Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Juzi tulikua tunajadili Yule mwanamke alomng'ata mmewe mpaka kuelekea logo chake.Basi katika stori mi na mr.nikmwambia lakini si sheria inasema kuvumilia katika shida na Raha.Mr.ananiambia inabidi sa hivi hicho kipengele kinadilishwe au waspesfy kabisa ni shida zipi.


Kiukweli ndoa nyingi zipo ICU ndani japo nje zinaonekana hai.
 
Hakuna mwanaume aliyekubali kuhudumia familia 50/50

Mimi mwanaume si ndio nimeanzisha familia basi ni wajibu wangu niitunze
Wewe jisemee mwenyewe usiwasemee wanaume wote isitoshe hapa tunaongelea wanaume na wanawake wote duniani hatuongelei wa jamii fulani tu, ni wanaume wangapi kila siku wanalalamika kwamba wanawake ni wavivu hawataki kutafuta pesa wanasubiri kuhudumiwa kama walemavu, wewe mwenyewe umetoka kusema kwamba wanawake wana njaa ndio maana hawawezi kuachika kwenye ndoa sasa kama mnajua ni wajibu wenu kuwahudumia kwanini huwa mnawasema kwamba wana njaa
Sasa mbona mnawasimanga na mnawanyanyasa kwa kigezo cha kwamba mnawahudumia
Ndio maana nikasema kwenye hii dunia siyo kila mtu anaamini unachoamini wewe na siyo kila mtu anayaona mambo kama unavyoamini wewe, wewe kama unaona ndoa lazima iwe na kiongozi ni sawa ila tu tafuta mwanamke ambaye atakuwa na mtazamo kama huo wako lakini kuna wengine wanaona siyo lazima ndoa iwe na kiongozi wote mkishirikiana na mkisikilizana ndio vizuri, kwahiyo ni wewe tu kuchagua mfumo unaotaka na hakuna mfumo ambao ndio guarantee ya ndoa kudumu maana ndoa zinazovunjika ni zenye mifumo yote
Nini maana ya mfumo dume?
Ni mfumo ambao wanaume ndiyo wanakuwa watawala
 
Mimi sina shida na hilo mkuu as long as mwanaume ndio provider wa kila kitu bila kutaka mke wake amsaidie, haki sawa inawafaa wale wanaume ambao wanataka wake zao wawasaidie majukumu ya kuendesha familia kiuchumi, kwahiyo wakati mnanukuu hivyo vifungu mkumbuke pia kuwa mwanaume hakuumbwa kuwa mtawala tu bali pia aliumbwa kuwa provider
 
Basi hukunielewa mimi nilimaanisha wanaume ambao wanataka wake zao watimize majukumu yote ya nyumbani hawana budi kuoa wamama wa nyumbani, na wanaume ambao wanataka wake zao wawasaidie kuendesha familia kiuchumi hawana budi kuoa wafanyakazi au wafanyabiashara, ndoa kuvunjika ni matokeo ya mwanaume kuoa mwanamke ambaye hawezi kumpa kile alichokitarajia na kiuhalisia huwezi kupata vyote hivyo kwa mwanamke mmoja ni lazima ukubali kuchagua kimoja na kupoteza kimoja
 
Mkuu kujitoa kunaendana na uwezo wa mwenza wako, kama kweli mtu anampenda na anamjali mwenza wake, sidhani kama atakubali abebe majukumu mengi kuliko uwezo wake eti ili amfurahishe yeye
 
Upendo Hauna balance.
Kila mmoja ana jitahidi Kwa kadri awezavyo kutokana na fursa na vipawa alivyojaliwa na mwenyezi Mungu, kumfurahisha mwenzie.
Mkuu kwa kifupi ni kwamba kilichowafanya wanawake wa leo waache kujitoa kwa wanaume ni wanaume kutokuwa na upendo wala shukrani kwao simple as that
 
Mkuu hivi katika muktadha huo kati ya wanaume na wanawake ni kina nani wanaotafuta ulinganifu, kama hamtaki ulinganifu basi kila mtu afanye majukumu yake maana hata wanawake wakifanya vyote nanyi hamtakuwa na thamani kwao, wewe endesha familia kiuchumi mke asimamie majukumu ya nyumbani hapo ndio mnaweza mkaleta hizo story zenu za utawala na hizo blah blah nyingine
 
Hilo swali lako hapo mwishoni ndilo ulilotakiwa uanze nalo kabla hujaandika yote hayo, ambayo mimi hakuna mahali nimeyasema maana clearly unaonesha kabisa hukunielewa, kindly rudia tena kusoma comment yangu na ya yule jamaa niliyemquote then ndio utaelewa
 
Ndoa asili yake sio usawa.
Itakapofikia hapo kwenye usawa,
Ni pale ambapo mahali litaondolewa kuwa takwa la kufunga ndoa.
Hakuna shida siku mtakayokubali wanawake waache kutumia majina ya waume zao, na watoto nao waanze kutumia majina ya koo zote mbili wa mama na wa baba basi bila shaka utaratibu wa mahari utafutwa tu, maana hilo ndilo lengo kubwa la mahari mengine yote ya sijui kujitunza ni porojo tu
 
Sawa sasa kama mmeshajipata kwanini msumbue wake zenu wawasaidie majukumu yenu ya kuendesha familia kiuchumi, tena kama nikishajua mwanaume mwenyewe ndio kama wewe basi hutakaa uone hata mia yangu, nitasimamia majukumu yangu yote ya nyumbani ila na wewe hakikisha hizo pesa zako hazikati yani shida yoyote ya kipesa ikitokea unaisolve mwenyewe
 
Bwebwe nyingi ila ndoa ikishanyoosha mikono juu imeishaa hiyoo...
 
ndo ujikute umeoa mtu mjinga kama huyu, kesho yake tu unamnyonga au unamuwasha moto kwa gunia mbili za mkaa
Jadili hoja acha hasira za kipumbavu, aliyekuambia kwamba mimi nina shida ya kuolewa na wanaume wajinga nani, kwa wanawake wa dunia ya leo mjiandae tu kisaikolojia vinginevyo mtawachoma hadi waishe mbaki wenyewe mkafie jela
 
Sasa shida za wanawake ninyi huwa mnazivumilia hebu tuongee tu ukweli ndugu yangu, ni wanaume wangapi wanaweza kuvumilia wanawake wasaliti, wavivu, wabishi na wajeuri nk, lakini wanawake wanalazimishwa kuwavumilia wanaume wenye tabia kama hizo
Wewe hufai kuwa hata kwenye ndoa kabisa
 
Uzuri kuna wanawake wanaofanya vyote bila kelele.
Acheni kuwadanganya wenzenu humu, yani ni sawa na wanawake wadanganyane kuwa kuna wanaume wanaoweza kufanya vyote, kama hao wanawake wangekuwepo basi kusingekuwa na malalamiko kutoka kwa wanaume kwenye ndoa nyingi
 
Wewe hufai kuwa hata kwenye ndoa kabisa
Kuliko kuwa kwenye ndoa ya namna hiyo kwakweli ni heri nisifae tu, acha wanawake walio desperate na wenye low self esteem waendelee kuhangaikia ndoa za aina hiyo, wanawake wanaojielewa washatoka huko
 
Yaani dada uko vzr sana unajielewa kwelikweli natamani ungekuwa make wangu aise, sikujua kuwa bado wanawake wenye akili mpo bado ila ni nyie wa zamani kidogo sio hivi vibinti vya 90. Hongera sana my dear
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…