Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Unaongelea shirika moja la ndege inaonekana umekurupuka kuandika hivi unajua kabla ya kuvunjika jumuhiya ya kwanza tulikuwa na mashirika kama hayo likiwemo la posta na mengineyo.
Unajua nini kilitokea baada ya jumuhiya kuvunjika kuna watanzania wenye uzalendo walitorosha ndege zilizokuja kuanzisha ATC. Sasa hivi tumechukua tahadhari zote kwani tunajuana vizuri wengine ardhi wamegawia wazungu halafu wanataka sisi tuwape ardhi.
 
Hatuwezi kupeleka majeshi yetu Somalia kwa interest za mmarekani, tutaenda tu ikiwa kuna sababu za msingi za kwenda
 
Wakenya mrudishe kwanza Ndege na mali za iliyokuwa jumuiya ya Africa Mashariki ndio tufikirie kurudi mezani...

Kinyume na hapo msahau.
Mbona sisi tulibaki na majengo ya Arusha na tumeyatumia miaka na miaka.
 
Ndio maana nilisema uzi kama huu unapaswa kujadiliwa na wenye uwezo kushirikisha ubongo, wengine mtaishia kukojoa humu bila umuhimu wowote.
Hii ni mijadala inayoangalia zaidi ya miaka 100 ijayo.
Na wewe unajihesabu kuwa kwenye kundi la hao "wenye uwezo kushirikisha ubongo"? Kama hivyo ndivyo, sina sababu ya kuwa kwenye kundi hilo.

Miaka hiyo mia, inawezekana sana Somalia akawa kwenye umoja wa EAC kuliko hiyo nchi unayoifikiria kuwa wao ni bora zaidi ya wengine waliopo Kigoma.
Nadhani damu yenu inasumu ndani yake, hii si bure.
 

Negativity zilezile yaani ukiwa diaspora ni kukimbia nchi😂 wakati wengine wanaona ni kutafuta maslahi. Ni mtazamo wako mtatuita kila kitu fisi, kondoo, beberu nk lakini ukisoma ujumbe ni kwamba tunaongelea maendeleo ni mambo binafsi. Sijui ufisi una uhusiano gani na manunuzi, kampuni za ndege na kuweka viwango juu vya elimu!
 
Maendeleo yanapatikana kwa njia mbalimbali. Usilazimishe utakavyo wewe.

Na hata yangetegemea hiyo njia ya kuunda vikundi, kwani ni lazima kuwa na kikundi hicho unachokipigia upatu hapa? Mbona yapo makundi mengi tu ya kujiunga nayo kama ni lazima kuunda kundi!
 

..unayosema ni kweli.

..lakini mbona tulikuwa na East African Community ikavunjika, na sasa hivi tumeunda njombo hichohicho tena?

..tunachotakiwa ni kujifunza hapo mwanzo tulikosea wapi, na tuazimie kwamba safari hii hatutarudia makosa ya miaka ya 70.

..Wana Afrika Mashariki tunapokutana nje ya nchi zetu[ulaya...] tunaishi kidugu bila matatizo. Lakini tunaporudi nyumbani kuna a lot of negativity baina ya raia wa nchi zetu. Hili ni tatizo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa undani na kushughulikiwa.
 

Ingependeza kama ungekuwa unatoa mawazo yako badala ya kupinga tu na kuita watu majina bila sababu ya msingi.

Mawazo ya kuwa na viwango sawa vya elimu vitasaidia kila nchi hakutakuwa na visingizio mfano kwa wale wanaosema elimu yetu iko chini. Kuhusu kuunganisha mashirika ya ndege na kuwa na shirika moja kubwa ni logic rahisi tu kwenye biashara ya ndege big is better. Kuhusu kununua madawa pamoja ni kupunguza bei ya dawa na gharama kwa wana EA sasa sijui hapo lakupjnga lipi!. Pesa mmoja sijasema lakini ni vitu hivyo. Lakini sitaendelea kubiashana bila sababu kama una mawazo tofauti yatoe badala ya kupinga kwasababu tu ni Kamundu
 

..kuna umuhimu pia wa sisi waTz kuanza kupendana na kuthaminiana.

..kuna chuki baina ya waTz ambayo ikiachwa iendelee itatuletea matatizo.

..kuna baadhi ya waTz wameanza kuona ni jambo la kawaida na halali kueneza chuki dhidi ya jamii fulani hapa Tz.

..utamaduni huo haukuanza leo, ulianza tangu awamu ya kwanza lakini nadhani sasa unaelekea kuota mizizi.

..nakubaliana na mawazo yako kwamba tuwe na mfumo mmoja wa ELIMU na pia uwe ni mfumo wenye USAWA kwa maana ya VIWANGO.

..zaidi ya elimu tuanze sasa kupiga vita chuki zisizo na msingi baina yetu Watanzania.
 

Yaani mtu ukiwa na mawazo tofauti tayari wanafikiri wewe ni Mkenya! na wenyewe tu ndiyo wazalendo wanaoipenda nchi kuliko wengine hizi ni akili za kutokujiamini!
 
Wakenya mrudishe kwanza Ndege na mali za iliyokuwa jumuiya ya Africa Mashariki ndio tufikirie kurudi mezani...

Kinyume na hapo msahau.
..hakuna nchi inayomdai mwenzake.

..masuala ya mgawanyo wa mali na madeni ya EAC iliyovunjika yalishamalizwa na Dr.Victor Umbricht.

..serikali za Tz, Kny, na Ug, kwa pamoja, zilimteua Dr.Umbricht, raia wa Uswizi, kuwa msuluhishi kuhusu suala la mali na madeni ya jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika.

..sanasana serikali ya Tz ndio imedhulumu fedha za pensheni za waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

cc MK254
 
Wewe ni mgumu sana kuelewa.
Huo umoja unaoutafuta hauwezekani na wala hauna tija kwa hao washirika unaowataka wewe. Tafuta washirika wengine, kwani ni lazima wawe hao?

Sina haja ya kutoa "mawazo"; (bila shaka una maana ya mapendekezo yangu, kwani si tayari natoa "mawazo" hapa?) kwa ushirika nisioutaka uwepo.
Hayo mambo ya ndege, madawa sio mambo mageni. Kwani hujawahi kusikia SADC na mpango wao wa ununuzi wa madawa? Usichotaka kuelewa kwa maksudi ni kwamba huwezi kulazimisha watu wasioweza/taka kushirikiana washirikine kwa lazima kwa vile wewe unataka iwe hivyo.
 
Yaani mtu ukiwa na mawazo tofauti tayari wanafikiri wewe ni Mkenya! na wenyewe tu ndiyo wazalendo wanaoipenda nchi kuliko wengine hizi ni akili za kutokujiamini!
Hujui maana ya maneno unapoyatumia, kama hilo la "Kutojiamini" mnapenda sana kulitumia upande huo.

Ndio maana nasema inawezekana kuna kitu ndani ya damu yenu kinachosababisha msiweze kujihisi kuwa na udhaifu/kasoro ya kudhani ni nyinyi pekee mmeumbwa kuwa na uwezo wa kujiamini.

Unaeleweka 'asili yako' ni wapi, hili linajulikana vyema.

Kwa bahati mbaya sana msimamo wako pamoja na kujitambulisha na kujivika 'uzalendo' wa nchi uliyoamua kuihamia, fikra zako zilibaki huko huko ulikoanzia na tabia zile zile za huko ulikotoka.
Huu uzalendo unaouhimiza hapa kila mara ni koti tu unalolivaa inapotakiwa kujikinga nalo.
 
Usidhani hii kitu serikali yetu haijui

Katika hizo nchi zote Ni Tz tu ndio inasita sita

Wengine wako tayari hata kesho unajua kwanini?

ARDHI

hao wengine Wana ufinyu wa ardhi na population Yao inaongezeaka day to day

Population na ardhi lazima viende kwa uwiano

Sisi huku tuna bonge la ardhi liko liko tu wanalimezea mate

Ukileta hayo Mambo ya EAC kuwa free kwa kila kitu ,usije shangaa watutsi na wanyankole wameshafiia nachingwea au namtumbo na mifugo Yao

Kila mtu ale keki yake[emoji1]
 
Huko Kenya undokaneni na ukabila wenu kwanza ndo tunaweza kukaa meza moja kujadiliana. Hatuwezi kuwa nchi moja na watu wanaouana kwa sababu ya kuwa makabila tofauti.
Ss tunauana sababu za kisiasa. Lakin tupo busy kunyooshea nchi zingine vidole kana kwamba tuko perfect sana.
Kila nchi ina madudu yake.
 
Nafikiri katika yote ubinafsi ndo sababu kubwa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…