Hilo ni swali nzuri.
Sisi kama wakenya hatukuelewa huo msimamo wa serikali yenu kuchoma vifaranga vyetu kwa sababu ya “virusi” nyinyi mngeturudishia vifaranga sisi tuendelee na shughuli zetu sasa kutuchomea ilisababisha wafanyibiashara waone hii serikali ya JPM iko na kasoro na hiyo kasoro ni hamaapendi wakenya na hamtaki afrika mashariki iendelee kusonga mbele. na wakumbuka ile time mlichukua ngombe wetu mkawashika wakenya wamasai na mkawatia rumande? Wakenya hatukuridhishwa na jambo hilo na namwelewa JPM ywafaa kulimda maslahi ya watu wake lakini zile vitu anazozifanya are in bade faith.
Na wacha nikuulize swali, katika afrika mashariki mbona watanzania hamtaki sisi sote tufanye trade, biashara na kazi pamoja? Kila masaa unaskia waganda na wakenya mara warwanda na waburundi wamefurushwa kwa sababu ya reasons zisizojulikana. Na je kama marehemu Nyerere angekuwa hai wadhani angeridhishwa na vile mnavyowafanyia wenzenu na vile tanzania haijihusishi sana na maswala ya EAC kama zamani?