mkuuu mimi nataka kujua structure halisi ya kibilogia ya hichi kirusi kimeumbwa je umbwaje..!? ....napia kinawezaje kupenye membrane zilizope kwe mwili na kuingia kwenye celll na kusababisha ugonjwa... !!!?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ndugu
victor moshi nadhani watu wa Molecular Biology na Madaktari wanaweza kujibu swali lako vizuri zaidi kuliko mimi. Ila nataka kuamini kwamba iwapo umesoma Biology, basi utakua unaelewa Viruses ni viumbe wa aina gani na structure/anatomy yao ikoje. Viruses wako wa aina nyingi sana na wana complex structures based on either RNA or DNA sequences (the genetic materials). Ila itoshe tu kusema Covid19 ana sifa za msingi za virusi wengine unaowafahamu.
Tofauti ya Covid2 na wengine ni upya wake kwenye familia au ukoo wa virusi wa Coronavirus. Hadi alipolipuka hakua amefahamika. Ila ukoo wa Coronaviruses unafahamika siku nyingi na wengi wao wanashambulia mfumo wa upumuaji (upper respiratory track). Covid19 ana binamu zake wa karibu wanasababisha mafua ya kawaida; ana pacha (twin sister) anayeitwa SARS-Coronavirus ambaye naye alilipuka China mwaka 2002/2004 lakini hakufanikiwa kusambaa kwa kiwango hiki. SARS-Covid1 alidhibitiwa kwa haraka na hajaibuka tena. Pia, ana dada yake mwingine anaitwa Middle East Respiratory Syndrome (MERS) Coronavirus aliyelipuka 2012 lakini hakusambaa njie ya Mashariki ya kati.
Sifa kubwa ya viruses ni viumbe ambao hawana uhai wao wenyewe hivyo wanakua inactive na kutozaliana bila kuwa ndani ya kiumbe mwingine (inaweza kuwa ndani ya bacteria, mmea au mnyama). Wanapoingia kwenye mwili au cell ya kiumbe mwingine, kazi ya kwanza na ya haraka wanayofanya ni kuzielekeza cells za kiumbe hicho kuzalisha virusi wengine (duplicating themselves). Ugonjwa wanaosababisha ni matokeo ya uwepo wao kwa wingi ndani ya mwili kama wavamizi; nini hasa wanashambulia ndani ya mwili; na ni cells au kungo gani la mwili.
Covid19 akiingia kwenye mwili anakimbilia kwenye nyuma ya matundu ya pua yako (nasal passage) na kwenye utando wa koo (mucus membrane at the back of your throat). Tazama picha yake hapa chini utaona vitu vinaitwa "spikes" (vyekundu) ambavyo ndivyo anavipenyeza kwenye membranes za cells na kuanza kumimina genetic material zake (tuite mbegu zake). Genetic material zake zinaanza kuingilia utendaji kazi wa kawaida wa cells za mwili na kuziamrisha zianze kufanya kazi ya kuzalisha virusi wengine.
Wanapoanza kuzalishwa wanaendelea kutoka kwa wingi na kuvamia cells zingine kwa haraka na ndio mana dalili za kwanza mtu anapoambukizwa ni mafua, kikohozi kikavu na koo kukereketa (sore throght). Kwa haraka sana wanaendelea kuzaliana na kushuka kwenye koo chini kueleka kwenye mapafu na kuingia kwenye cells za mapafu zinazohusika na kazi ya kuchuja hewa (kutoa hewa ukaa-CO2 na kuingiza Oksijeni O2). Hapa mapambano kati ya Covid19 na cells huwa makali zikijilinda ili kuendelea na majukumu yake. Cells za mapafu nyingi zinaanza kuvimba, kutoa usaha na hata kufa kwenye vita hiyo. Ndio mana dalili nyingine inayofuata kwa haraka ni kubanwa kifua na kushindwa kupumua maana oksijeni inashindwa kupita kama kawaida.
Sasa mtu mwenye afya njema, mwili wake unaweza kupambana na Covid19 na kuwashinda na ndio mana anakua na dalili zisizo kali na anapona ndani ya siku kuanzia 5 hadi 14. Kwa mtu ambaye tayari mwili wake uko busy kupambana na magonjwa mengine kama ya TB (kifua kikuu), diabetic (kisukari), cancer (kiharusi), magonjwa ya moyo, figo, nk; Covid19 wakiingia wanapelekea hali yake kuwa mbaya zaidi (cells zake zinalemewa na kushindwa kutimiza majukumu yake). Zikishindwa kabisa ndio kifo kinakuja. Ndio mana utaelewa ni kwa nini zaidi ya 95% ya vifo vyote vya Covid2 duniani ni wazee na watu wengine ambao tayari wana chronic diseases kama niliyotaja hapo juu. Asilimia ndogo sana ya watoto na vijana wenye afya njema ndio wameathika.
Na hii ndio sababu nilikosoa uharaka wa serikali ya Kenya, yetu na zingine za Afrika kufunga shule na vyuo haraka kama hatua ya kwanza ya kudhibiti ugonjwa (nimejadili kwingine). Kundi hili sio hatarishi kwa Covid19. Evidence from emprical data worldwide inaonesha hatari ya ugonjwa huu unategemea umri (age dependent). Kwa mfano, kwa wagonjwa chini ya miaka 20 ni mtu 1 kati ya 10,000 (0.01%) anakua na hali mbaya na kuhitaji intensive care wakati kwa watu wazima ni mtu 1 kati ya 12 (8.3%). Walifariki Italy, karibu 99% ni watu wazee na waliokua na magonjwa mengine. Kati wagonjwa zaidi ya 160 UK, mgonjwa mdogo kabisa kufariki ana miaka 45 na alikua na ugonjwa hatiri wa motor neurone disease hivyo Covid19 ikamalizia.
Sina hakika kama nimejibu vema swali lako. Kama nilivyosema, watu wa Microbilogy na Madktari wanaweza kukusaidia zaidi maana nami bado nina ujinga mwingi kwenye eneo hili. Mimi nimejikita zaidi kwenye mifumo ya namna ya kufuatilia na kuzuia magonjwa
(disease surveillance and response systems) hivyo ndio eneo ambalo naweza kuliongelea kwa mamlaka zaidi.
MM Togolani