Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Siyo ndoa za mikataba tu, Bali Kile kiapo kiandikwe upya.

Kiapo cha ndoa kinasema utamvumilia katika shida na Raha na maradhi, lakini jinsia ya Ke wengi wao kiapo hiki wamekariri kipengele cha wakati wa raha tu.

Kuna Jamaa yangu mmoja ilibidi Mimi niingilie Kati nimwambie mke wake ukweli Jamaa Hana pesa, kuna pesa anaidai kwangu ziko kwenye process ya kulipwa.

Imagine kuna mwanamke hataki kusikia lugha ya kumwambia wiki hii mipango yangu kipesa haiko Sawa kama Una akiba okowa jahazi nyumbani, sasa kuna haja gani ya kuwa na ndoa hapo? Ndoa ya upande mmoja?
Juzi tulikua tunajadili Yule mwanamke alomng'ata mmewe mpaka kuelekea logo chake.Basi katika stori mi na mr.nikmwambia lakini si sheria inasema kuvumilia katika shida na Raha.Mr.ananiambia inabidi sa hivi hicho kipengele kinadilishwe au waspesfy kabisa ni shida zipi.


Kiukweli ndoa nyingi zipo ICU ndani japo nje zinaonekana hai.
 
Hakuna mwanaume aliyekubali kuhudumia familia 50/50

Mimi mwanaume si ndio nimeanzisha familia basi ni wajibu wangu niitunze
Wewe jisemee mwenyewe usiwasemee wanaume wote isitoshe hapa tunaongelea wanaume na wanawake wote duniani hatuongelei wa jamii fulani tu, ni wanaume wangapi kila siku wanalalamika kwamba wanawake ni wavivu hawataki kutafuta pesa wanasubiri kuhudumiwa kama walemavu, wewe mwenyewe umetoka kusema kwamba wanawake wana njaa ndio maana hawawezi kuachika kwenye ndoa sasa kama mnajua ni wajibu wenu kuwahudumia kwanini huwa mnawasema kwamba wana njaa
Sasa mbona mnawasimanga na mnawanyanyasa kwa kigezo cha kwamba mnawahudumia
Umekumbuka ulisema haki sawa inamaanisna kwenye ndoa kila mtu ajiamulie mwenyewe hakuna mambo ya mke kumtii mume. Unafikiri hapo ndoa itakuwaje?

Tena ukasema haki sawa yaani 50/50 ikiwezekana hata kwenye kuhudumia familia wakati ni haki yenu kuhudumiwa mkiolewa
Ndio maana nikasema kwenye hii dunia siyo kila mtu anaamini unachoamini wewe na siyo kila mtu anayaona mambo kama unavyoamini wewe, wewe kama unaona ndoa lazima iwe na kiongozi ni sawa ila tu tafuta mwanamke ambaye atakuwa na mtazamo kama huo wako lakini kuna wengine wanaona siyo lazima ndoa iwe na kiongozi wote mkishirikiana na mkisikilizana ndio vizuri, kwahiyo ni wewe tu kuchagua mfumo unaotaka na hakuna mfumo ambao ndio guarantee ya ndoa kudumu maana ndoa zinazovunjika ni zenye mifumo yote
Nini maana ya mfumo dume?
Ni mfumo ambao wanaume ndiyo wanakuwa watawala
 
Mkuu ndoa haina haki sawa, ndoa ni mpango wa Mungu mwenyewe, mambo ya haki sawa yaache kazini kwako ukiingia ndani mume ndio mwenye sauti, na huo mpango wa Mungu uko hivi:

Mwanzo 3:16
[16]Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mimi sina shida na hilo mkuu as long as mwanaume ndio provider wa kila kitu bila kutaka mke wake amsaidie, haki sawa inawafaa wale wanaume ambao wanataka wake zao wawasaidie majukumu ya kuendesha familia kiuchumi, kwahiyo wakati mnanukuu hivyo vifungu mkumbuke pia kuwa mwanaume hakuumbwa kuwa mtawala tu bali pia aliumbwa kuwa provider
 
Jadda , pale mwanzo ulisema. Wanaume wanapaswa kuchagua mama wa nyumbani zidi ya wanawake wanao fanya kazi au wafanyabiashara. Kwa kua hao wanaofanya kazi,hawawezi kutimiza majukumu ya nyumbani.
Hivyo nikauliza kuwa kwa maana hiyo mwanamke akiwa mfanyakazi ni tiketi ya ndoa kuvunjika?
Basi hukunielewa mimi nilimaanisha wanaume ambao wanataka wake zao watimize majukumu yote ya nyumbani hawana budi kuoa wamama wa nyumbani, na wanaume ambao wanataka wake zao wawasaidie kuendesha familia kiuchumi hawana budi kuoa wafanyakazi au wafanyabiashara, ndoa kuvunjika ni matokeo ya mwanaume kuoa mwanamke ambaye hawezi kumpa kile alichokitarajia na kiuhalisia huwezi kupata vyote hivyo kwa mwanamke mmoja ni lazima ukubali kuchagua kimoja na kupoteza kimoja
 
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
1 kor 13:4-8.
Nina mashaka na tunda la upendo kuwepo Kwa wanandoa wengi.
Nonabyofahamu Mimi, palipo na upendo kila mmoja hujitahidi kujitoa kufanya jambo Kwa ajili ya kumpendeza mwenzie, kadhalika hujizuia kutofanya lolote ajualo kwamba litamchukiza mwenzie.
Ndoa nyingi zimevunjika na nyingine zimekufa kivitendo sababu mwanandoa mmoja au wote waliacha kujali Wala kuthamini hisia za wenza.
Mkuu kujitoa kunaendana na uwezo wa mwenza wako, kama kweli mtu anampenda na anamjali mwenza wake, sidhani kama atakubali abebe majukumu mengi kuliko uwezo wake eti ili amfurahishe yeye
 
Upendo Hauna balance.
Kila mmoja ana jitahidi Kwa kadri awezavyo kutokana na fursa na vipawa alivyojaliwa na mwenyezi Mungu, kumfurahisha mwenzie.
Mkuu kwa kifupi ni kwamba kilichowafanya wanawake wa leo waache kujitoa kwa wanaume ni wanaume kutokuwa na upendo wala shukrani kwao simple as that
 
Tukifanya vyote , mwanamke hata kuwa Tena na thamani kwetu.
Wanawake, msitafute ulinganifu.
Kiasili sisi ni watawala wenu.
Tunaweza kufanya chochote Kwa kujisikia. Hii haituongezei Wala kutupunguzia nafasi kwenye utawala wetu, kama ambavyo mfanyakazi hawezi kijaji kumuwajibisha bosi wake.
Halafu mwatafuta ulinganifu ili iweje!!
Mahali nani kalipa?
Mkuu hivi katika muktadha huo kati ya wanaume na wanawake ni kina nani wanaotafuta ulinganifu, kama hamtaki ulinganifu basi kila mtu afanye majukumu yake maana hata wanawake wakifanya vyote nanyi hamtakuwa na thamani kwao, wewe endesha familia kiuchumi mke asimamie majukumu ya nyumbani hapo ndio mnaweza mkaleta hizo story zenu za utawala na hizo blah blah nyingine
 
Kwani huwa hatufanyi vyote tulete chakula, tulipe ada za watoto, tutume matumizi kwa wazazi wa wake zetu, tuwavishe mke na watoto. Mda huo wewe kama unafanya kazi ela yako ni ya kwako. Tuweke mtu wa kufanya kazi za nyumbani mwanaume ndio amlipe.

Nguvu inayotumika kutafuta hiki kipato kutimiza haya yote kwako ni sawa na wewe unaekaa nyumbani kudeki na kupika na pengine kuna mfanyakazi unamuelekeza tu anafanya.

Basi mi mwanaume uniwekee mfanyakazi nikae nyumbani au kama nafanya kazi ela yangu iwe yangu halafu tuone kama ntashindwa kufanya vyote

Au vyote vipi unaviongelea?
Hilo swali lako hapo mwishoni ndilo ulilotakiwa uanze nalo kabla hujaandika yote hayo, ambayo mimi hakuna mahali nimeyasema maana clearly unaonesha kabisa hukunielewa, kindly rudia tena kusoma comment yangu na ya yule jamaa niliyemquote then ndio utaelewa
 
Ndoa asili yake sio usawa.
Itakapofikia hapo kwenye usawa,
Ni pale ambapo mahali litaondolewa kuwa takwa la kufunga ndoa.
Hakuna shida siku mtakayokubali wanawake waache kutumia majina ya waume zao, na watoto nao waanze kutumia majina ya koo zote mbili wa mama na wa baba basi bila shaka utaratibu wa mahari utafutwa tu, maana hilo ndilo lengo kubwa la mahari mengine yote ya sijui kujitunza ni porojo tu
 
Mtoto wa Mbweni hivyo tushazungumza sana miaka tisa na kenda iliopita.😁

Hivi bado hadi leo hutaki kuelewa kwamba mwanaume wa Kiafrika hawezi kupiga deki na kuosha vyombo akishajipata? Na ndio maana tunaoa ili hizo shughuli mfanye wake zetu.

Huo uzungu uliojaa kichwani peleka Norway au Sweden huko ndio itafaa ila hapa Bongo utaumia sana kichwa.
Sawa sasa kama mmeshajipata kwanini msumbue wake zenu wawasaidie majukumu yenu ya kuendesha familia kiuchumi, tena kama nikishajua mwanaume mwenyewe ndio kama wewe basi hutakaa uone hata mia yangu, nitasimamia majukumu yangu yote ya nyumbani ila na wewe hakikisha hizo pesa zako hazikati yani shida yoyote ya kipesa ikitokea unaisolve mwenyewe
 
Ndoa ni muhimu lakini sio lazima.Mimi kwa uzoefu wangu wa miaka 20plus nimejifunza mengi sana.Mojawapo ni kuwa furaha yako hupati kwa mwenzako kama nilivyokuwa nafikiria ,pia tunaingia kwenye ndoa na matarajio makubwa kutoka kwa kila mmoja wetu.Sasa kikubwa kwenye ndoa ni kupata mtu unae endana nae angalao kwa asilimia 40% kitabia na pia kila mmoja aweze kuchukua mapungufu ya mwenzake kama yakwake na kuyafanyia kazi na kuyakubali na sio kumbadilisha.Mfano ,mimi nilimkuta mume wangu ni mywaji (sisemi mlevi) ila mimi sinywi so nilichofanya ni kuakikisha nampa muda wake wa kunywa kama ndio kitu kinampa furaha uwezi amini after 15yrs ameacha mwenyewe na hataki hata kusikia kwa kuwa ameona haimpi faida wala kwa umri wake sio kitu kinampa furaha nay more.Shida ni pale sasa unataka kumbadilisha fika uliolewa unajua kabisa ulimkuta anakunywa ,unafoka,unanuna why !unless aanze mkiwa ndani ya ndoa that is something else huu ni mfano mmoja tu.Kikingine lazima muweke issue za finances /kifedha wazi ,haijalishi nani anapata zaidi au hapati,try to communicate kwa habari ya budget,spending nk including investment au namna ya kuongeza kipato.Ukiona mwenzako anatumia kipato let say anamchepuko huwa nawaambia ladies be calm ,deal na furaha yako my dear you can not compete with man chini ya jua.Jipende,jidhamini ,glow my dear ,kama ulikuwa unaenda maili moja kutafuta fedha move to next miles jifanye hata ujui kinachoendelea (yaani ignore).Kingine ile mwanzo tu hamjaoana ,muwe na moment together tafuta karatasi kila mtu aandike anachokipenda kwa mwenzake ,anachokichukia na nini anataka afanyie,review after one year and hii iwe sehemu ya maisha yenu kila mwaka mshirikishe Mungu (sio mchungaji ,shehe.mashoga au nabii) wewe na Mungu wako.Trust me ,ndoa ni PARADISO nina enjoy
Bwebwe nyingi ila ndoa ikishanyoosha mikono juu imeishaa hiyoo...
 
ndo ujikute umeoa mtu mjinga kama huyu, kesho yake tu unamnyonga au unamuwasha moto kwa gunia mbili za mkaa
Jadili hoja acha hasira za kipumbavu, aliyekuambia kwamba mimi nina shida ya kuolewa na wanaume wajinga nani, kwa wanawake wa dunia ya leo mjiandae tu kisaikolojia vinginevyo mtawachoma hadi waishe mbaki wenyewe mkafie jela
 
Sasa shida za wanawake ninyi huwa mnazivumilia hebu tuongee tu ukweli ndugu yangu, ni wanaume wangapi wanaweza kuvumilia wanawake wasaliti, wavivu, wabishi na wajeuri nk, lakini wanawake wanalazimishwa kuwavumilia wanaume wenye tabia kama hizo
Wewe hufai kuwa hata kwenye ndoa kabisa
 
Uzuri kuna wanawake wanaofanya vyote bila kelele.
Acheni kuwadanganya wenzenu humu, yani ni sawa na wanawake wadanganyane kuwa kuna wanaume wanaoweza kufanya vyote, kama hao wanawake wangekuwepo basi kusingekuwa na malalamiko kutoka kwa wanaume kwenye ndoa nyingi
 
Wewe hufai kuwa hata kwenye ndoa kabisa
Kuliko kuwa kwenye ndoa ya namna hiyo kwakweli ni heri nisifae tu, acha wanawake walio desperate na wenye low self esteem waendelee kuhangaikia ndoa za aina hiyo, wanawake wanaojielewa washatoka huko
 
MKwa uzoefu wangu,mwanamke wa ndoa kufanya kazi za nyumbani ni kujipanga.My experience nilikuwa na dada wa kazi wakati watoto wangu ni wadogo .Walivyoenda form 1 boarding wote ,niliondoa dada na principle yangu kuanzia wakiwa primary wakiwa holiday dada anaenda likizo na wenyewe wanajipanga na kila siku tunapanga majukumu ya nyumbani pamoja(from Baba yao mpaka watoto) .Mimi nafanya kazi ,tena niko busy sana na ni bosi mkubwa tu kwa level ya director na bado naweza kupika naosha vyombo nafanya usafi(utakuta mwanamke analipa kwenda "gym" akiamua kazi za nyumbani akafanya ndio gym yake) .Watoto wako university na sina dada wa kazi for almost 5 yrs now nina kijana anakuja twice a week kwa ajili ya huko nje tu.Niko Likizo ndio maana nina muda hata wa kuelimisha wamama wenzangu (sisemi kila kitu kita work kwa kila mtu) ila malezi na exposure ni muhimu sana.Kwa kuwa ungekuwa ulaya una luxury ya kuwa na mdada wa kazi unajipanga my dear.
Yaani dada uko vzr sana unajielewa kwelikweli natamani ungekuwa make wangu aise, sikujua kuwa bado wanawake wenye akili mpo bado ila ni nyie wa zamani kidogo sio hivi vibinti vya 90. Hongera sana my dear
 
Back
Top Bottom