Utafiti; Wakenya wengi wamekata tamaa ya maisha

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Wakenya wengi wamekata tamaa ya maisha kutokatana na gharama za maisha kuwa juu nchini mwao, rushwa na ukosefu wa ajira. Matokeo ya utafiti huu yanaendana na utafiti mwingine ulioonyesha kwamba, wakenya wengi hawapendi kuishi nchini mwao na wanapenda kutoroka na kuishi nchi za nje.

Hali hii ya wakenya kukata tamaa ya maisha na kuwaza kutoroka, imesababisha mkenya mmoja Jana kujificha katika eneo la gurudumu la ndege ya KQ ili aweze kutoroka Kenya, bahati mbaya amefariki kabla ya kutimiza lengo lake.
 
Ngoja waje, waseme ya kuwa wao ndiyo happiest nation in the bloc if not on earth.
Mmoja alitaka kukimbilia ulaya kama wanavyofanya inzi au mbu.
 
Ngoja waje, waseme ya kuwa wao ndiyo happiest nation in the bloc if not on earth.
Mmoja alitaka kukimbilia ulaya kama wanavyofanya inzi au mbu.
Aisee, ikifikia mtu anaona bora kufa kuliko kuishi nchini mwake, basi jua hali imefikia kiasi cha kutovumilika. Hali hii ilijitokeza sana hapa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 80s, vijana wengi walikua wanajificha katika meli ili waende Ulaya, wengi walitupwa na kufa baharini.
 

Wakenya wengi wanavyoishi wanashindwa kutofautisha uhai na kifo. Wamekata tamaa ya kuishi.
 
Saa zingine huwa nafurahi nikiona mandugu zangu watz mitandaoni mkiongea vibaya kutuhusu sisi wakenya. Hizi nguvu mnazoziweka kutuharibia jina haitafanya Tanzania ingare wala ifanikiwe na ninawaomba mtoke online mwende mkajenge nchi yenu vile.
 
Ni ukweli gharama ya maisha imepanda sana Kenya lakini mnatudanganya mkisema hakuna watz ambao wanataka kuenda ngambo wajaribu kupata maisha bora. Stop being negative majamaa si ungwana.
 
Ni ukweli gharama ya maisha imepanda sana Kenya lakini mnatudanganya mkisema hakuna watz ambao wanataka kuenda ngambo wajaribu kupata maisha bora. Stop being negative majamaa si ungwana.
Ni vizuri ukaelewa "Mukhtadha", yaani " context" ya mazungumzo. Hakuna nchi hata moja duniani ambako raia wake hawapendi kutoka nje ya nchi yao, ila kinachotofautiana ni kwa kiwango gani na sababu zipi.

Wajapan wengi wanapenda kuishi Marekani, sawa na wakenya au watanzania wanavyopenda kuishi Marekani, lakini sababu kubwa ya wajapani kupenda kwenda USA ni "Social", wakati sisi huku ni " Economical".

Kwa sasa hivi uchumi wa Kenya umeyumba sana ukilinganisha na Tanzania, kwahiyo ni wazi kwamba wakenya wengi wanapenda kwenda USA kuliko watanzania.
 
Nimekuskiza na hatakama sijakubaliana na
mengi uliyosema, umesema vitu vya maana.
 
Nimekuskiza na hatakama sijakubaliana na
mengi uliyosema, umesema vitu vya maana.
Wewe inaonekana ni mgeni, lakini inaonekana bado hujachafuliwa na malumbano ya hapa JF, bado unatumia busara kujadili hoja kuliko sisi wenyeji ambao wengi tunatumia ushabiki zaidi.

Ningependa kukuuliza maswali machache unijibu.
1)Hivi kwanini wakenya mumeambizana na kuamini kwamba kitendo cha Tanzania kuchoma vifaranga pale Namanga ni kosa, na lengo ni kuhujumu Kenya?
 
Saa zingine huwa nafurahi nikiona mandugu zangu watz mitandaoni mkiongea vibaya kutuhusu sisi wakenya. Hizi nguvu mnazoziweka kutuharibia jina haitafanya Tanzania ingare wala ifanikiwe na ninawaomba mtoke online mwende mkajenge nchi yenu vile.

kwani nchi yenu imejengeka?
na sio ingare bali ni ing'are
 
Hilo ni swali nzuri.

Sisi kama wakenya hatukuelewa huo msimamo wa serikali yenu kuchoma vifaranga vyetu kwa sababu ya “virusi” nyinyi mngeturudishia vifaranga sisi tuendelee na shughuli zetu sasa kutuchomea ilisababisha wafanyibiashara waone hii serikali ya JPM iko na kasoro na hiyo kasoro ni hamaapendi wakenya na hamtaki afrika mashariki iendelee kusonga mbele. na wakumbuka ile time mlichukua ngombe wetu mkawashika wakenya wamasai na mkawatia rumande? Wakenya hatukuridhishwa na jambo hilo na namwelewa JPM ywafaa kulimda maslahi ya watu wake lakini zile vitu anazozifanya are in bade faith.

Na wacha nikuulize swali, katika afrika mashariki mbona watanzania hamtaki sisi sote tufanye trade, biashara na kazi pamoja? Kila masaa unaskia waganda na wakenya mara warwanda na waburundi wamefurushwa kwa sababu ya reasons zisizojulikana. Na je kama marehemu Nyerere angekuwa hai wadhani angeridhishwa na vile mnavyowafanyia wenzenu na vile tanzania haijihusishi sana na maswala ya EAC kama zamani?
 
Huo mtazamo ulionao dhidi ya Tanzania, ndio sababu kubwa inayotufanya tukorofishane na Kenya, tatizo ninyi wakenya muda mwingi hamfikirii sana, huwa mnatumia mihemuko badala ya kutumia busara.

Kwa mfano wewe umeenda China, ukanunua "Plastic bags" na ukazileta hapo Kenya, ulipofika JKIA hiyo mifuko ya plastic ikakamatwa na kuchomwa moto;
1) Je, hiyo mifuko ya plastic ni Mali yako au ni Mali ya nchi ya China?
2)He, China inapaswa kuilaumu Kenya kwa kuchuma hiyo mifuko ya plastic?
 
 
Hivi unajua tofauti kati ya utafiti na maoni ya mtu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…