Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 5,319
- 10,416
Thank you so much kaka..incredibly helpful.Hii route yako bonge moja la adventure , Dar utapata chai nangurukuru, then utazuga mnazi mmoja pale kiaina unywe maji kidogo, hapo utajiandaa kuingia mtwara, utasimama na kushangaa kidogo Dangote cement, ukifika mtwara utaanzia magomeni, utaenda stand ya zamani pale ule supu ya pweza, ukitembea hapo uiwaze ndanda, then masasi, ukitoka masasi utaenda kusimama mangaka, kidogo utagonga pori hapo maeneo ya majimaji hadi kiuma hadi kilimasera pale kuna down moja matata kote huko utapita then ukifuka tunduru utanunua korosho bei nafuu kidogo ili unywe na maji hapo utapata story kiasi za mpunga, mbao pori, kitu na mziki hapo unaisaka namtumbo, songea mjini utalala iwe matarawe au bombambili, pale utapiga story za nyasa, mbambabey, utapata samaki aina ya mberere na mbufu na ugali wa muhogo sijui utalala appleline au utakua na tent najua utatamani ufike ziwa nyasa au manda huko lakini utadamka kwenda mliyayiyo uiage songea ulenge madaraja hadi lilondo upate kuku wa kukaanga na ndizi mbivu hapo utakua ushapita madaba, mkongotema umebeba tangawizi kidogo, then utapata kuiona kifanya, hapo unaitafuta njombe milima panda shuka, njombe baridi kali utapata chai ya rangi na majani ya asili, ukitoka hapo uiangalie makambako pale utapita Kwa mama anita upate dona na mbogamboga kama tisa hapo unapishana na akina mwendamseke, another G , utaacha kwenda iringa wewe unaanzia mbeya road sasa hapo uitafute halali, igawa, chimara, igurusi, itewe mara kidogo mlima nyoka, unapita dampo uyole hiyo hapo utaamua ukale supu Kwa wasomali au utajua ufanye nini halafu ukifika uyole useme tuanzie uyole kwenda mitaa ya nane nane, ilomba, mwanjelwa, simike nzovwe, unatokomea iwambi kuiona mbalizi hapo ukivuka mbali kama unaumwa utapita pale ifisi Kwa dokta rena au upate tiba kidogo halafu utajua uelekee senjele, upige mpaka mlowo, vwawa, mpemba, tunduma pale sasa utulie kidogo ndio uanze route yako kufika laela, sumbawanga, piga barabara hadi namanyere, hapo kidogo lyazumbi hiyo hapo kula supu na mbuzi choma then ianze hifadhi ya katavi utaona twiga, viboko pale mtoni, tembo kiasi hadi unaibukia stalike, hapo sasa utakua unaitafuta mpanda, ukifika mpanda wape salamu zao halafu kigoma nitakujuza up nafikaje,
Yaani mkuu hii post yako nai print kabisa. Duh umenifanya nizidi kuharakisha mipango yangu. Kiukweli ni safari nimeitamani siku nyingi sana. Ni aibu tuna graduate ujana na hatujawahi kufanya utalii proper wa nchi yetu. Nimepania sana. Sijawahi kwenda mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini.
Angalizo, Nina Usafiri wangu na nimepanga 7 days toka Dar mpaka Kigoma. Itatosha? Lakini pia ukiwa unapata mda uwe unaweka dondoo za hotel na sehemu nzuri nzuri za kutembelea. Mfano natamani nikifika songea nikatembee Peramiho…lots of plans in my head.
Kiongozi Asante sanaaaaaa kwa hii post. Siku mambo yakiwa tayari.. ntakuja inbox.
RRONDO uzi wako wa safari ulinihamasisha sana. Kindly share what you have on this….