Utafiti mpya wa kisayansi wa Covid19 – Msaada mkubwa wa kujikinga na kuzuia maambukizi kwa wengine

Utafiti mpya wa kisayansi wa Covid19 – Msaada mkubwa wa kujikinga na kuzuia maambukizi kwa wengine

Kumbe siyo kweli kwamba wanasayansi si wanasiasa!
Ingawa robo robo watukanane Hawa wataalamu wetu (MM Togolo na X bar) ila malumbano yao yamesaidia kutuongezea mwanga
Nilichofurahi mwishoni Kila mtu kamsamehe na kumuomba radhi mwenzie.

Hitimisho kwa nilivyowaelewa. Wasiopendekeza kuvaa mask wameangalia matokeo baada ya kuvaa.
1. Taharuki
2. Uwezo wa kugharamia maana atleast uvue Kila baada ya masaa 3
3. Namna sahihi ya uvaaji haijulikani
4. Kuenea kwa magonjwa kupitia njia ya hewa kwa kutozingatia kanunni za uvaaji

Wanaopendekeza kuvaa mask
1. Biashara nzuri
2. Hakuna kutengana wote tuwe na haki ya kujilinda.
3. Itapu guza unyanyapaaa wote tutakuwa tumevaa
4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo mazuri sana ila rudia namba 2 utaona kuna point inamislead...

Siku 2-14 ni window period ya virus na ndani ya muda ndipo signs za uwepo wake ndani ya mwili wako zitakapoanza kuonekana. Siyo kipindi cha virus kufa..

Kalantini watu hukaa ili kama ameambukizwa ndani ya muda huo dalili zitaonekana ama hata vipimo vitaweza kuonyesha maambukizi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
X-bar, Nimekusamehe ndugu X-bar kwa uliponikwaza. We all make mistakes. Mungu akubariki kwa ustaarabu wako.

Pamoja na kwamba majibizano hayajawa mazuri sana lakini yanaweza yakawa yamesaidia kuipanua mada.

As my yake, yako niliyojifunza na next time nitajitahidi kufafanua points zangu vizuri zaidi na penye utata niuweke wazi.

MM Togolani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante ndugu MAGO.

Nirekebishe kama nitakosea ila nadhani kuna concepts 2 ndani ya huu muda tunauongelea: kuonesha dalili (symptomatic) na kuwa na uwezo wa kuambukiza.

Moja: kama ulivyosema mtu anakua symptomatic ndani ya siku 2-14. Hivyo kama mtu amekua na contact na mwenye maambukizi anashauriwa kujitenga ndani ya muda huu hata kama hana dalili maana inawezekana dalili hazijawa wazi. Kama kaambukizwa inategemewa ndani ya muda huu atakua kaonesha either mild or severe symptoms and that will determine the nature of care needed.

Dhana ya pili, mtu mwenye maambukizi anategemewa kuwa kwenye hatari ya kuambukiza wengine (kwa sehemu kubwa) muda ambapo dalili zimejitokeza. Muda huu ndio kuna uwezekano mkubwa atakua anapiga chafya na kukohoa, hivyo na kujishika usoni kunakua kwingi pia.

Kwenye point namba 2 uliyorejea niliandika based on this fact na sikua namaanisha ni muda wa half-life decay. Nisaidie kuweka sawa kama kuna gap.

Moja ya study iliyofanyika China inatoa hitimisho hili:

"These findings confirm the current recommendations for quarantine: Most patients who become symptomatic do so within 11 or 12 days and the vast majority within 14 days. However, we already know that asymptomatic or mildly symptomatic persons can transmit infection, and this group was not included here. Better access to testing for asymptomatic infection will shed light on this issue".

MM Togolani.

MAGO,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa. Kutukanana ni mbali sana ndugu. Huwezi nifikisha huko hata kwa kiboko maana moja ya kanuni za kutofautiana hoja na ni kinyume na maadili yangu.

Kuhusu wanasayansi na siasa, ushahidi ulioko unaonesha sisi ndio tunaweza kuwa wanasiasa wazuri zaidi[emoji41]. Siasa ni sehemu ya maisha na kwenye sayansi inatumika kwa kiasi kikubwa kuliko unavyodhani.

Kwa mfano, unaweza ukaandika utafiti wako mzuri sana wa kisayansi lakini kama matokeo yake yatachafua ugali wa watu fulani wenye nguvu, unaweza kataliwa kuchapishwa au ukalazimishwa ubadili baadhi ya findings.

Leo ukiibuka na utafiti kuonesha madhara makubwa ya simu za mikononi kwa afya, usishangae kila publisher akagoma kuuchapisha au akanyamazishwa na makampuni makubwa yanayotengeneza simu. It is the same in pharmacetical industry.

Hizo ni siasa ndani ya kazi za kisayansina lazima uweze kukabiliana nazo.

MM Togolani masandare,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MM Togolani,
Aisee mkuu Una uwezo mkubwa Sana wa kujitawala na kujipa utulivu hata katika mazingira yanayoudhi na kuleta kejeli...nimependa saaana majibu yako kila wakati Kwa kila hoja mlipokuwa katika majibizano-hayakeli,hayaudhi,hayana ujuaji wala kujionesha mjuaji bali yanashawishi kuendelea kusoma.

Binafsi nirudie kukupongeza kwa elimu nzuri na mahususi iliyotakiwa kwa wakati huu wa taharuki. Niseme tu elimu hii imetufaa sana Japo kila mtu atakuja kukushukuru hapa.

Ni kweli sijaona mahali ulipokataa kukosolewa ama kusahihishwa Kwa lolote katika bandiko lako,shida ni pale mtu mwingine anapochukua nafasi hiyo kujitahidi kujenga hoja katika baadhi ya mistari iliyo katika uzi kusema Yale anayodhani ulitakiwa pia kuyaandika Japo katika muktadha wa kuleta uzi hayakuwa na nafasi...

Kiufupi elimu tumeipata na kila mmoja aliyesoma btn lines amefaidika.

Asante sana na pongezi nyingi kwako mkuu.
 
X-bar,
Ninashawishika kukubali kwamba ulikuwa na Nia nzuri ya kupanua mada kurekebisha pale ulipoona panahitaji maboresho,ila duh sidhani kama angekuwa mtu mwingine mngemaliza simple hivi na kusema Tu ikaisha.

Binafsi nakupongeza Kwa uwezo wako mkubwa wa kujenga hoja na kuisimamia hata kama itaonekana kuhafifishwa Kwa namna fulani.

Lakini ni bora kujitahidi kila mara kutumia lugha stahiki isiyokwaza,na ya kiuungwana inayomwacha msomaji na mtu mnaejibizana naye na amani na utulivu,ukifanya hivi utaepusha kumkosesha amani mwanajamvi mnaejadili ama kujibizana kuhusu Jambo fulani.
Lakini pia hongera kwa kuwa muungwana mwishoni kuliko mwanzo na kufikia kumwomba msamaha mkuu Togani na nyote mkamaliza Kwa amani.

Pamoja mkuu.
 
Wazungu na wachina ni wajinga sn ndio maana kuna msemo unasema AKILI NYINGI HUONDOA MAARIFA nilitaka kushangaa ugongwa utoke china adi africa huku wakisema hausambai kwa njia hewa kisa kirusi cha korono ni kikubwa kwa mocro meter kadhaa sasa basi

kwa mujibu wa ripoti hii iweke sheria kila mtu avae barakoa na gloves kilazima ili km ana vidudu ivyo akikohoa vibaki kwenye barakoa zaidi ya ayo tujiandae kwa majanga makubwa kwa sababu ni vigumu kuona ayo matone yanayoelea na ni vigumu mtu kujizuia asikohoe.asipige chafya au aongee bila kutoa mate au asijishike uso pua na mdomo ni vigumu mno mbaya zaidi uku dar tushazoea supu za mama ntilie kwann tusige chafya vyumba tunavyoishi ni vichafu. vyoo vichafu.

mabasi machafu dah

AFRICA tuna tabu
 
RENATUS GODIAN,
Mkuu "barakoa" ndo mask bila shaka. Asante kwa kiswahili, tupatie na kiswahili cha gloves tafadhali🙏🙏
 
Late to the party, but these are my 0.02 Shillings:

1. Kuhusu kushauriwa wananchi wa kawaida tusivae barakoa (mask) iwapo hatukuathirika, nadhani hiyo inatokana na uhaba na gharama za barakoa. Nusu ya barakoa kwenye soko la dunia hutoka China. Sasa hapo China wenyewe hawazileti sokoni, wanazitumia wenyewe.

Kana kwamba hiyo haitoshi, China ilinunua barakoa toka nchi nyingine wakati China ilipokuwa nchi pekee yenye ugonjwa. Unaanzaje kuwashauri wananchi kutumia bidhaa ambayo haipatikani? Simba akikosa nyama hula majani. Heri nusu shari kuliko shari kamili.

2. Kila nchi inajaribu kupambana kivyake kusaidia wananchi wa nchi husika. Ni vema pakawa na mbinu ziendazo na mazingira ya kwetu. Tukitumia mbinu za wenzetu, tutapata matokeo wanayopata wenzetu. Mazuri kwa mabaya. Tukiasili mbinu zao kuzifanya ziende na mazingira yetu, tutapata matokeo mazuri zaidi, IMHO.
 
Asante sana kwa Elimu na muda wako, Mimi Bado najiuliza ‘zamani tumeambiwa kua virus HUA havionekani hata kwa darubini ya kawaida , Vipi huyu korona anaonekana kirahisi? ‘ je ni virus gani huyu?
 
Mkuu "barakoa" ndo mask bila shaka. Asante kwa kiswahili, tupatie na kiswahili cha gloves tafadhali🙏🙏
Mask sio parakoa lugha yetu mbuz mask inaziba uso mzima parakoa zinaziba pua na mdomo nadhan ipo haja kiswahili kifutwe furish language
 
Asante sana kwa Elimu na muda wako, Mimi Bado najiuliza ‘zamani tumeambiwa kua virus HUA havionekani hata kwa darubini ya kawaida , Vipi huyu korona anaonekana kirahisi? ‘ je ni virus gani huyu?
Ndugu gkileo hiyo zamani muliambiwa na nani? Pili, teknolojia inakua kila siku, hivyo sio ajabu sana kama sasa linawezekana lililokua haliwezekani huko zamani.
 
Vipi kuhusu virusi vya corona vikidondokea keyboard za ATM zetu kwa siku si itakuwa majanga tuombe sana Mungu atuepushe na janga hili.
Kwenye zile geti za maduka makubwa watu hubonyeza kutoa kadi za parking na pia Airport getini Mgeni akitoka nje akagusa pale wote wanaopita pale wanaambukizwa
 
Late to the party, but these are my 0.02 Shillings:

1. Kuhusu kushauriwa wananchi wa kawaida tusivae barakoa (mask) iwapo hatukuathirika, nadhani hiyo inatokana na uhaba na gharama za barakoa. Nusu ya barakoa kwenye soko la dunia hutoka China. Sasa hapo China wenyewe hawazileti sokoni, wanazitumia wenyewe.

Kana kwamba hiyo haitoshi, China ilinunua barakoa toka nchi nyingine wakati China ilipokuwa nchi pekee yenye ugonjwa. Unaanzaje kuwashauri wananchi kutumia bidhaa ambayo haipatikani? Simba akikosa nyama hula majani. Heri nusu shari kuliko shari kamili.

2. Kila nchi inajaribu kupambana kivyake kusaidia wananchi wa nchi husika. Ni vema pakawa na mbinu ziendazo na mazingira ya kwetu. Tukitumia mbinu za wenzetu, tutapata matokeo wanayopata wenzetu. Mazuri kwa mabaya. Tukiasili mbinu zao kuzifanya ziende na mazingira yetu, tutapata matokeo mazuri zaidi, IMHO.
Bado watu wanasongamana sana hapo Dsm vituo vya basi vijiweni watoto licha ya kufunga shule bado wanajikusanya uswahilini wanacheza pamoja, wenyeviti wa Serikali za mitaa hawataki kumsaidia Daud Bashite wamekalia kutegea watu wafe kwa wingi wapate sababu ya kuahirisha uchaguzi
 
Back
Top Bottom