Utafiti binafsi: Mara nyingi ukimpa mdada hela/zawadi bila yeye kukuomba, huko mbeleni ndo atazidi kukupiga vizinga

Utafiti binafsi: Mara nyingi ukimpa mdada hela/zawadi bila yeye kukuomba, huko mbeleni ndo atazidi kukupiga vizinga

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
3,490
Reaction score
10,749
Habarini,

Kuna huu ushauri unaotolewa na wadada humu jf na baadhi ya wanaume, kwamba ukitaka mdada asikupige vizinga mara kwa mara, usiruhusu mpaka yeye akuombe, mwanaume inatakiwa ujiongeze, utoe bila kuombwa, juzi kati nikajaribu kuiweka hii myth to the test

Sample za research yangu zilitoka kwa wadada tofauti walio na rika tofauti watoto wa elf 2, na wadada ambao wanakaribia 30 ila hawajaolewa.

Results nilizotarajia baada ya kuwapa ofa ya pesa/zawadi hao wadada, ni kuwa maybe uhusiano wangu na wao ungeimarika kwa namna chanya (wao kuniona mwanaume wa kufanya nae maisha serious) ila results nlizopata toka kwa hao wadada wote ni tofauti na matarajio yangu, na results zote zimefanana.

Nimegundua kuwa mara nyingi ukimpa mdada pesa/zawadi bila yeye kukuomba, na mwanaume sometimes unafanya hivyo kama ishara ya kumuonesha upendo, sio kwamba unajaribu ku-show off kuwa una hela, au una-fake maisha, au hujui unachofanya, mdada ndo ataangalia namna nyingi zaidi za kukufanya umpe hela, vizinga ambavyo ni unreasonable toka kwake ndo vitaongezeka, hata kama hapo mwanzo alikua hakuombi hela.

Kwenye soko la dating, sometimes mtu unakua na nia nzuri, ila nia nzuri, inakuletea results ambazo sizo.
 
Inashangaza.

Utawasikia wakilalamika kutafsiriwa vibaya; wanapowaonesha wanaume ustaarabu kidogo tu, wanaume hukimbilia kuwatongoza,

Wakati na wao wakioneshwa ustaarabu kidogo tu wa kusaidiwa vocha wanajiingiza moja kwa moja...

Inabidi vijana masikini wote tuamue kujitoa kwenye mapenzi.
 
Tatizo sio umasikini wenu tatizo mnatafuta usawa na wanawake!!
 
Inashangaza.

Utawasikia wakilalamika kutafsiriwa vibaya; wanapowaonesha wanaume ustaarabu kidogo tu, wanaume hukimbilia kuwatongoza,

Wakati na wao wakioneshwa ustaarabu kidogo tu wa kusaidiwa vocha wanajiingiza moja kwa moja...

Inabidi vijana masikini wote tuamue kujitoa kwenye mapenzi.
Saidia fundi upo? 😹😹
 
Inabidi vijana masikini wote tuamue kujitoa kwenye mapenzi.
Kuna vijana nawafahamu ambao kwa maisha ya levo za kibongo bongo kwenye swala la pesa wamejipata gari na nyumba wanazo, income nzuri wanayo, ila bado wako single, moja ya sababu nahisi ni hii tabia ya wadada wengi sahivi kuweka hela mbele..

Mwanaume hata kama unapata tsh million 8 kwa mwezi, ukisema utafte mke kwa kuangalia tabia za uwaifu matirio, sijui mwenye upendo wa kweli, kuna uwezekano wa asilimia 80 hutaoa, maana karibia wote wako kimaslahi..😁 mshamba_hachekwi
 
Back
Top Bottom