Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,258
- 20,386
Habarini za wikend wadau, bila shaka mu wazima na kwa wenye hitilafu kiafya Mwenyezi Mungu awapeni wepesi.
Ipo hivi:
Unamfatilia binti kwa mda mrefu weee halafu mwishowe anakubali mnapanga siku ya kukutana (appointment) unamsihi aje kwako ( yaani gheto) mtoto anakubali anakwambia atakuja wikiend.
Unafurahi unaanza kuliangalia gheto kama lina hadhi ya kuhost mrembo kama huyo, unaona kuna mapungufu kadhaa ghetoni kwani kwenye mazungumzo yenu ya nyuma alishawahi kusema anapendelea vitu fulani ambavyo wewe huna kwa muda huo. Unaamua kwenda mjini kati kwenye maduka ya hadhi angalau na wewe uonekane huwa unaenda supermarket au maduka yenye hadhi, unarudi mapema gheto huku umejaza mazaga ikiwemo matunda ya Apples ambayo ulinunua kwa buku mbilimbili na juice za hadhi kidogo ukiacha za miwa.
Kumbuka manzi hana nauli ya kuja (kama sh.7000 hivi) unaenda kibanda cha m-pesa unaweka 22000 unamtumia ishirini elfu nyingine atatumia mdogomdogo, baada ya mda kidogo unaona meseji ikisema "...Aksante huby nimeipata.." unafurahi moyoni.
Jioni mnaongea vizuri binti anasema alienda saluni. Unasema moyoni tayari ukijua bila shaka hayo ni maandalizi ya ujio wake. Mnaelewana kuwa atafika kwako mida ya saa nne asubuhi ( kesho yake). Asubuhi unaamka mapema kupangilia vitu vyako ikiwemo kutandika vizuri kitanda kwa mashuka ambayo ni nadra kuyatandika, unapulizia air fresher spray, hadi gheto linakaa poa.
Kwakuwa alisema anapendelea kupika unaenda butcher kuchukua kilo 1 ya maini ( lakini sio kawaida yako). Hapo saa tatu na arobaini na kitu unakimbia bafuni fasta kupata maji kwa mwili, unajiweka safi, papara hazikuishi mara usome kitabu cha mapenzi cha bwana Erick Shigongo. Saa nne na dakika takribani saba hivi unatuma meseji ".. umefika wapi bebi.." lakini kimya.
Baada ya robo saa unaona incoming call ya mrembo mwenyewe, unatabasam kabla ya kupokea unamwambia mshikaji wako aliyeingia ghetoni kwako aondoke kwani kuna ugeni maalum, then unapokea simu. Bila kusikiliza unauliza nikufate stendi? Anasema nisikilize mpenzi, samahani sitoweza kufika kwani tumefiwa na shangazi huko Moshi tuko njiani sasa hivi, nakupenda tufanye siku nyingine, halafu anakata simu. Unamnyokea hewani anakata anakwambia tuma meseji. Tehetehetehe😀😀😀😀
Je, ilishakutokea? Au kama bado vipi ungefanya nini na hizo mbwembwe za kwenda supermarket kununua mazaga?