haki ya mungu nyie wagalatia sijui mna nini!
yaani we unaona mimi sina maana kuosha uso wangu na maji kabla ya kuabudu??
hebu tuliulize andiko! je kuna walionawa na kuosha nyuso na miguu yao!
au walikunywa damu tu ya yesu!!
Kutoka 40: 30-32, Mose aliweka birika la kutawadhia katikati ya hema na kutia maji ya kutawadha. Mose, Aroni na wanawe wote walinawa mikono na miguu ya humo walipoingia ndani ya hema.
halafu ngoja nikuongeze kidogo!
wewe ukiingi kanisani kunywa hiyo damu huwa unaswali vipi?? unakaa kwenye mabenchi sio!! halafu unaomba sio?? hebu tazama andiko linakufundisha vipi yesu aliswali!!
Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali
Basi akaenda mbele kidogo akaanguka kifudifudi, akasali (Mathayo 26: 36 39). Naye Abramu akasujudu (Mwanzo 17: 3). Yoshua akainama chini akasujudu (Yoshua 5: 14). Naye Elia akapanda juu ya mlima Karmeli, na huko akainama hadi chini na kuuweka uso wake katikati ya magoti yake (1 Wafalme 18: 42).
haya mgalatia, na wewe unatakiwa uanguke kifudifudi kama waislamu na kama yesu!