Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 54
- 140
...Kuna siku mkongwe @edokumwembe alisema Yanga wako karibu zaidi kupoteza mchezo au kutoa sare kuliko kushinda watu hawakumuelewa...
Kuna Wachambuzi pale Wasafi Fm walitanabaisha ubora wa Yanga viongozi wakapiga simu studio na kuanza kukosoa...
Iko hivi...
Kabla ya Yanga kupoteza walikua wamecheza mechi 7 na kushinda zote...
Katika kushinda hizo zote,Mechi 5 kati ya 7 walishinda kwa bao 1-0.
Mechi mbili wakashinda kwa mabao 2+ (4-0 vs Pamba na 2-0 vs JKT Tanzania)
Tafsiri nyepesi ni kwamba ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi 5 kati ya 7 maana yake safu yako ya Ushambuliaji ina tegemea uimara wa safu ya ulinzi kushinda mechi.
Yaani timu ipo karibu zaidi kumaliza mchezo bila bao...ndio ukaribu wa sare au kufungwa..
Kama kwenye hizo mechi 5 wangeruhusu bao kwenye mechi mbili au 3 maana yake wangedondosha alama..
Leo safu ya Ushambuliaji haijafunga na safu ya ulinzi imefungwa ndio maana utofauti kwenye mchezo umeonekana.
Ukweli Yanga wana struggle kufunga mabao msimu huu tofauti na misimu iliyopita ingawa Kuna watu hawataki kuamini hicho kitu...
Project inaelekea mwishoni hii...
#NB: Lile goli hata uwaweke kina Diarra wawili wanakufa pale...
✍️Sospeter Ilagila