Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Chief mimi na wewe wote wachangiaji na kwenye kuchangia mada kila mmoja ako na opinions zake!

Narudia tena maoni yangu muungano wa nchi za Africa mashariki na Africa kwa ujumla unafaida nyingi zaidi ya utengano, na kile ukionacho kibovu kwako kwa wengine kina thamani na kinyume chake!
Unatafuta pawepo tatizo mahali ambapo hakuna tatizo, ila unalolianzisha mwenyewe.

Kwa mfano: hakuna anayekukatalia wewe kuona faida katika muungano wa nchi za Afrika mashariki. Wewe unapoona faida hizo, kuna wengine wanaona kivingine na unavyoona wewe. Hili sio kosa. Hawa nao wana haki ya kuona hivyo wanavyoona, na pia wana haki ya kukujibu wewe unapoandika mawazo yako hapa.

Usidhani kwa wewe kuona faida hizo, basi wengine wanaoona tofauti wasijibu mawazo yako uliyowasilisha hapa. Kama hutaki unayoamini wewe yajibiwe hapa, basi kaa nayo tu kichwani mwako. Ukiyaweka hapa, watu watayajibu tu. Kuna watakaokubaliana nawe, na kuna ambao hawatakubaliana nawe. Usitake wasiokubaliana nawe wasikujibu. Hilo haliwezekani.

Halafu usitake kupotosha. Sijaandika popote kwamba sioni faida katika ushirikiano baina ya nchi mbalimbali.
Najua haya ni matatizo ya elimu yetu ya kisasa, tunapata taabu sana kuchambua na kutofautisha mambo tunaposoma yaliyoandikwa.
 
1) Nimetafuta na kuanzisha tatizo gani?!

2) Sijalazimisha opinion yangu ndio iwe sahihi, nimesema kibovu kwako chaweza kuwa kizuri kwangu na kinyume chake!!

3) Sijamzuia mtu yeyote kujibu opinion zangu kwa kupinga ama kusupport!!

Chief, umerandaranda mno!

Hoja yangu ni kwamba kila mmoja wetu hapa yupo kwa ajili ya kukubaliana na mleta mada ama kupingana nae na kila mmoja yuko na rights to their own opinion! Simama na hoja yako nami nisimame na yangu, Shukran!

“Elimu yetu ya kisasa “!! Una hakika nimeipata hiyo ya kisasa? Unafahamu elimu yangu??
 
1) Nimetafuta na kuanzisha tatizo gani?!
Hukusoma mfano niliokupa, mbona unaniuliza swali na kumbe nimekupa jibu hapo hapo?
2) Sijalazimisha opinion yangu ndio iwe sahihi, nimesema kibovu kwako chaweza kuwa kizuri kwangu na kinyume chake!!
Kwani kuna sehemu nimeandika kuwa "unalazimisha"?
Diversity is the real future! Na ndicho kinawabeba sana wamarekani mpaka sasa! Considering the fact of technology being the world’s current state, ujanja ni kuungana na sio kutengana!
Mfano mzuri wa "aina ya elimu yetu" niliyoandika juu yake na ukadhani kwa kuwa sijui elimu yako siwezi kudadisi kupitia ninayoyasoma unayoandika hapa. Na inawezekana kabisa bado usielewe ninachokueleza hapa kutokana na mstari huo, pamoja na kwamba nilikupa jibu kwa mfano wa China, Japan na kwingineko.
Chief mimi na wewe wote wachangiaji na kwenye kuchangia mada kila mmoja ako na opinions zake!
Hakuna popote "ulipokatazwa na yeyote kuwa na "opnion zako" katika kuchangia. Hili ni "tatizo" unalotafuta wewe liwe tatizo, na kumbe hakuna anayeona kuwa ni tatizo, kama lisivyokuwa tatizo kwa maoni ya wengine wanapojibu hayo unayoweka hapa; ikiwa kama njia ya kujihami.
Narudia tena maoni yangu muungano wa nchi za Africa mashariki na Africa kwa ujumla unafaida nyingi zaidi ya utengano
Kwa mara nyingine nirudie hapa: sijaandika mahali popote katika mjadala huu kwamba "muungano wa nchi" kadhaa hauna faida. Mada hii inahusu muungano wa nchi za "Africa Mashariki" pekee na sio hizo nyingine, na kwa mara nyingine tena, nirudi huko kwenye 'elimu' zetu. Mtu makini, hukaa kwenye mada, na sio kuingiza mengine yasiyohusika na mada.
 
Kwa ufupi tu umoja ni nguvu. Ukiangalia vizuri kuna vitu ambavyo wana EAC tungeweza kufanya pamoja na kurahisisha maendeleo ya nchi zote

1. Madawa tungeweza kuagiza pamoja maana tunaumwa magojwa yale yale hii ingesaidia kupunguza bei ya uagizaji kwasababu tuna nunua kwa jumla. Lakini kwenye chanjo kama za Corona tungeweza kuagiza kwa pamoja na kugawana zikifika hapa!.

2. Mfumo wa elimu tungeweza kuweka mfumo mmoja hii ingesaidia wawekezaji wakija kwenye nchi mmoja kuwa na vijana wenye elimu zenye uwiano sawa. Vilevile ingesaidia kwa elimu za madaktari na walimu.

3. Usalama pamoja na kuwa na majeshi yetu tungeweza kuwa na jeshi ya EAC kwa ujumla kupambana na ugaidi na ku share hata satellite za usalama. Hii ingepunguza matumizi mabaya ya kijeshi maana tumekuwa dump la kuuziwa vifaa vya kizamani.

4. Shirika la ndege moja ni vichekesho kuwa na shirika la ndege kila nchi ! Tungefungua kampuni moja halafu wawe wanakodisha ndege kutoka nchi shiriki na kila nchi itakuwa na share kutokana na mchango wake hii ingepunguza gharama na kuongeza ushindani bila hivi mashirika ya nje yataendelea kutawala anga zetu.

5. Masoko ya mzao ya pamoja yaani kuwe na shirika la kuonhoza masoko ya biashara za mazao na bei ziwe wazi na kutangazwa kote kuwe na masoko ya jumla kila mpakani ya kisasa. Kama ilivyo dhahabu bei za mazao ziwe zinatangazwa kwa uwazi .

6. Tuwe na vyuo vya technologia na ufundi pamoja kufundisha teknologia mpya kama programming. Fungueni kampuni na kuingia mkataba na kampuni kama Microsoft, google, Apple na Oracle ili vijana wetu waweze kufanya kazi kutokea nchi hizi washiriki.

India mfano wana vijana kwa milioni wanafanya kazi za nchi nyingine kuanzia engineering design, customer service, payroll and accounting, bank support. kwanini sisi tushidwe wakati tuna vijana wengi.

Kwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa.
Hii niliandika 2020 lakini bado ushauri uchukuliwe na serikali yetu na viongozi
 
Hayo mawazo ni mazuri sana, maana ukifuatilia waafrika wote tunafanana vitu vingi mno, ila hilo haiwezekani kwasababu waafrika tuna laana ya ubinafsi na kutopendana wenyewe kwa wenyewe na ndo maana hatuendelei, na hatutokuja kuendelea kamwe kama tutashindwa kuondoa hivyo vitu viwili
 
Back
Top Bottom