzi bali the aftermath ya mapinduzi, najua unakijua walichokifanya waliopindua kwa waliopinduliwa!, mshukuruni sana Mwalimu Nyerere na Muungano, kuna wengine mnapiga kelele humu kulaani na kuubeza muungano. bila kujua kuwa bila muungano, kuna baadhi yenu msingezaliwa, maana hao watu wa kuwazaa wote wangemalizika, kama Juliasi asingemdhibiti Okello, amini nakuambia, hata Karume mwenyewe angefyekwa kwa sababu ameoa mke kutoka jamii inayopaswa kufyekwa!, na Okello angawafyeka wote kabisa wa jamii ile!, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo!, alikuwa anakwenda kufanya kufanya genocide.

wachaa porojo hao wauwaji wote walipelekwa na kambarage nyerere
 
Back
Top Bottom