Utafiti mpya wa kisayansi wa Covid19 – Msaada mkubwa wa kujikinga na kuzuia maambukizi kwa wengine

Utafiti mpya wa kisayansi wa Covid19 – Msaada mkubwa wa kujikinga na kuzuia maambukizi kwa wengine

X-bar,
Ndugu X-bar, samahani sana kujua toka kwako kwamba nimepotosha. Haijawahi kuwa nia yangu kupotosha mtu kwenye hili wala lingine lingine kokote. Niko tayari kurekebisha makosa maana lengo la nilichoandika ilikua ni kuelimisha.

For the record, sijasema popote nilichoandika ni amri ya 11 (kwamba ni absolute thruth). Dhana, utafiti, maoni, uchambuzi au ushauri wowote katika sayansi unaweza kukosolewa, kuchambuliwa, kuongezwa, kukanushwa, kurekebishwa, nk.

La muhim tu kwa anayefanya hayo afanye akiwa na malengo ya kuelezea ukweli mbadala (objectively) na sio kuishia kusema kuna upotoshaji. Ana wajibu wa kutoa ufafanuzi mzuri, wa kueleweka zaidi, na uliobeba ukweli.

Kwa mfano, ungetusaidia sana tunaosoma hapa kuelewa wewe unaelewa nini kuhusu infection dose kwenye muktadha wa maambuzi ya Covid19 na ni kwa jinsi gani hicho unachoelewa wewe ni sahihi kuliko au kinatofautiana na watafiti waliochapisha article niliyoirejea au nilichoandika mimi.

Mimi sina guts za kukuambia umepotosha, ila nina kiu ya kuelewa hicho ambacho hutaki kutuelimisha nacho. Kwa mfano:
  1. kupunguza infectious dose kwa kuvaa mask kwako ina maanisha nini kwenye kwa Covid19?
  2. Kwamba mask itakusaidia kuambukizwa virusi kumi badala ya 20 na hivyo utakua salama zaidi?
  3. Unaposema kuvaa masks ni njia kuu ya kujikinga unamaanisha nini na unatumia ushahidi ya kisayansi au logic "za wenye akili" kama ulivyosema?
  4. Unamaanisha aerosols zenye virusi zimejaa kila mahali mtu anapokua na sio location specific?
  5. Katika kutafuta upotoshaji kwenye nilichoandika, je umezingatia mazingira ambayo huu utafiti umefanyika kwenye kuangalia njia ya aerosols hewani (kwamba ni kwenye closed doors na sio kwenye open space)?

    Mwisho, ninataka kuamini wewe ni expert wa hiki unachokiongea na ndio mana unaongea kwa mamlaka kwamba nimepotosha. Kwa uelewa wangu experts (wa eneo lolote) huwa wanasoma updates za eneo lao (tafiti mpya), wanajielimisha kwa wasiyoyajua, na wanafuatilia experts wenzao duniani wanafanya/wanase nini. Hivyo sitegemei expert wa infectious diseases kunishangaa kwa nilichokisema kuhusu masks na kunawa mikono ambacho ni "common knowledge" katika mikakati ya kudhibiti Covid19.

    Otherwise, someone seems to have a serious personal problem with a messenger irrespective of the authenticity of his message. I bet this is not the case. Is it?

    MM Togolani
 
MM Togolani,
Wala huna haja ya kuogopa kwamba nina mamlaka ya kuongea kwa kujiamini kama bingwa. Mimi siyo bingwa. Bali yakupasa ukumbuke kwamba mchango wangu katika uzi wako huu ulikuja kwa mtindo wa swali lililolenga kupata ushauri/maoni au mtazamo wako kuhusu umuhimu wa matumizi ya maski kwa watu ambao hawajaambukizwa kulingana na matokeo ya utafiti uliofanyika kuhusu aerosols and stability ya virusi vya corona.

Zaidi nilitaka nijue maoni yako endapo matokeo ya utafiti huu yanakubaliana au yanapingana na maelekezo ya Dr. Janeth Mghaba wa Kitengo cha Magonjwa ya Mlipuko aliyekosoa uvaaji wa maski kwa watu ambao hawajaambukizwa.

Nilitegemea kupata shukrani kutoka kwako kama mdau/mtaalam wa magonjwa ya mlipuko kwa kukumbusha kuhusu wasio na maambukizi nao wavae maski ili wajikinge na "potentially contaminated aerosols". Lakini kinyume chake ukatoa majibu kwa namna ya kunikosoa eti corana ana kiherehere cha kuingia hata machoni na kwahiyo kuvaa maski ni kazi bure.

Kwa maoni yako ni kwamba maski haziwezi kumkinga mtu na covid-19 na kwahiyo hakuna haja ya kuzivaa. Umekazia hoja yako ya kupuuza uvaaji wa maski kwa kutaja vifo vya wahudumu wa afya huko Italia ambao huvaa mavazi maalum ya kujikinga (PPE) zikiwemo maski.

Labda tu nikukumbushe kitu ndugu yangu; uzi/darsa ulilotuletea ni sayansi. Moja kati ya misingi ya sayansi ni "falsifiability" (kukosoleka/kubishiwa) yaani mawazo au nadharia hazipaswi kutolewa kama hitimisho kwasababu kunaweza kupatikana ushahidi (empirical evidence) unaokinzana na kile tunachokiamini.

Hapa namaanisha kwamba, wewe kama mwanasayansi hukupaswa kupuuza moja kwa moja wazo langu kwamba mtu akivaa maski anaweza kusalimika na CoV zinazosambaa kwa aerosols. Kiufupi ni kwamba hukupaswa kuhitimisha kwamba "maski haizuii Cov" eti kwavile kuna wahudumu wa afya huko Italia wamepata maambukizi ya CoV.

Sasa kwa taarifa yako ni hivi ndugu yangu, kuna makumi hadi mamia ya tafiti zilizofanyika juu ya ufanisi/uwezo wa maski kuzuia vijidudu (vikiwemo virusi). Kila aina ya mask ina uwezo wake wa kuzuia vijidudu na wanasayansi wamezipa madaraja kulingana na uwezo wake kama vile FFP1, FFP2, FFP3, N95, surgical mask n.k. Baadhi ya maski zimetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora maalumu kwa mask (EN 149:2001) na kuidhinishwa na FDA au kuwekwa CE mark.

Lakini wakati wewe unapinga uwezo wa maski dhidi ya CoV, mataifa ya Korea inaaminika wamefanikia kwa kiasi kikubwa kudhibiti covid-19 kutokana na ukweli kwamba raia wote wanavaa maski. Zaidi ya hiyo, CDC, ECDC na WHO zinashauri uvaaji wa maski na wanatoa miongozo juu ya aina ya maski za kuvaa dhidi ya CoV (Guidance for wearing and removing personal protective equipment in healthcare settings for the care of patients with suspected or confirmed COVID-19) Miongozo ya kujikinga na CoV (PPE) kutoka kwa taasisi hizi za afya zinalenga kudhibiti njia zote zinazopelekea kusambaa kwa maambukizi ambazo ni
1. Respiratory protection (FFP2 or FFP3 respirators)
2. Eye protection (Goggles for face shield)
3.Body protection (Long-sleeved water-resistant gowns)
4. Hand protection (Gloves)

Ukweli ni kwamba huwezi kuwa "professional" kwa kushauri jamii kujikinga dhidi ya maambukizi ya CoV kwa kusisitiza kunawa mikono peke yake na kuacha kuvaa mavazi ya kujikinga (PPE) eti hadi mtu awe ameathirika. Mtu "smart" ni yule anayevaa PPE bila kujali ameambukizwa au la kwasababu kuvaa PPE kuna faida mbili kwa wakati mmoja; kunapunguza hatari ya kuambukiza wengine endapo mtu ameathirika na pia kunamkinga mvaaji dhidi ya hatari ya kuambukizwa na walioathrika. Hii ndio akili.

Lakini ile hoja yako kwamba kuvaa PPE dhidi ya covid-19 kunawahusu wahudumu wa afya tu wawapo kazini haina mana. Nasema haina mana kwasababu ugonjwa huu sio "nosocomial/occupational infection" tu bali ni janga la jamii yote na kwamaana hiyo anayepaswa kujikinga ipasavyo si wahudumu peke yao.

Yoyote anayelazimika kuingia kwenye "hot spots" na mwenye "access" na PPE na avae kadiri awezavyo; wala usijali eti utaonekana kituko "ukitokelezea" mtaani au ofini na muonekana kama mtu "aliyetua mwezini" au eti utasababisha "panic" kwa wengine! We jali uzima wako!

Lakini kama unapinga uvaaji wa PPE kwa wasioambukizwa kwa hoja kwamba kufanya hivyo ni kujiweka kwenye hatari ya kiafya, ulitakiwa kwanza ubainishe hizo hatari za kiafya na ikiwezekana kwa ushahidi wa kitaaluma. Vinginevyo ni hoja ya kupuuza. Mtu anatakiwa kwanza alinganishe hizo "hatari za kiafya" zitokanazo na uvaaji wa maski na hatari ya kupata covid-19 ndipo aamue kuvaa au kuacha kuvaa. Kama kuvaa maski ni hatari zaidi kuliko covid-19 ni bora kuacha kuvaa; na ikiwa ni kinyume chake kulingana na mtazamo wake basi na avae kadri atakavyo lazimika.

Asante sana.
 
X-bar,

Ndugu,

Pamoja na majibu mazuri. Nijaribu kufafanua maeneo machache.
  1. Naona umerudia nilichosema mwenyewe kwenye majibu yaliyotangulia.Hoja ya kwamba nilichoandika kinaweza kupingwa nimeiongelea mwenyewe na nikasisitiza anayepinga anasaidia kuweka mwanga kama ulivyofanya. Sijajua why umeirudisha tena kama hoja mpya.
  2. Kuhusu kusema Italy wamefariki wanaovaa masks, haikua msingi wa hoja yangu bali nilitoa kama mfano tu kusisitiza hoja ya kwa nini masks sio kinga. Kutumia neno "kiherehere cha Covid19" isikupe shida. Nadhani tatizo ni hatufahamiani tu. Katika uandishi wangu (kwenye makumi kama sio mamia maandishi na michango yangu mitandaoni), ninapenda kutumia "lugha za kuchomekea" kumsaidia anayesoma asisome akiwa kakunja ndita muda wote kama anapigana. Hivyo nilidhani ungelisoma kwa muktadha huo ila naona wewe ulisoma ukiwa umevaa miwani kali ya ya kuchomelea vyuma (same style) na imekupa hasira zaidi ya kuniona naposha. Pole na samahani.
  3. Wewe unakazia umuhim wa masks kiafya katika ujumla wake wa kumsaidia mtu kujiepusha na hewa chafu na maambukizi hasa yanayosambaa kwa mfumo wa hewa. Kusema ukweli hii ni common knowledge ambayo sidhani kama tunatakiwa kujadili hapa. Tunachoongelea hapa ni tatizo specific (Covid19) na kama nilivyosema awali, huu sio ugunduzi wangu. It is an expert opinon which is all over in scentific dicussions on Covid19.
  4. Sijaelewa ushahidi wa WHO wa matumizi ya masks unauchukua ni upi maana nikitazama HAPA kwenye website yao wanapoongelea Covid19 wanashauri nilichoshauri mimi: kwamba mtu ambaye hana maambukizi (kwa maana ya hajawa na dalili za kukohoa, chafya, nk) hana haja ya kuvaa masks. Tazama hapa : When and how to use masks
  5. Maswali na maelezo yako umeyatoa katika mtizamo wa kisayansi. Ila napata shida kidogo kuelewa unaposema, "mataifa ya Korea inaaminika wamefanikia kwa kiasi kikubwa kudhibiti covid-19 kutokana na ukweli kwamba raia wote wanavaa maski". Hii ya kuaminika ni myth maana haina ushahidi wowote. Halafu Korea wamefanikiwa wapi wakati ni moja ya nchi zenye cases nyingi na hata leo kuna cases mpya 147 na vifo vipya 8? Korea na China mlipuko ulipoanzia na kukumba idadi kubwa ya watu, wapi wanavaa zaidi masks (iwapo una data)? Kwa hiyo ni sahihi kutoa hitimisho kwamba nchi zote zilizoathirika sana ni kwa sababu watu hawavai masks na zilizo na wagonwa wachache ni kwa sababu wanavaa masks?
  6. Nimejaribu kutazama nilipoandika lakini sijaona mahali nimesema kubaa masks kunatakiwa KWA WAHUDUMU WA AFYA TU. Nimesema zinafaa kuvaliwa na wenye maambukizi tayari (kukinga wengine) pamoja na wahudumu wa afya maana wao tayari wako kwenye risk ya kuwa exposed kwa sababu wanahudumia suspected and confirmed cases. By the way, nilisisitiza kwamba wao hawavai masks pekee bali wana kinga za mwili mzima (at least majority niliowaona).
  7. Ulichodemand nifanye kwenye paragraph yako ya mwisho is beyond the scope of what I intended to share on this forum. Sikua na lengo na sio mpango wa kufanya competitive analysis ya uvaaji wa masks na madhara yake kiafya. Kwa wataalamu wanahotaji evidence za aina hii kama wewe ili itusaidie katika hali ya kupambana na Covid19, nadhani wanaweza kutusaidia kufanya hivyo.

    Mwisho naomba tukubaline kutokukubalina. Sio kila hoja lazima watu wakubaline, much more katika scientific community. Wewe endelea kusisitiza uvaaji wa masks kama njia ya kujikinga na Covid19 na ikiwezekana andika kabisa uchambuzi wa kitaalamu kuhusu hilo ili tuusome. Mimi nitaendelea kusisitiza kwamba kuvaa masks kama njia ya kujikinga kwa mtu ambaye hajaathirika na hayuko katika eneo hatarishi kama kuhudumia au kuongea na waathirika, HAINA TIJA. Ni kujisumbua, kujichosha, na kujiweka kwenye hatari ya mambuziki mengine hasa kwenye mazingira ya uvaaji huokatika nchi yetu.

    MM Togolani
 
X-bar,
Nimeruka jambo moja.

Uvaaji wa PPE kama kinga sijapinga popote. Nadhani moja ya majibu yangu nilikuambia unaweza kuvaa sio to mask bali na miwani na suti. Unasema mtaalamu anatakiwa atoe huu ushauri. Ni sawa.

Ila kwenye kutoa ushauri wa kitaalamu huwa tunazingatia sana "context and practicability of the proposed solution". Pamoja na uzuri wa ushauri wa kitaalamu ( hasa unaolenga population kubwa), lazima utazame mazingira halisi ya watu unaowashauri, mazingira ya utekelezaji wake, uwezo, uhalisia, upatikanaji, . Duniani kote sijaona serikali wala wataalamu wanaoshauri watu wavae PPE kama protection gear za kujikinga na Covid19.
  1. Hebu piga picha unakwenda kazini, madukani, stand ya bus, au sokoni halafu kila unayekutana naye kavaa kama wanavyovaa wahudumu wa afya.Ninaamini utakua unaelewa ni kwa jinsi gani hilo pekee litakua ni chanzo cha tatizo kubwa la kiafya (hofu, wasiwasi, panic, mental health, etc) kuliko hata Covid19.
  2. Pili, ni watanzania wangapi wanaweza kununua hizo gear hasa wakati huu ambapo watu wote 55M wanatakiwa kujikinga? Tukitaka kuvaa wote (assume tuna huo uwezo) kuna supply ya kutosha?
  3. Tutatekelezaje majukumu yetu kila mtu akiwa ndani ya full protection gear muda wote?
  4. Chukulia tu madhara ya ushauri unaotelewa na ninyi munaodai uvaaji wa masks ni kinga na wale wanaosisitiza matumizi ya sanitisers. Umeona panic wananchi waliyopata na aina za masks zinazovaliwa?

    Makosa ya ushauri wa jumla jumla kama huu unaouita ndio wa kitalaamu (kwamba nilitakiwa niseme kila mtu avae PPE), ndio yamepelekea nchi za kiafrika kuibuka na solutions za kupanic kuwaambia watu "work from home" huku asilimia kubwa ya watu hawana umeme, maji, intenet ni shida na ni ghali, na wengi computer wanaiona makazini. Pia, asilimia kubwa ya kazi ni ambazo zinafanyika ndani ya kituo cha kazi tu.

    Pia unakimbilia kufunga shule ukiwa na mgonjwa mmoja huku watoto na vijana wakiwa sio kundi hatarishi kuambukizwa wala kusambaza maambukizi. Pia kukiwa hakuna mpango wowote wa nini kitaendelea muda watoto wamefunga shule na hakuna miundombinu wezeshi ya kuwasaidia kujifunza wenyewe wakiwa nyumbani. Wenzetu wamefunga shule na vyuo wakati epidemic imefikia kiwango cha juu na kukiwa kumeandaliwa utaratibu wa kujifunza kutokea nyumbani na mifumo wezeshi ipo.

    "CONTEXT"

    MM Togolani
 
X-bar,
Nimpe pongezi sana Togolan kwa kiweka Tafsiri ya Wanasayansi toka USA! amewaomba wana JF members kuvumilia pale alipotoa tafsiri isiyo rasmi kwa chapisho lake!!

Pia ame acknowledge kwa yeyote mwenye ufahamu zaidi, azidi kutuelimisha lakini pia kumuelimisha na yeye!! yeye hajui kila kitu*

Nikuombe Mkuu X-Bar, usimkatishe tamaa mtoa mada, kwakuwa kabla ya yeye kuleta mada hii sisi tulikuwa kimya pamoja na ufahamu wetu juu ya mada hii!!

Tunaomba kurekebisha pale alipokosea na sio kukaa kimya au kusema utaleta elimu pale utakapoona inafaa!! sisi walaji tunabaki hatujui ukweli ni upi!! na hichi ni kipindi ambapo elimu inafaa na sio wakati mwingine.

Ahsante!
 
Hizo disnfecting sprays Tanzania zinapatikana wapi na kwa bei gani? Kwa wanaojua tusaidiene maelezo ya hilo swali langu.
MM Togolani,
 
MM Togolani,
Kaka Togolani, kwa faida yako, yangu na wana JF wanaotusoma ningependa niweke sawa jambo tunalolumbana mimi na wewe. Jambo tunalobishaniana hapa ni dogo sana; UMUHIMU WA KUVAA MASKI KAMA KINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA COVID-19. Kuna maswali madogo madogo yanayopaswa kujibiwa katika somo hili kama ifuatavyo.

1. Je, maski zina uwezo wa kuzuia virusi vinavyosababisha covid-19?
2. Nani anapaswa kutumia maski; aliyeambukizwa, asiyeambukizwa au muhudumu wa afya?
3. Katika mazingira/mahali gani yatupasa kuvaa maski kunapotokea mlipuko wa corana?
4. Je kunawa mikono peke yake bila kuvaa maski inatosha kujikinga na covid-19"
5. Je, inatosha kudhibiti covid-19 kwa kuruhusu matumizi ya maski kwa walioambukizwa au watoa huduma tu na kushauri wasiombukizwa kutembea midomo na pua wazi palipo na mlipuko wakati tayari tunajua ugonjwa huu unaambukizwa kwa hewa?

Lakini nasikitika sana kuona umeamua kutonielewa na kuendeleza ligi tena kwa njia ya kunishambulia eti nimekunja uso kwa hasira kwavile ninasoma hoja zako nikiwa nimevaa mawani ya mafundi vyuma. Katika kuendeleza ligi kukwepa kukubaliana na hoja au ushahidi ninaotoa unakosa "consistence" (unajichanganya) katika kauli zako. Lakini ninapokupa hoja au ushahidi nzito wa mawazo ninayoyatetea, unahamisha mada. Labda nikuoneshe jinsi unavyojichanganya, kuhamisha mada na kukwepa hoja kama ifuatavyo.

1. Mwanzoni kabisa ulipinga matumizi ya maski kwa hoja zifuatazo,
a) nanukuu "...maski hazina msaada wowote kumkinga mtu kama wewe sio tabibu unayehudumia wagonjwa wa covid-19" . (majibu yako # 16).

Je, ikiwa mtu ana access na maski na ana elimu ya matumizi yake haitamsaidia eti kwavile mtu huyo sio tabibu? Yaani unataka kutuambia kuwa maski zimetengenezwa mahususi kwa madaktari na siyo kwa matumizi ya jamii inapotokea majanga ya milipuko inayosambazwa kwa hewa kama hii covid-19?

2. ".....hakuna ushahidi wa kitafiti ulioonesha uvaaji wa maski ni kinga." (Majibu yako #36). Nilipokujibu kuwa kuna zaidi ya mamia ya tafiti zilizofanyika kuonesha ufanisi/uwezo wa maski kuzuia vijidudu vikiwemo virusi na maski zimewekwa katika madaraja kutokana na uwezo wake, ukahamisha na kukwepa ukweli kwa kudandia hoja nyingine ya virusi kupitia machoni pale uliposema kwenye majibu yako #36, nanukuu "....masks siyo kinga maana haizuii wewe kujishika macho wala droplets kuingia machoni".

Hili siyo swali nilililouliza; mimi sijauliza kuhusu ufanisi wa kinga ya machoni (goggles) bali nimespecify kwenye mask; je maski inaweza kuzuia virusi vya corona kupenya na kumuingia mtu kupitia mdomoni na puani na siyo machoni kwakuwa maski haikingi macho. Nilihitaji ujibu hoja je, endapo mtu atavaa "full PPE" je SARS-CoV-2 vitapenya kwenye mask?

Lakini kama kweli hakuna utafiti unaoonesha maski ni kinga kwanini wahudumu wa afya na wagonjwa wanatakiwa wazivae? Kwanini taasisi za afya kama WHO, CDC na ECDC wanatoa miongozo juu ya kuvaa maski kwa ajili ya corona wakati hawana ushahidi kuwa maski ni kinga?

3. Lakini ili kukwepa na kuponda hoja zangu zinazotetea umuhimu wa kuvaa mask na PPE zingine dhidi ya covid-19 kwa jamii yote, ukakimbilia kwenye suala la upatikanaji na gharama za maski kwamba ni "impracticable". Wewe unapenda sana kusisitiza tuangalie "context" na wakati huo huo mwenyewe huzingatii hiyo context katika kujibu hoja zangu. Context ya somo hili siyo practicability, availability wala cost, bali ni "effectiveness" ya mask kama sehemu ya PPE dhidi ya corona kwa jamii yote, wahudumu, waathirika na wasioambukizwa.

Lakini kwa kuwa naona unatapatapa sana katika hoja ni vema nipitie hoja zako muhimu katika majibu yako hapo juu kama ifuatavyo.

Hoja 4.Sijaelewa ushahidi wa WHO wa matumizi ya masks unauchukua ni upi maana nikitazama HAPA kwenye website yao wanapoongelea Covid19 wanashauri nilichoshauri mimi: kwamba mtu ambaye hana maambukizi (kwa maana ya hajawa na dalili za kukohoa, chafya, nk) hana haja ya kuvaa masks. Tazama hapa : When and how to use masks

Jibu langu: Hakuna ubishi kwamba mtoa mada umeamua kwa makusudi kutokubaliana na hoja zangu. Nimeshasema hapo juu kwamba suala siyo namna ya kutumia mask (how to use) na wala siyo wakati gani mask zinapasa zivaliwe (when to use). Hoja yangu ni je maski zina uwezo wa kuzuia corona. Lakini utakuwa unashangaza sana kusema kwamba tips za WHO ulizozitoa zinapinga kwamba maski zinazuia corona.

Bila shaka umeichukulia kibubusa tip inayosema "...because there is no evidence that they (masks) protect people" na ukaifanya kuwa ndo ushahidi kwa mujibu wa WHO kwamba maski si lolote si chochote katika kujikinga na corona. Hatari sana. Ingekuwa kweli WHO hawaamini uwezo wa maski dhidi ya corona wasingetoa tips/tutorial juu ya matumizi yake.

Vinginevyo ni sawa na mtu akukataze kutumia bangi na bado mtu huyo huyo akufundishe jinsi gani bangi inatumika. Lakini kwanini mtu afundishe matumizi ya kitu kisicho na manufaa? Inabidi ujifunze kuelewa misingi ya hoja na sio kuzikariri kiupofu upofu.

Tambua kuwa msingi wa statement hii ni ukweli usiopingika kwamba "..medical masks cannot protect the new coronavirus when used alone" kama walivyoelezwa kwenye tutorial. Kauli hizi mbili zikiunganishwa inaweza kusomeka "There is no evidence that medical masks when used alone can protect people from the new corona virus".

Lakini ni muhimu kutambua kuwa kukosekana kwa ushahidi wa uwezo wa maski kuzuia CoV, maana yake ni kwamba hakuna utafiti uliowahi kufanyika kuhusu uwezo wa maski dhidi ya corona. Wala hatupaswi kupuuza uwezo wa maski kwa misingi ya kukosekana ushahidi wa kitafiti kwa maana utafiti ukifanyika unaweza kutoa ushahidi ku-prove otherwise.

Lakini katika kukazia precaution hii "mtaalamu" wa WHO kwenye tutorial ameongeza kuwa "when you wear them, you must combine them with hand hygiene and other preventive measures". Statements hizi zote tunaweza kuzi-rephrase kama ifuatavyo "Medical masks cannot protect people from the new corona virus unless used in combination with hand hygiene and other preventive measures".

Hapa sasa utaona kuwa maski ina uwezo wa kuzuia corona endapo mvaaji atazingatia masharti yake (kuchanganya na kinga zingine na usafi wa mikono)

Kauli ya WHO kwamba combine the use of masks with hand hygiene and other preventive measures haipuuzi/haipingi uvaaji wa mask dhidi ya corona. Bali kauli hii ndiyo niliitarajia kusikia kutoka kwako katika kukubaliana na mimi kuwa kunawa mikono kunatakiwa kuwe complemented na matumizi ya PPEs kama vile masks (mdomo na pua) gogles (macho) na gloves (mikono) endapo mtu atalazimika kuwepo kwenye "hot spots".

Ninaposema "hot spots" ninamaanisha PPE zivaliwe kwenye mazingira hararishi ambayo WHO wametumia term "specific cases" na siyo kila wakati au kila mahala. Kumbuka nimetumia neno hili karibu kwenye maandiko yangu yote kuchangia bandiko hili kuonesha wapi PPE zivaliwe.

Asante sana.
 
Hata mimi nimeshitukia hapo

Ndugu Herbert Nkuluzi, ukweli ni kwamba sio Coronavirus pekee wanaokufa kwa half-life decay. Hii ni tabia ya virusi wengi hasa wanaotushambulia kwenye mfumo wa upumuaji. Njia nyingi ya virusi kutokomea ni kua inactivated kwa matumizi ya disinfectant kama sanitisers (yaani unakua kama vile umewachomolea batteries vile), au kuwa destroyed kwa kua exposed kwenye joto kali au miozi (kuwapiga bomu la maangamizi). Wanapoingia kwenye miili yetu wanaangamizwa ama kwa dawa (inategemea na kirusi) au mwili kupambana nao kwa mfumo wake wa kujilinda (immunity) kama tunavyopona mafua bila tiba. Wengine kama yule anayekomesha species ya wanyama inayoitwa "Homo Sapiens", wao wamevaa bulletproof na kisha kujificha kwenye underground banker (naogopa kuwataja).

Half-life decay ya virusi tunaweza sema ni kupungua au kufa nusu ya idadi ya walio hai na ambukizi exponentially kila baada ya muda fulani. Kumbuka wako kwa wingi sana hata katika tone moja tu. Kalamu1 alifafanua vizuri process hii kwa kutumia mfano wa kuku.

Kumbuka hata kwenye chemistry tunapozama half-life decay ya radioactive element tunaangalia ni kwa muda gani nusu ya atoms (basic unit of matter/elements) zake zitakua zimepungua (eg.converted into energy) hadi zinapoisha. Hivyo kinacho-decay ni kundi la atoms na sio atom moja moja au element nzima as one unit.

MM Togolani
 
X-bar,
Ndugu X-bar nashukuru kwa maelezo mazuri sana na hoja zinazopangiliwa vema. Natamani ningekua na muda nami nirejee mjadala mzima na kujibu hoja moja moja kama ulivyofanya wewe. Hata hivyo niseme machache kwa haraka kidogo:
  1. Mambo mengi uliyoeleza hapa yako kwenye tulipojibizana (wewe umeita ligi) hivyo umerudiarudia mulemule. Kama nilivyotangulia kusema, nilichoandika awali sikusema popote ni timilifu wala kinajitosheleza kwa kila kitu. Na zaidi sana katika kujibizana, nimejaribu kufafanua na kuongeza maeneo mengi tu ambayo sikutaja awali hasa kwenye hili la matumizi ya masks.
  2. Nirudie kusema kwamba matumizi yangu ya maneno kama virusi wana kiherehere, kuvaa miwani ya kuchomelea chuma, nk.. hayana maana unazolazimisha. Nilishasema ni utani na kama umekukwazika jitahidi kuruka hayo maneno.
  3. Nikiri una uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kutetea unachokifahamu. Ila nasikitika kwama jumbe zako zimeambana na dharau nyingi kwa unayemjibu hivyo kuondoa objectivity ya hoja zako. Sidhani kama mtu anaonekana wa maana, mwenye akili zaidi na mjuaji sana anapolazimika kuambatanisha kejeli na dharau anapotofautiana hoja na mtu mwingine. Nikupe mifano michache ya ulivyonirejea:
    1. Unatapatapa
    2. unapotosha
    3. Unahamisha mada
    4. watu wenye akili
    5. kuchukua kibubusa
    6. unapenda ligi
    7. najichanganya
    8. nakariri kiupofu upofu
  4. Sijawahi kuwa na muda wa ligi za kubishana for the sake of kubishana. Muda wote niliotumia hapa niliutumia kwa adabu zote nikijua tunajadiliana, naendelea kujifunza, na ninaondoa tofauti za hoja zilizojitokeza. Sikua napoteza muda wala natafuta ligi.
  5. Nikisoma baadhi ya hoja zako, iko kama kuna namna ambayo wewe ulitaka niongee kwa nilichoandika. Hiki hakiwezekani kwa kua nimeandika kwa mtizamo na uelewa wangu. Kama nina namna nzuri zaidi ya kuelimisha watu, nadhani badala ya mimi kumshambulia kwa kajeli ninayedhani haelewi sawasawa, nitadanya mimi kwa namna nyingine kutoa alternative.

    Nikushukuru tena kwa mchango wako ambao kuna maeneo umejadili vizuri. Ila nadhani mimi ni dhaifu wa kujadiliana na mtu ambaye anatanguliza dharau na kejeli kama namna ya kujenga hoja. Hivyo sitaendelea na mjadala nawe kwenye hili kwa ajili ya nafsi yangu na nisije nikakose wanaotusoma. Kama kuna lolote baya kote nilipojibizana nawe au limebeba tafisri mbaya, tafadhali samahe. Haikua nia yangu.

    God bless you.

    MM Togolani
 
MM Togolani,
Tusameheane ndugu yangu. Mimi ni mstaarabu kama wewe na siwezi kukusudia kukushambulia. Lakini ndio maana kama utakumbuka kwenye mchango wangu wa mwanzo kabisa niliandkika kwa heshima "Hivi Mkuu kutokana na matokeo ya utafiti huu huoni kuwa kuna haja......."

Nakili nilikosea sana kutumia neno "umepotosha" na huwezi amini nilijutia sana kusema hivyo hasa pale uliposema haikuwa lengo lako kupotosha na ukaniomba msamaha wakati mimi ndiye nilikosea.

Lakini nashukuru kwamba angalau sikuendelea kufafanua huo upotofu licha ya kunitaka nifanye hivyo.Nisamehe ndugu yangu. Lakini nikili tu kwamba kuna seheme nimekuta umeelezea vizuri concept ya half-life labda hii ndo ilinifanya kukaa kimya.

Ukweli nimelipenda bandiko lako kwa vile linazungumzia sayansi tena juu ya janga muhimu tunalokabiliana nalo. Nakupongeza kwa juhudi zako za kufuatilia sayansi zinazoendelea juu ya ugonjwa huu na kutupa update kwa haraka kuifundisha jamii kufahamu na covid-19 na namna ya kujikinga kwa kutumia matokeo ya utafiti mpya kabisa.

Naomba kila utoapo mada humu niunge ili nami nichangie inapobidi.

Kila la kheri ndugu yangu.🙏🙏
 
Back
Top Bottom