UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Mod One Mod Two Moderator futeni huu uzi maana hauna ukweli wowote. Ni kipande tu mtu kakaa na kukitengeneza maana hakuna pahala huu utafiti ulipofafanua njia waliyotumia kufanya utafiti, hakuna validity wala reliability ya variable/data zao. Huu ni upotoshaji mkubwa sana, futeni haraka sana!

Unaona sasa, hawa ndio washatumwa kwenda kupinga tafiti,
na hii NGO ifungwe na kufutwa
 
Hebu soma vizuri kwa makini, usikimbilie tu kusema Bawacha.
Wewe ndio usome vizuri....Magufuli ana kubalika kwa 55% kwa hiyo hata ingelikuwa ni uchaguzi lazima angelishinda kabisa.....halafu CCM haihitaji utafiti ili kushinda Uchaguzi ...ccm kushinda uchaguzi ni lazima
 
Halafu unakuta hao waliohojiwa wote ni Wanachama wa vyama vya upinzani pamoja na viongozi wao, kwahiyo ukijumlisha sasa na wale ambao wanamuunga mkono ila hawakuhojiwa unakuta percentage ipo around 96%.
 
pamoja na mapunguvu kuwa sample iliyochukuliwa bado ndogo lakini nakubaliana na majibu kuwa bora iwe chini ili serikali ipate muda zaidi wa kukabiliana na changamoto kuliko kubweteka na sifa zisizotuvusha tulipo.
 
Mod One Mod Two Moderator futeni huu uzi maana hauna ukweli wowote. Ni kipande tu mtu kakaa na kukitengeneza maana hakuna pahala huu utafiti ulipofafanua njia waliyotumia kufanya utafiti, hakuna validity wala reliability ya variable/data zao. Huu ni upotoshaji mkubwa sana, futeni haraka sana!
Ule uchunguzi wa kamati za makinikia uliwahi kuonyesha jinsi ulivyofanyika?

Mbona mlikuwa mnasifia tu bila kuhoji?

Iweje leo uhoji huu utafiti kama ile ripoti mliisifia pasipo kuona ripoti nzima?

Ovyooo!!
 
FB_IMG_1530781249277.jpg
Utafiti wa Shirika la TWAWEZA uliotolewa leo unaonyesha kuwa kukubalika kwa Rais Magufuli kumeporomoka kutoka 96% mwaka 2016 mpaka 55% mwaka 2018. Mporomoko Huu ni wa kasi zaidi kupata kutokea nchini kwani Rais John Magufuli hakubaliki zaidi kuliko marais wengine wote waliopita.
Rais ambaye hakubaliki namna Hii kiasi cha watu masikini wa vijijini kuwa tayari kuandamana dhidi yake, ni Rais wa nani? Anamwakilisha nani? Ni Rais wa wanyonge kweli?

Ndio maana Rais wetu kila siku anazindua vitu ambavyo kiitifaki ni kazi ya MaDC. Anagawa fedha barabarani. Anagawa mapapai barabarani. Anaonyesha hasira, dharau na hata ukatili kwa Viongozi wenzake bila sababu. Anatoa kauli za kudhalilisha wanawake na kuligawa Taifa. Anagombana na Viongozi wa dini na kupandikiza chuki kwenye jamii.
Rais wetu anajua kuwa hakubaliki. Ndio maana anajaza watu wake kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, anateua ndugu na jamaa zake kwenye Mahakama zetu na kwenye hazina yetu.

Rais asiyekubalika namna hii anapaswa kuondolewa madarakani kwa mujibu wa Katiba yetu. Kuendelea kuwa naye ni Hatari kwa usalama wa Taifa letu.
 
Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 wa Aprili 2018 umebaini 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani 2015.

Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016 na 71% mwaka 2017

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Wazee (71%) kwa kiwango kikubwa wanaukubali utendaji wa Rais, huku wenye umri wa miaka 18-29 (46%) wakiukubali kiasi.

Wanawake (57%) wanaukubali utendaji wa Rasi kuliko wanaume (53%) na wasio na elimu (58%) wanaukubali zaidi kuliko wenye elimu ya juu (47%)

Kukubalika Vijijini

Mwaka 2017, wananchi wa vijijini (72%) waliukubali zaidi utendaji wa Rais kuliko wale wanmijini (70%)

Takwimu hizi zinaonesha kukubalika kwa utendaji wake kumeshuka zaidi vijijini kutoka 72% hadi 52% ukilinganisha na mijini 70% hadi 59%

Je, hii inaashiria nini kwa uongozi wa Rais Magufuli?

Nina wasi wasi kama Taasisi hii itaendelea kutoa takwimu hizi bila kuingiliwa. Hata mimi naona mvuto unaelekea kwisha kabisa. Ni halali yake kwani anavuna alichopanda!
 
Hizi Takwimu Ni Kwa Mujibu Wa Nbs? Hii Taasisi Imepata Kibali Wapi Kutoa Takwimu Hizi? Kwa Faida Ya Nani?
 
Ule uchunguzi wa kamati za makinikia uliwahi kuonyesha jinsi ulivyofanyika?

Mbona mlikuwa mnasifia tu bila kuhoji?

Iweje leo uhoji huu utafiti kama ile ripoti mliisifia pasipo kuona ripoti nzima?

Ovyooo!!
Salary Slip unajua ninavyokuheshimu kama GT. Ule utafiti kama ulipata nakala yake au ulimsikiliza yule presenter, walionesha jinsi walivyochukua sample, walieza jinsi walivyo fikia conclusion, na waliefafanua zaidi reliability na validity ya matokeo ya utafiti wao. Labda kama wewe umeamua kuvaa miwani ya mbao na kuachana na fikra za GT.

Huu uzi nasisitiza ufutwe haraka Mod Two
 
Hizi Takwimu Ni Kwa Mujibu Wa Nbs? Hii Taasisi Imepata Kibali Wapi Kutoa Takwimu Hizi? Kwa Faida Ya Nani?
 
Mod One Mod Two Moderator futeni huu uzi maana hauna ukweli wowote. Ni kipande tu mtu kakaa na kukitengeneza maana hakuna pahala huu utafiti ulipofafanua njia waliyotumia kufanya utafiti, hakuna validity wala reliability ya variable/data zao. Huu ni upotoshaji mkubwa sana, futeni haraka sana!
Sasa Mods waufute Uzi kwa kisa gani??

Mmezoea kulishwa data za kupikwa nyiye, watu wa Lumumba

Wacha sindano iwaingie
 
Back
Top Bottom