Mbona tunaambiwa kwa vitabu Yusuf alipata ndoto za mambo yatakayotokea mbele na ikatokea. Wengine wanapewa uwezo tu wa kuota mambo na yakatokea. Tuache ujuaji wa dini tulizoletewa na 'mabwana' zetu wa Mashariki ya mbali. Sijaona kosa lake.
Yusuf ('Alayhis Salaam) alikuwa ni Nabii Wa Allah. Hakuwa kuhani/ mtabiri/mpiga ramli/soothsayer.
Katika Uislam tumekatazwa kuwasikiliza na kuwasadikisha Soothsayers. Usighurike na baadhi ya wanayosema kutokea kweli. Sababu hupewa taarifa na mashetani wa kijini wanaoiba taarifa kutoka katika maongezi ya Malaika. Kisha wanauleta kwa rafiki zao wanaoshirikiana nao. Na huuchanganya na uongo mwingi.
Aisha reported: Some people asked the Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, about soothsayers. The Prophet said, “
They are upon nothing.” They said, “O Messenger of Allah, sometimes they speak about things that come true.” The Prophet said, “
Those are the words snatched by the jinn, who whisper it into the ears of their friends and it is mixed with more than one hundred lies.”
Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 6213, Ṣaḥīḥ Muslim 2228
Grade:
Muttafaqun Alayhi (authenticity agreed upon) according to Al-Bukhari and Muslim
Hivyo kuwafuata/kuwasikiliza wapiga ramli, watabiri na makuhani ni Haramu na kuwasadikisha ndio kabisaaa ni Kufru.
‘Imran ibn Husayn reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “
He is not one of us who reads omens or has them read for him, or who performs soothsaying or has it performed for him, or who practices magic or has it practiced for him.”
Source: Musnad al-Bazzār 3578
Grade:
Sahih li ghayrihi (authentic due to external evidence) according to Al-Albani
Hivyo jambo la Nabii Yusuf ('Alayhis Salaam) huwezi fananisha na Soothsaying.
Ndio nimekumbuka yule aliyedai eti Qur'an inasema Nabii Sulayman ('Alayhis Salaam) alikuwa anafuga majini. Nabii Sulayman hakuwa ana"fuga majini" bali Allah alimpa Ufalme ambao Majini pia walilazimishwa kutii amri yake na walidhalilishwa juu yake.
Wakati wanao"fuga majini" ni washirikina ambao huingia makubaliano (mkataba) na majini; wao hufanya shirki pamoja na dhambi nyengine kubwa kubwa kisha majini ndio huwatumikia baada ya hao washirikina kufanya shirki na dhambi nyengine kubwa kubwa ambazo nyengine ni kufru kubwa kabisa.
Hivyo wafuga majini ni wachawi na Nabii wa Allah Sulayman hakuwa mchawi wala hakukufuru;
102. Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
(Qur'an 2:102)
Kisai