Utafiti: Wanaosafiri wana raha sana kuliko shopping

Thank you so much kaka..incredibly helpful.

Yaani mkuu hii post yako nai print kabisa. Duh umenifanya nizidi kuharakisha mipango yangu. Kiukweli ni safari nimeitamani siku nyingi sana. Ni aibu tuna graduate ujana na hatujawahi kufanya utalii proper wa nchi yetu. Nimepania sana. Sijawahi kwenda mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini.

Angalizo, Nina Usafiri wangu na nimepanga 7 days toka Dar mpaka Kigoma. Itatosha? Lakini pia ukiwa unapata mda uwe unaweka dondoo za hotel na sehemu nzuri nzuri za kutembelea. Mfano natamani nikifika songea nikatembee Peramiho…lots of plans in my head.

Kiongozi Asante sanaaaaaa kwa hii post. Siku mambo yakiwa tayari.. ntakuja inbox.

RRONDO uzi wako wa safari ulinihamasisha sana. Kindly share what you have on this….
 
Siku saba zinatosha sana , na ungeweza beba na portable tent kabisa, spare tyre mbili, jeki, triangle, spana yetu ile multifunctional, service ufanye vyema, halafu uwe unatembea walau ikifika saa moja unatafuta sehemu unalala maana usiku hitifaidi maeneo mengi, reflectors, panga kali au kisu cha wamasai, maji ya kunywa kiasi, na kadhalika,
 
Kutembea kuzuri sana hata watoto nimewarithisha hiyo kitu.
Kenya shule nyingi Zina tour studies mingi sana wamefika hata ambapo sijafika.
Alhamdulilah East Africa Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda na Congo nishamaliza next trip ni Ethiopia na Somalia
Mtembea bure sio sawa na mkaa bure!
 
Kusafiri ni zaidi ya shule. Hongera sana chief. Kuna moja naipigia mahesabu. Dar-Lindi-Mtwara-Masasi-Tunduru-songea-Sumbawanga-Katavi-Kigoma....

If you know anything here..share your experience. Tuendelee kujifunza.
Mimi mwisho wangu ni MASASI hii barabara naijua ndani nje
 
Wale madereva wa lori ni watu wenye furaha sana , japo kazi yao ina risk kubwa hasa hawa wanasafiri nchi mbalimbali .

Vijana wengi wanajiona maisha wameyapatia wakifanya kazi za kusafiri ..Napenda sana stori zao.
 
Alafu anakuja MTU mwingine anabisha kuwa hizi ruti haujawahi kufanya basi atakuwa chizi maana Kwa jinsi ulivyonipa data kutoka DAR Hadi MASASI na Mangaka hakika umetisha sanaaa mkuu...

Safi sana aiseeee
 
Alafu anakuja MTU mwingine anabisha kuwa hizi ruti haujawahi kufanya basi atakuwa chizi maana Kwa jinsi ulivyonipa data kutoka DAR Hadi MASASI na Mangaka hakika umetisha sanaaa mkuu...

Safi sana aiseeee
Kusafiri ni gharama kubwa na muda akija mtu anakueleza weka ushahidi, tayari unajua kiwango chake cha uelewa na uchumi unaachana nae, unamjibu ameshinda ili afurahie,
 
Binafsi starehe yangu kubwa ni kusafiri ,nimezunguka sehemu kubwa nchi hii bila kua na ndugu wala shuguli maalumu ili nitulize moyo wangu na kila mwaka husafiri mara 2 kwa ajili ya kujiweka poa.
Safi Mkuu. Ukiweza pia safiri na familia (mke na watoto)
 
Safi Mkuu. Ukiweza pia safiri na familia (mke na watoto)
Mke na watoto watakula sana life kwenye kusafiri hasa mke wangu labda awe mduwanzi. Kusafiri kunaleta sana muunganiko na kuongeza upendo baina ya mtu na mtu nashauri watu hata wakiwa na ugomvi wa kimapenzi wao wapange tu safari kila kitu kinasettle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…