Songoro
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 4,122
- 1,021
ok! MIMI MWEHU! WE MWENYE AKILI UNASEMA YESU ALIKUWA ANAJIITA MWENYEWE KUWA NENO! SIO?? YAANI YESU NI MUNGU AU SIO?? NA AKISEMA AMETUMWA BILA HIARI YAKE :ANA MAANA KAJITUMA MWENYEWE SIO?
HEBU NIFAFANULIE NA HAPA SASA!!
YOHANA 7:28
Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, "Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui!!
HUYU YESU ANAESEMA " NANYI HAMUMJUI NI NANI??
NA HAPA YESU ANDIKO LINASEMA:Mathayo 27.45-50
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
SASA WEWE MWENYE AKILI NYINGI, NA USIE MWEHU NAKUULIZA! HAPA YESU ALIKUWA ANAJIITA MWENYEWE SIO???
NA KWA KUMALIZIA TU! NYIE WENYE AKILI NYINGI SI HUWA MNAVAA ILE MISALABA SIO!
Ama utumiaji wa msalaba katika kuvaa umezagaa kabisa kwa Wakristo wa zamani na wa sasa. Kufanya hivyo kwao ni kukumbuka kule kusulubiwa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za wanadamu nao waingie katika kusamehewa dhambi zao hapa duniani na kurithi uzima wa milele Siku ya Qiyaama. Hata hivyo, tukisoma katika Biblia tunapata kuwa Yesu hakusulubiwa kwani aliyesulubiwa atakuwa amelaaniwa. Hebu tutazame mistari ifuatayo:
- "Kama mtu amefanya kosa la jinai linalompasa auawe na akauawa kwa kutundikwa mtini" (Kumbukumbu la Sheria 21: 23).
- "Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; maana Maandiko yanasema: 'Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa" (Wagalatia 3: 13).
Hakika ni kuwa wenye kuamini kuwa Yesu kasulubiwa na misalaba kwa ajili ya kusamehewa dhambi wanapingana na Biblia. Hebu tusome mistari ifuatayo:
- "Maana ninachotaka kwenu ni upendo na si dhabihu, kumjua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa" (Hosea 6: 6).
- "Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: 'Nataka huruma, wala si dhabihu'. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi" (Mathayo 9: 13).
- "Kama tu mngejua maana ya maneno haya: 'Nataka huruma wala si dhabihu', hamngewahukumu watu wasio na hatia" (Mathayo 12: 7).
Kwa hivyo Yesu hakuja kuwa dhabihu, yaani kuuliwa msalabani bali amekuja kuwaokoa wenye hatia waingie katika mafundisho ya haki na hivyo kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu
SASA NAKUSISITIZA TU! KUWA MSTAARABU NA ACHA KASHFA!! We weka andiko tu! bila kulichakachua na HAKUNA ALIYEKURUHUSU KULETA LOGIC YAKO KUBADILI MAANA!! ANDIKO LIKO WAZI!!
Vitu kama hivi ndio vinawasukuma kufuta Mihadhara, Zamani kuwaonesha Maandiko haya iliitwa Kashfa, Baada ya hukumu ya Dibagula Court of Appeal, siku hizi ukiwaonesha haya Mnaandiko inaitwa Uchochezi na Uvunjifu wa Amani, Kazi yao wakikutana ni Kelele za Kwaya eti hakuna Mwanaume kama yesu halafu hapo hapo wanasema Yesu Mungu wakat washasema ni Kidume kisicho mfanowe!