Utafiti: Watanzania wana hofu ya kukosa huduma za kijamii wakimchagua kiongozi wa upinzani

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Utafiti wa Taasisi ya Utafiti Repoa unaonesha Watanzania wana hofu ya kukosa huduma muhimu za za kijamii endapo watamchagua kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Utafiti huo wa Repoa walioufanya kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung ya nchini Ujerumani, mwaka 2021, ulihusisha watu 2,014 katika Wilaya za Ilala, Temeke, Ubungo, Kigamboni na Kinondoni mkoani wa Dar es Salaam, Karatu mkoani Arusha na Makete mkoani Njombe.

Akiwasilisha utafiti huo ulioangazia kwenye eneo la ukuaji wa miji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za kisiasa na huduma za jamii, Mtafiti Mwandamizi wa Repoa, Dk Hubert Shija alisema kuna utaratibu wa kidemokrasia wa kuwa na vyama vingi unaosababisha wananchi kulalia chama kimoja.

Pia utaratibu wa upigaji kura au kuchagua viongozi wa kisiasa katika Serikali za mitaa, Serikali kuu, Rais, wabunge na madiwani, unakuta tuliowahoji wanaona kwamba ukipigia chama tawala ndiyo utapata huduma zaidi, ukipigia chama cha upinzani unaweza usipate huduma…

Akizungumzia utafiti huo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara) Benson Kigaila, alisema jambo hilo limesababishwa na viongozi wa chama cha Mapinduzi ambao kila kukicha wamekuwa wakiwaambia wananchi wakiwachagua wapizani hawatapata maendeleo.

"Mfano wa wazi ni hayati John Magufuli akiwa kwenye kampeni zake mwaka 2020 alikuwa akisema ukiniletea viongozi wa upinzani sitawaletea maji hapa, kwahiyo ni propaganda ya kuwatisha wananchi wasiwachague upinzani” alisema

Utafiti wa REPOA unaonesha kuwa:
  • Watanzania wawili kati ya watatu wanatilia shaka demokrasia nchini
  • Watanzania 9 kati ya 10 hawapo tayari kuandamana wasiporidhishwa na mwenendo wa serikali
  • Watanzania 3 kati ya 4 hawapo tayari kuandamana kudai huduma za kijamii, ongezeko la kodi
  • 40% ya wananchi mijini hawashiriki kwenye michakato wa kufanya maamuzi ya kisiasa
  • 17% ya wananchi vijijini hawashiriki kwenye michakato ya kufanya maamuzi ya kisiasa
 
Ukweli ni kuwa nchi yetu ni masikini, hivyo ni ngumu kupeleka maendeleo kila mahali kulingana na mahitaji, hivyo viongozi wajinga hawasemi kuwa serikali haina uwezo wa kupeleka maendeleo kila mahali kwa wakati, bali huwahadaa kwa kuwaambia hawatawapelekea maendeleo. Na kweli utakuta kutokana na udogo huo wa bajeti wanafanya upendeleo kwa maeneo waliyochaichagua CCM.
 
Mtoa Mada, jiulize kwanza" ni wananchi wangapi wanaojua haki na wajibu wao kwa serikali, je nafasi hiyo ya kulalamikia serikali wanayo? na kwa kiwango gani! Nje ya hapo ni mchezo wa kuingiza kama mchezo mwingine wowote ule. (Rejea Bawata VS Serikali) miaka hiyo nyuma.
 
Utafiti wa Taasisi ya Utafiti Repoa unaonesha Watanzania wana hofu ya kukosa huduma muhimu za za kijamii endapo watamchagua kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Utafiti huo wa Repoa walioufanya kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung ya nchini Ujerumani, mwaka 2021, ulihusisha watu 2,014 katika Wilaya za Ilala, Temeke, Ubungo, Kigamboni na Kinondoni mkoani wa Dar es Salaam, Karatu mkoani Arusha na Makete mkoani Njombe.

Akiwasilisha utafiti huo ulioangazia kwenye eneo la ukuaji wa miji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za kisiasa na huduma za jamii, Mtafiti Mwandamizi wa Repoa, Dk Hubert Shija alisema kuna utaratibu wa kidemokrasia wa kuwa na vyama vingi unaosababisha wananchi kulalia chama kimoja.

Pia utaratibu wa upigaji kura au kuchagua viongozi wa kisiasa katika Serikali za mitaa, Serikali kuu, Rais, wabunge na madiwani, unakuta tuliowahoji wanaona kwamba ukipigia chama tawala ndiyo utapata huduma zaidi, ukipigia chama cha upinzani unaweza usipate huduma…

Akizungumzia utafiti huo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara) Benson Kigaila, alisema jambo hilo limesababishwa na viongozi wa chama cha Mapinduzi ambao kila kukicha wamekuwa wakiwaambia wananchi wakiwachagua wapizani hawatapata maendeleo.

"Mfano wa wazi ni hayati John Magufuli akiwa kwenye kampeni zake mwaka 2020 alikuwa akisema ukiniletea viongozi wa upinzani sitawaletea maji hapa, kwahiyo ni propaganda ya kuwatisha wananchi wasiwachague upinzani” alisema

Utafiti wa REPOA unaonesha kuwa:
  • Watanzania wawili kati ya watatu wanatilia shaka demokrasia nchini
  • Watanzania 9 kati ya 10 hawapo tayari kuandamana wasiporidhishwa na mwenendo wa serikali
  • Watanzania 3 kati ya 4 hawapo tayari kuandamana kudai huduma za kijamii, ongezeko la kodi
  • 40% ya wananchi mijini hawashiriki kwenye michakato wa kufanya maamuzi ya kisiasa
  • 17% ya wananchi vijijini hawashiriki kwenye michakato ya kufanya maamuzi ya kisiasa
wamekata tamaa hata wakishiriki hawaoni cha maana kinachofanyika lkn kuna wakati watazinduka watakapoona mambo yanazidi kuwa magumu kwao.
 
Ukweli ni kuwa nchi yetu ni masikini, hivyo ni ngumu kupeleka maendeleo kila mahali kulingana na mahitaji, hivyo viongozi wajinga hawasemi kuwa serikali haina uwezo wa kupeleka maendeleo kila mahali kwa wakati, bali huwahadaa kwa kuwaambia hawatawapelekea maendeleo. Na kweli utakuta kutokana na udogo huo wa bajeti wanafanya upendeleo kwa maeneo waliyochaichagua CCM.
Nadhani ndiyo maana kuna wanasiasa wana guts kusema chama chao haking'oki madarakani. Wanacheza na "fursa".
 
Back
Top Bottom