Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Baada ya kufuatilia ushauri wa Profesa Janabi kwa watanzania kuhusu aina ya maisha wanayoishi (lifestyle) na ambayo ni kisababishi kikuu cha magonjwa yanayoua lakini yanayoweza kuzuilika, ilinibidi nifanye utafiti kujiridhisha. Katika utafiti wangu nimegundua kuwa watanzania tunajiua wenyewe kwa upumbavu wetu. Acha tufe tu, hakuna namna!

Kwa mfano utakuta mtu anakula mayai 3 ya kukaanga, mishikaki 5, supu ya ng’ombe lita moja, chapati 3 na ndizi 2 za kukaanga kama kifungua kinywa. Ikifika lunch atafakamia wali-nazi na nyama choma akisukumia soda ya pepsi na maji baridi. Na supper/dinner atakula ugali, maini na filigisi akisukumia bia ya safari larger. Kwa staili ya ulaji kama huu kwanini mtu asife mapema? Unategemea nini kutoka kwa mtu mpumbavu kama huyu? Si ameamua kujiua mwenyewe kwa makusudi?

Tatizo la ulaji wa ovyo limekithiri sana hasa kwa akina mama wa mjini. Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa wanawake wanawapiku wanaume kwenye suala la kutengeneza vitambi. Hii sio kwa sababu nyingine bali ni kwa sababu ya ulaji wa ovyo.


1704279100969.png

Mwanamke mnene kama huyu hawezi kunyumbulika kitandani, hivyo kupelekea ndoa kuvunjika!

Wakati nafanya utafiti, nilimkuta mwanamke mwenye uzito wa kilo 85 na urefu wa meta 1.72 (BMI = 28.73) lakini anashindia chips-yai (zege), nyama na vinywaji vyenye sukari nyingi kama vile soda na juice. Kwa mujibu wa BMI, huyu tayari uzito wake umepindukia. Hili ni tatizo lakini mwenyewe wala hajali.

Aina ya maisha tunayoishi inachangia maradhi kwa 90% na 80% ya vifo. Na utashangaa wengine ni watu wazima na wanafahamu fika kuhusu madhara ya ulaji wao lakini hawachukui hatua kujirekebisha. Ripoti hii hapa inadhihirisha kuwa 50% ya wanawake wana uzito uliopindukia. Tatizo wanawake hawapendi kufanya mazoezi. Hata umbali mdogo tu ambao anaweza kutembea kwa miguu utasikia anasema: “namuita bodaboda wangu aje kunibeba”. Matokeo yake ni kuendelea kurundika mafuta mwilini hadi kufikia wakati anashindwa kugawa tendo la ndoa kwa mumewe kwani hawezi kukunjika tena kwa sababu ya unene uliopitiliza. Hii haifai hata kidogo.

USHAURI WANGU
Kwa kuwa tatizo la ulaji wa ovyo limekuwa sugu, naishauri serikali ianzishe tozo kwa watu wanene na tozo hii ilipwe kulingana na uzito wa mtu. Hii itasaidia kuinua uchumi wa nchi kwani hizi fedha ambazo watu wanazitumia kulisha miili yao na hatimaye kuiletea shida serikali kwenye suala la matibabu zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya serikali.

Sasa ikiwa mtu amebarikiwa kuwa na uchumi mzuri halafu uchumi huo anautumia kujiletea magonjwa kuna tatizo gani serikali ikampunguzia uchumi huo na kuutumia kwa maslahi ya taifa?

Tukumbuke kuwa serikali ndiyo inayolaumiwa kila siku kwa kutoboresha huduma za afya, zikiwemo afya za hawa wazembe wanaojiletea magonjwa wenyewe kwa makusudi. Serikali isipochukua hatua za makusudi kukabili tatizo la ulaji wa ovyo kwa wananchi wake, mwisho wa siku ndiyo itakayobebeshwa lawama. Wakati wa kuchukua maamuzi magumu ni sasa.

Nawasilisha.

Pia soma:
1. Kwanini baadhi ya watu hawapungui uzito hata kwa mazoezi na kubadili mlo? - BBC News Swahili
2. Mtalaamu aeleza namna ya kumtambua mwanaume, mwanamke mwenye kitambi

 
Naamini 95% hawatakuelewa kwa ujinga wao na watajifanya wanaelewa sana na wataleta hoja za kijinga mradi wakupinge na kujifanya wao wanajuwa kumbe hawajuwi.

Niliwahi kuandika hivi kuhusu Watanzania:

Huku mitaani mtu akinenepa anasifiwa kwamba Amependeza !
 
Naamini 95% hawatakuelewa kwa ujinga wao na watajifanya wanaelewa sana na wataleta hoja za kijinga mradi wakupinge na kujifanya wao wanajuwa kumbe hawajuwi.

Niliwahi kuandika hivi kuhusu Watanzania:

Bibi mbona kwenye imagination zangu wewe ni kibonge unamashavu dodo mguu wa bia imekuaje Tena???🤔

Usinambie na wewe ni modo kimbaumbau 😂
 
Naamini 95% hawatakuelewa kwa ujinga wao na watajifanya wanaelewa sana na wataleta hoja za kijinga mradi wakupinge na kujifanya wao wanajuwa kumbe hawajuwi.

Niliwahi kuandika hivi kuhusu Watanzania:

Wewe kisa humu katajwa muhamedi lazima uje mbio kuunga mkono hoja...una shida ya udini sana
 
Kumbe Biblia ilivyosema kwamba sisi ni writhing wa UZIMA WA MILELE ilikuwa sahihi kabisa, ila shetani anatufanya tuwe walafi ili tufe Mungu aonekane mwongo!!!
Kweli kabisa mkuu. Wakati mwingine hawa wapendakula wana mapepo ya ulafi. Wanapaswa waende kwa mtume Mwamposa awaombee mapepo ya ulafi yawatoke.
 
Back
Top Bottom