Mkuu bila shaka unafahamu kuwa wanaume hawahitaji uwape sababu ya kuchepuka, wao wanajiona kwamba wameumbwa hivyo tu kuwa hawatosheki na mwanamke mmoja hata wakioa mke mmoja ila wakichepuka lazima wasingizie kwamba sababu ni wake zao hata kama si kweli, na kwanini unaona kama mwanamke tu ndiye anayetakiwa ayachukulie na ayapotezee madhaifu ya mume wake au unashauri na mwanaume naye afanye vivyo hivyo kwa mke wake
Nimegundua ninyi ndio mnaodanganya wanaume kwamba inawezekana mwanamke kufanya majukumu yake huku akisaidia na ya mwanaume, mwisho wa siku wakiingia kwenye ndoa wakakutana na hali tofauti wanaanza kuwalaumu wanawake, wakati kumbe ni wao ndio walikuwa na expectations nyingi zisizo na uhalisia
Hivi kwa karne hii unadhani ni wanawake wangapi wanaweza kubalance hayo yote bila kutetereka mahali, ukizingatia wanaume wenyewe ndio hawa wasio na shukurani hivyo wanawake nao wanaona ya nini kujichosha, wewe mwenyewe umesema ulianza kubalance hayo yote pale watoto wako walipokuwa wakubwa na kuanza kuenda boarding unaona sasa hapo
Sasa vipi katika ile miaka yote ambayo watoto ni wadogo na wanasoma day schools unadhani mtu anajibalance vipi hapo, mimi hoja yangu ni kwamba kwanini mwanamke atwishwe majukumu mengi kuliko mwanaume, ilihali wote wana uwezo wa kusaidiana sawa kwa sawa au kuweka wasaidizi na maisha yakaenda vizuri tu