Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona sisi tulibaki na majengo ya Arusha na tumeyatumia miaka na miaka.Wakenya mrudishe kwanza Ndege na mali za iliyokuwa jumuiya ya Africa Mashariki ndio tufikirie kurudi mezani...
Kinyume na hapo msahau.
Na wewe unajihesabu kuwa kwenye kundi la hao "wenye uwezo kushirikisha ubongo"? Kama hivyo ndivyo, sina sababu ya kuwa kwenye kundi hilo.Ndio maana nilisema uzi kama huu unapaswa kujadiliwa na wenye uwezo kushirikisha ubongo, wengine mtaishia kukojoa humu bila umuhimu wowote.
Hii ni mijadala inayoangalia zaidi ya miaka 100 ijayo.
"Ndiyo maana nchi yetu iko hapa leo"? Nchi 'isiyokuwa hapa leo' ni nchi gani, ile uliyoikimbia?
Ingekuwa hivyo usingeikimbia.
Unapojifanya wewe ni kondoo, unajificha kwenye kundi la kondoo, kumbe wewe ni fisi, unadhani watu hawawezi kutambua?
Ukweli ni kwamba hiyo ngozi ya kondoo haikufai kabisa, kwa sababu haifichi chochote wakati tabia ni zile zile za fisi.
Nisome vizuri unielewe nilichoandika hapa. Usirukie tu kujibu kwa mihemuko. Ni ujumbe mahususi niliokupa.
Maendeleo yanapatikana kwa njia mbalimbali. Usilazimishe utakavyo wewe.Negativity zilezile yaani ukiwa diaspora ni kukimbia nchi😂 wakati wengine wanaona ni kutafuta maslahi. Ni mtazamo wako mtatuita kila kitu fisi, kondoo, beberu nk lakini ukisoma ujumbe ni kwamba tunaongelea maendeleo ni mambo binafsi. Sijui ufisi una uhusiano gani na manunuzi, kampuni za ndege na kuweka viwango juu vya elimu!
Unaongelea shirika moja la ndege inaonekana umekurupuka kuandika hivi unajua kabla ya kuvunjika jumuhiya ya kwanza tulikuwa na mashirika kama hayo likiwemo la posta na mengineyo.
Unajua nini kilitokea baada ya jumuhiya kuvunjika kuna watanzania wenye uzalendo walitorosha ndege zilizokuja kuanzisha ATC. Sasa hivi tumechukua tahadhari zote kwani tunajuana vizuri wengine ardhi wamegawia wazungu halafu wanataka sisi tuwape ardhi.
Maendeleo yanapatikana kwa njia mbalimbali. Usilazimishe utakavyo wewe.
Na hata yangetegemea hiyo njia ya kuunda vikundi, kwani ni lazima kuwa na kikundi hicho unachokipigia upatu hapa? Mbona yapo makundi mengi tu ya kujiunga nayo kama ni lazima kuunda kundi!
Hatuna tofauti ya kiutamaduni yeyote makabila ni yaleyale. Arusha huku na Nairobi hakuna tofauti , wa pwani hawana tofauti nk hatuna tofauti ya kiutamaduni maana hatuna utamaduni wa nchi bali utamaduni wetu ni makabila.
Pili mawazo yangu sio ya kunufaisha nchi mmoja mfano tukiwgiza dawa pamoja gharama zitapungua lakini zikifika hapa kila nchi inachukua kiasi walicho agiza ni sawa na ku share container lakini hata bei itashuka. Kuhusu ndege mfano ni share sasa kuna shida gani kama tutapata ulicho wekeza.
Elimu mbona hao viongozi wetu wamesoma nje? Kwanini tusiwe na system ina fanana ili isiwe kila siku tunaambiwa elimu ya nchi mmoja iko chini? Sasa hapo kuna ukenya na Utanzania upi?
Mnao shinda kuogopa Kenya bado sielewi ni wapi watanufaika zaidi yetu maana mawazo yangu bado kila mmoja ana haki sawa
Sasa tuambie: "ulipoishi Bongo ulimwona mzawa wa huko mbali Kigoma", ulimwona huyo mkigoma akiwa na kisababu cha "kumwogopa mtu kutoka Laikipia?"
Na mtu wa kule Kwale au Kilifi, hapana, hata pale Baringo na sehemu nyingi tu huko Kenya yupo 'level' gani kielimu na mzawa wa huku Tanzania??
Ni vitu kama hivi msivyovitambua kuwa vinawasumbua sana watu wa huko, kiasi kwamba mnajisahau na kudhani nyinyi ni bora zaidi ya wengine, kumbe hamna lolote. Uoga wenu ndio unaowafanya mhangaike na vijimada visivyokuwa na mbele wala nyuma kama hii hapa.
..hakuna nchi inayomdai mwenzake.Wakenya mrudishe kwanza Ndege na mali za iliyokuwa jumuiya ya Africa Mashariki ndio tufikirie kurudi mezani...
Kinyume na hapo msahau.
Wewe ni mgumu sana kuelewa.Ingependeza kama ungekuwa unatoa mawazo yako badala ya kupinga tu na kuita watu majina bila sababu ya msingi.
Mawazo ya kuwa na viwango sawa vya elimu vitasaidia kila nchi hakutakuwa na visingizio mfano kwa wale wanaosema elimu yetu iko chini. Kuhusu kuunganisha mashirika ya ndege na kuwa na shirika moja kubwa ni logic rahisi tu kwenye biashara ya ndege big is better. Kuhusu kununua madawa pamoja ni kupunguza bei ya dawa na gharama kwa wana EA sasa sijui hapo lakupjnga lipi!. Pesa mmoja sijasema lakini ni vitu hivyo. Lakini sitaendelea kubiashana bila sababu kama una mawazo tofauti yatoe badala ya kupinga kwasababu tu ni Kamundu
Hujui maana ya maneno unapoyatumia, kama hilo la "Kutojiamini" mnapenda sana kulitumia upande huo.Yaani mtu ukiwa na mawazo tofauti tayari wanafikiri wewe ni Mkenya! na wenyewe tu ndiyo wazalendo wanaoipenda nchi kuliko wengine hizi ni akili za kutokujiamini!
Ss tunauana sababu za kisiasa. Lakin tupo busy kunyooshea nchi zingine vidole kana kwamba tuko perfect sana.Huko Kenya undokaneni na ukabila wenu kwanza ndo tunaweza kukaa meza moja kujadiliana. Hatuwezi kuwa nchi moja na watu wanaouana kwa sababu ya kuwa makabila tofauti.
Safari hii hatuna haraka,Kenya si watu wazuri hata kidogoKwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa
Unahitimisha mambo ya kipuuzi sana..., wewe sio mbongo? Lugha hiyo naisikia toka huko kwingine, wewe ni mmoja wa hao watu?Wabongo ni waoga Sana kwenye ushindani
Nafikiri katika yote ubinafsi ndo sababu kubwa zaidiHamna jipya haya unayoyaongea tulishayafanya na mpaka sasa tunajaribu lakini haitawezekana kwasababu ya tofauti zetu za kijamii,mila na desturi, malengo ya kiuchumi ,kisiasa na ubinafsi ndani yake.
Hujiulizi leo hii kwanini Britain anajitoa katika umoja wa ulaya.? Tuendelee kuvumiliana labda siku moja ndoto yakuwa pamoja itatimia.