Utafiti: Ripoti yaonyesha vijana wengi nchini hawana heshima

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Ripoti ya utafiti wa stadi za maisha na maadili kwa vijana imeonyesha asilimia kubwa ya vijana nchini hawana heshima, hawajitambui na hawana ushirikiano kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

Utafiti uliozinduliwa Leo Januari 26, 2023 na Taasisi ya Regional Education Learning Initiative (Reli) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uwezo Tanzania umeonyesha kundi kubwa la vijana nchini hawana Maadili na stadi za maisha.

Ripoti hiyo ya ' Assesment of Life Skills and Values in East Africa' iliyofanyika Julai, 2022 imehusisha vijana kuanzia umri wa miaka 13 hadi 17 katika wilaya 34, kaya 11,802 zikihusika na vijana 14,645 walihusishwa kutoka Tanzania Bara.

Utafiti huo umeonyesha kijana mmoja pekee kati ya 10 ana heshima na kujali maadili katika jamii, ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ya vijana wote waliohusika katika utafiti huo

Vilevile, ripoti imeonyesha kuwepo kwa uelewa mdogo wa vijana kujitambua na kutatua tatizo ambapo asilimia 16.8 pekee wana uwezo huo.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo na mdau wa Elimu, Profesa Kitila Mkumbo amesema uelewa mdogo wa kutatua matatizo na stadi za maisha unasababishwa na hali ya ubora wa elimu.

"Vijana waliohusika kwenye uchunguzi huu wengi wapo shuleni, napata mshituko kuona Wanafunzi Wana uelewa mdogo wa kutatua matatizo na nalihusisha hili na ubora wa elimu yetu," amesema.

"Tukiwekeza hapa kwenye elimu Bora huko mbele kazi itakuwa rahisi kwenye stadi za maisha Kama kujitambua, kutatua matatizo, ushirikiano na heshima," ameongeza.

Chanzo: Mwananchi
 
Hili ni janga kubwa sana, vijana ni wajuaji na wakishamaliza elimu zao za awali (bachelor degree) hawakamatiki. Hawana uvumilivu, wanataka ndani ya wiki mbili awe tayari ana gari zuri, nyumba ya kifahari na awe na pisi kali kila kona ya jiji.

Lazima jitihada za makusudi zifanyike kuukuza uzalendo, kuongeza uaminifu na soft skills ambazo zitaweza kufanya uwekezaji kutoka nje kuwa himilivu na endelevu
 
Ripoti hiyo ya ' Assesment of Life Skills and Values in East Africa' iliyofanyika Julai, 2022 imehusisha vijana kuanzia umri wa miaka 13 hadi 17 katika wilaya 34, kaya 11,802 zikihusika na vijana 14,645 walihusishwa kutoka Tanzania Bara.
Kwa Tanzania, mtu mwenye umri kati ya miaka 13 na 14 sio kijana! Kijana ni kati ya miaka 15 na 35.
 
Maadili ya kuvaa nguo zinazovuka magoti, kusalimia shikamoo na kutotoa maoni tofauti na mtazamo wa wakubwa?

Natamani kujua vigezo gani hasa vilitumika kupima maadili ya hao watoto walioitwa vijana humu!
 
Zamani nilipenda kukaa na vijana ili niwe mzee mjanja kama vjana ila hamna niliombulia zaidi ya kuwa na fikira za kijinga kama wao.
 
Vijana tumekua tukililia tuweze kupewa nafasi mbalimbali za uongozi lakini ndio tumekua mwiba miongoni mwetu. Tunafanyiana fitna, Chuki, Roho mbaya.

Unakuta kijana yupo ofisini anakuhudumia uku muda wote anachati na simu tu mpaka unapata hasira. Mara nyingi sio watu wa kutoa msaada pale ambapo inahitajika busara.

Inafika mahali unatamani ni bora maofisini wangebaki wazee tu maana ndio wamejawa busara kwa madhira tunayokutana nayo huko kwenye huduma za kijamii zinazosimamiwa na vijana hasa kada za Afya kwakweli tuseme tu vijana hatuna uwezo wa kujisimamia wenyewe tunahitaji busara za wazee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ripoti ya utafiti wa stadi za maisha na maadili kwa vijana imeonyesha asilimia kubwa ya vijana nchini hawana heshima, hawajitambui na hawana ushirikiano kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

Utafiti uliozinduliwa Leo Januari 26, 2023 na Taasisi ya Regional Education Learning Initiative (Reli) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uwezo Tanzania umeonyesha kundi kubwa la vijana nchini hawana Maadili na stadi za maisha.

Ripoti hiyo ya ' Assesment of Life Skills and Values in East Africa' iliyofanyika Julai, 2022 imehusisha vijana kuanzia umri wa miaka 13 hadi 17 katika wilaya 34, kaya 11,802 zikihusika na vijana 14,645 walihusishwa kutoka Tanzania Bara.

Utafiti huo umeonyesha kijana mmoja pekee kati ya 10 ana heshima na kujali maadili katika jamii, ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ya vijana wote waliohusika katika utafiti huo

Vilevile, ripoti imeonyesha kuwepo kwa uelewa mdogo wa vijana kujitambua na kutatua tatizo ambapo asilimia 16.8 pekee wana uwezo huo.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo na mdau wa Elimu, Profesa Kitila Mkumbo amesema uelewa mdogo wa kutatua matatizo na stadi za maisha unasababishwa na hali ya ubora wa elimu.

"Vijana waliohusika kwenye uchunguzi huu wengi wapo shuleni, napata mshituko kuona Wanafunzi Wana uelewa mdogo wa kutatua matatizo na nalihusisha hili na ubora wa elimu yetu," amesema.

"Tukiwekeza hapa kwenye elimu Bora huko mbele kazi itakuwa rahisi kwenye stadi za maisha Kama kujitambua, kutatua matatizo, ushirikiano na heshima," ameongeza.

Chanzo: Mwananchi
Bakora za papo kwa papo ziruhusiwe nchi nzima kweli hali sio nzuri.
 
Back
Top Bottom