KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Unatafuta pawepo tatizo mahali ambapo hakuna tatizo, ila unalolianzisha mwenyewe.Chief mimi na wewe wote wachangiaji na kwenye kuchangia mada kila mmoja ako na opinions zake!
Narudia tena maoni yangu muungano wa nchi za Africa mashariki na Africa kwa ujumla unafaida nyingi zaidi ya utengano, na kile ukionacho kibovu kwako kwa wengine kina thamani na kinyume chake!
Kwa mfano: hakuna anayekukatalia wewe kuona faida katika muungano wa nchi za Afrika mashariki. Wewe unapoona faida hizo, kuna wengine wanaona kivingine na unavyoona wewe. Hili sio kosa. Hawa nao wana haki ya kuona hivyo wanavyoona, na pia wana haki ya kukujibu wewe unapoandika mawazo yako hapa.
Usidhani kwa wewe kuona faida hizo, basi wengine wanaoona tofauti wasijibu mawazo yako uliyowasilisha hapa. Kama hutaki unayoamini wewe yajibiwe hapa, basi kaa nayo tu kichwani mwako. Ukiyaweka hapa, watu watayajibu tu. Kuna watakaokubaliana nawe, na kuna ambao hawatakubaliana nawe. Usitake wasiokubaliana nawe wasikujibu. Hilo haliwezekani.
Halafu usitake kupotosha. Sijaandika popote kwamba sioni faida katika ushirikiano baina ya nchi mbalimbali.
Najua haya ni matatizo ya elimu yetu ya kisasa, tunapata taabu sana kuchambua na kutofautisha mambo tunaposoma yaliyoandikwa.