Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Utaifa wa EAC unachelewesha maendeleo

Kwani historia inahusu mambo ya sasa hivi?

..Historia ni jambo zuri.

..Na historia inatakiwa itusaidie kufanya maamuzi mazuri zaidi.

..Historia haitakiwi itukwamishe ktk kufanya maamuzi, au iwe kikwazo cha maendeleo ktk EAC.
 
Mimi Mkenya hapa, ila huu uzi ukijadiliwa na great thinkers wasiokua wazembe wa kushirikisha ubongo unaweza ukawa uzi muhimu sana JF. Afrika yote hii kinachotukwamisha ni hii mipaka ya mkoloni, hatuna nguvu ya wingi au volume inayotumika na walioendelea, kwa mfano China wale wako bilioni moja, yaani ukikuza matikiti yako uko na uhakika wa soko la watu bilioni ambao unaweza ukawafikia bila kikwazo, Marekani wako zaidi ya milioni mia tatu, watu wote hao kama soko moja.

Afrika hapa tuko watu zaidi ya bilioni moja ila tunabanana na kuzongana kwa misingi ya viinchi, vingine hata saizi ya mkoa kama vile Rwanda na Burundi, hauwezi kuvusha chochote uuze hapo Kigali bila kupitia usumbufu wa kufa mtu.

Hapa EAC siku tutakuja kubuni mtaala wa pamoja ndio huu uwoga wa kuogopana utaisha, mzawa wa huko mbali Kigoma akiwa kwenye level moja kielimu na mzawa wa huku Kenya maeneo ya mbali kama vile Laikipia, hapo hapatakua na kijisababu cha kuogopana. Nimeishi Bongo, nimekatiza mikoa na wilaya nyingi sana, sijaona chochote tofauti na kwetu huku, masela mitaani ni wale wale, vijana vijiweni pande zote mbili hujadili yale yale tu ya akina Manchester United sijui Arsenal.
big up sana Omera nakuunga mkojo. Kuna vizee vijinga sana pande hizi mbili eac ilikuwa moja tu.

mzungu kawagawa ikawa hivo mpaka leo naona km walituroga hivi. Eti anakata nchi km andazi na inakuwa hivo hadi leo!

Jitu kubwa lina nywere nyeupe kila mahali linaogopa kuungana. Eti mara huyu hivi mara hivile yaani ijinga mtupu.

hapa ni kuzichapa tuondoe wajinga wote tubaki damu mupya!
 
Kama wewe wakati ule wa EAC ya zamani ulikuwa hujazaliwa, uwe unasoma basi angalao historia ya EAC kabla ya kuja na mawazo kama haya. Tunatakiwa kwanza kujua tulikotoka, mahali tulipo kabla ya kuamua tunakotaka kwenda.

Mara baada ya nchi za Uganda chini ya rais Milton Obote, Kenya (Jomo Kenyatta) na Tanzania (Julius Nyerere) kupata uhuru wake kutoka kwa muingereza ziliungana pamoja na kuunda EAC ambapo shughuli zote za kiuchumi na maendeleo za nchi hizi ziliendeshwa kwa pamoja kupitia umoja huo wa EAC. Hata pesa (currency) ilikuwa ni moja = East Africa shilling chini banki kuu moja ya EAC. Njia za mawasiliano, reli, ndege, meli, bandari na anga zote zilimilikiwa kwa pamoja. Viwanda vyote vilivyokuwa vinazalisha bidhaa mbali mbali hususani zana za kilimo, mafuta ya kula, blue band, beer na kadhalika vyote vilikuwa vinamilikiwa na EAC.

Lengo la waasisi wa umoja wa EAC lilikuwa baadaye nchi hizo tatu kuja kuungana kuwa nchi moja chini ya rais mmoja. Kilichokuja kutokea ni majonzi ambayo hatupaswi kuyasahau. Nchi ya Tanzania ilikuwa na siasa za kushoto, yaani za kijamaa, hivyo haikuwa inapendwa na nchi za magharibi. Nchi ya Uganda ilikuwa na siasa za kati. Kenya ilikuwa na siasa za kulia yaani za kibepari (capitalism) na hivyo ilikuwa kipenzi cha nchi za magharibi. Hata wazungu waliokuwa wakoloni wengi wao hawakuondoka Kenya baada ya uhuru. Wazungu hao walibaki huko wakimiliki mashamba makubwa makubwa (estates) na njia kuu za kiuchumi. Kwa kuwa wafadhili wakuu wa maendeleo ya nchi hizo za EAC walikuwa ni kutoka nchi za magharibi, walihakikisha karibu viwanda vyote vya EAC vilikuwa vinajengwa nchini Kenya - Nairobi, Mombasa etc. Ili kutupumbaza, kitu pekee kilichojengwa Tanzania ni jengo la makao makuu ya EAC pale Arusha.

Janja janja nyingi zifanyika kwenye jumuiya hiyo zikiendeshwa na upande wa Kenya walianza na kujitoa kwenye currency ya EAC. Wakaanzisha KSh na benki kuu yao. Mwaka 1977 wakati Tanzania tukigombana na Nduli Iddi Amini wa Uganda, Kenya walipora mali zote za EAC na kuvunja jumuiya hiyo. Kabla ya kuivunja walihakikisha vitu kama ndege zote za EAC, meli zote na train zote ziko nchini kwao. Hivyo tukajikuta hatuna hata kiwanda cha kutengeneza sabuni, bia, kiberiti, sindano wala cho chote kile. Yaani nchi yetu ikawa fukara wa kutupwa. Tukaanza upya from the scratch tena kwenye wakati mgumu sana kwani ilikuwa tunatoka kwenye vita dhidi ya nduli Amini iliyokuwa imetugharimu sana. Baada ya kufanya uporaji huo wa viwanda vya EAC, nchi ya Kenya ikawa ni nchi ya viwanda na soko kubwa la mazao ya viwanda hivyo likawa ni Tanzania na Uganda hadi leo.

Sasa baada ya kupitia yote hayo, tumejikongoja na kujenga viwanda, uchumi wetu unaendelea kupaa kwa spidi kubwa na karibu uchumi wetu utaupita huo wa Kenya: sasa utakuwa ni mjinga kiasi gani kuanzisha tena muungano wa aina hiyo na watu wa aina hiyo hiyo? Wanajifanya tumesahau waje watukwapue tena. Never over our dead bodies!
Tunapoandika humu tujaribu kuandika mambo ya ukweli na kuacha upotoshaji wa kijinga.

Baada ya uhuru wa Tanganyika, nchi hii ikiwa chini ya utawala wa Mwl Nyerere iliamua kufuata mfumo wa ujamaa na kujitegemea na ndipo mwaka 1967 Nyerere alipoamua kutaifisha mali zote za mabepari baada ya kutangaza azimio la Arusha.

Na kimsingi matatizo ya Tanzania yalianzia hapo rasmi, vita ilikuja kuongezea tu balaa ambalo tayari liliisha kuwepo.

Tanzania baada ya kuwadhulumu matajiri mali zao haikuweza kupata tena wawekezaji na eti serikali ndio ikageuka kuwa mwekezaji mambo anayotaka kutuletea tena Magufuli leo.

Nchi ikabaki bila viwanda na kilimo kikabaki kwa watu maskini ambao hawakusoma na wale waliokata tamaa ya maisha. Nchi ikawa inanyemelewa na njaa hadi Nyerere kwenda nje kutembeza bakuli.

Itakumbukwa kwamba jumuiya ilivunjika mwaka 1977 na vita vya Tanzania na Uganda vikaja kuanza Novemba 1978 hadi Aprili 1979.

Itakumbukwa kwamba Kenya ilikuwa ni koloni kamili la Uingereza na hivyo waliwekeza sana huko tofauti na walivyofanya Uganda na Tanzania.

Hivyo sera ya Nyerere ya ujamaa ndio ilikuwa msingi wa Tanzania kuwa na uchumi dhaifu toka mwanzo na hiyo fikra aliyowarithisha watu walio kwenye mamlaka ktk nchi hii hadi leo ndio imekuwa chanzo cha nchi hii kutokupiga hatua yoyote ya maana katika maendeleo pamoja na kuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi kama Kenya na Uganda.

Tanzania haina nafasi yoyote ya kuipiku Kenya kiuchumi kwani kufuatia yanayoendelea katika nchi hii kwa sasa tukinyimwa tu haki ya kukopa.....tumeisha ndani ya wiki moja tu, sasa uchumi tegemezi hivyo una kipi cha kutambia, absolute nothing.
 
..kila wakati waTz tunasema hatuko tayari ktk masuala ya EAC.

..yaani sisi waTz ndio wenye kigugumizi ktk mambo mengi ya EAC kuliko wanachama wenzetu.

..mimi nataka kujua jambo moja ambalo waTz tuko tayari, au tunalitaka ktk EAC, lakini wenzetu hawako tayari au wanaliogopa.

..kwa mtizamo wangu VIONGOZI wa Tz ni incompetent ktk kuwaandaa waTz ili kufaidika na fursa zinazotokana na malengo na mipango ya EAC.
Tumezoea kukaa kwenye jumuia za kupiga domo. Wakisema tufanye vitendo mambo yaende tunaanza visingizio.
Mi mwenyewe huwa najiuliza, hivi hatuna jambo ambalo tukilipeleka huko EAC litatufaidisha sana sisi? Kwanini kila mara wenzetu wanaleta miswada tunagoma eti haitatufaidisha lakini sijasikia sisi tukipeleka!. Tupo defensive muda wote. Mfano, sisi tuna advantage kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula, tumewahi peleka mswada kuwe na soko huru la chakula EAC? Ni kama hatutaki huu muungano ila tunaogopa kuwaambia wenzetu.
Kwa deadline waliyojiwekea nafikiri mwaka huu tulikuwa tuwe na sarafu ya EA.
Mi naona bora nchi zingine zitutoe kwenye jumuia. Uganda, Kenya, Rwanda na SS waunde jumuia yao. Sisi wazembewazembe tubaki hivyohivyo.
 
Mleta mada nakuunga mkono asilimia Mia!

Diversity is the real future! Na ndicho kinawabeba sana wamarekani mpaka sasa! Considering the fact of technology being the world’s current state, ujanja ni kuungana na sio kutengana!

Ipo siku kama sio watoto wetu basi wajukuu zetu wataifanya Africa Taifa moja, United Nations of Africa (UNfA the f will be silent). Ipo siku!

Hata wahenga wa kabla ya Uhuru walisema “umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu “ (bahati mbaya wengine tukatafsiri in terms of vijiji vya ujamaa)
 
..kila wakati waTz tunasema hatuko tayari ktk masuala ya EAC.

..yaani sisi waTz ndio wenye kigugumizi ktk mambo mengi ya EAC kuliko wanachama wenzetu.

..mimi nataka kujua jambo moja ambalo waTz tuko tayari, au tunalitaka ktk EAC, lakini wenzetu hawako tayari au wanaliogopa.

..kwa mtizamo wangu VIONGOZI wa Tz ni incompetent ktk kuwaandaa waTz ili kufaidika na fursa zinazotokana na malengo na mipango ya EAC.
mngekuwa mnafikiri sawa sawa mngejua engene ya huu muungano ni TZ,ndio maana inaposua sua hakuna kinachoendelea.TZ yenyewe binafsi imeshajua ndio maana hamuoni ikiunga mkono wa hili swala.

EA inaihitaji TZ kuliko TZ inavyoihitaji EA.
kuna Kenya,UG na Ethiopia wanaweza wakiamua,waache uoga.
 
Diversity is the real future! Na ndicho kinawabeba sana wamarekani mpaka sasa!
Mbona hujazungumzia waChina, Wajapan, n.k.; wao hawakujibeba?

Hujawahi kumsikia Trump akilalamika kuhusu NAFTA, ushirikiano kati ya Mexico, Canada na USA?

Hiyo 'diversity' unayozungumzia ni kitu tofauti kabisa na haya yanayojadiliwa hapa.

Hakuna anayekataa kushirikiana na wengine, lakini ushirikiano hauwezi kulazimishwa.

Kushirikiana sio swala la kushirikiana tu, ni lazima nchi washirika wawe ni nchi zinazopenda kushirikiana kwa dhati, huwezi kutaka ushirikiano kwa nchi moja kudhani itafaidika zaidi ya washirika wenzake kwa hira au mbinu chafu..
 
Chief, ni mjadala huru hence mawazo huru! Huo ndio mtazamo wangu!

Lakini ipo siku East Africa na Africa itasimama pamoja kama kitu kimoja chenye kauli moja! Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!

Ipo siku!
 
Kwani wanaokwamisha shirikisho la EAC ni nani kama sio wabongo?
Swali ni: Kwanini iwe lazima kuwa na "shirikisho la EAC"?

Kwani hatuwezi kuwa na 'Mashirikisho' mengine, mbona tunao majirani wengi tu wa kuunda shirikisho nao?
 
mngekuwa mnafikiri sawa sawa mngejua engene ya huu muungano ni TZ,ndio maana inaposua sua hakuna kinachoendelea.TZ yenyewe binafsi imeshajua ndio maana hamuoni ikiunga mkono wa hili swala.

EA inaihitaji TZ kuliko TZ inavyoihitaji EA.
kuna Kenya,UG na Ethiopia wanaweza wakiamua,waache uoga.

..ninavyoelewa mimi engine inarahisha kazi, badala ya kufanya kazi ziwe ngumu zaidi.

..sasa kama Tz ni engine ya eac basi tulitakiwa tuonyeshe njia kwa wenzetu, tuwe chachu na siyo kikwazo ktk jumuiya.

..yako mambo mengi ambayo yanatokea ktk jumuiya na reaction ya serikali na wananchi wetu ni kama vile tumeshtukizwa.

..serikali yetu inajua nini kinachokuja mbeleni ktk masuala ya integration lakini wananchi hawaandaliwi ku-take advantage au kukabiliana na hali hiyo.

..Labda nikupe mfano mdogo...Tanzania tuna population kubwa kuliko majirani zetu, kwa hiyo sisi ndio wenye labour force kubwa zaidi. Je, tumefanya marekebisho na maboresho yoyote ktk mfumo wetu wa elimu ili vijana wa Tz wawe in high demand kujaza soko la ajira la Afrika Mashariki?

..Unaposema EA inaihitaji Tz kuliko Tz inavyoihitaji EA una maana gani? Nchi za EA zinahitaji waalimu toka Tz? Zinahitaji Engineers toka Tz? Zinahitaji bidhaa za viwandani toka Tz?

..Wenzetu wanatuhitaji "Watanzania", au wanaihitaji "Tanzania"? Na kwanini?
 
Chief, ni mjadala huru hence mawazo huru! Huo ndio mtazamo wangu!

Lakini ipo siku East Africa na Africa itasimama pamoja kama kitu kimoja chenye kauli moja! Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!

Ipo siku!
Ni wapi nilipokukataza kuwa na "mawazo yako"; kwani mimi hutaki niwe na mawazo yangu kama hayo niliyoyatoa?

Tatizo liko wapi?
 
Ni wapi nilipokukataza kuwa na "mawazo yako"; kwani mimi hutaki niwe na mawazo yangu kama hayo niliyoyatoa?

Tatizo liko wapi?

Mtazamo wangu; kuungana EAC ni bora na Faida zaidi kuliko hasara!

Mtazamo wako; sio bora wala sio lazima, miungano ipo mingi!

Kila mmoja abaki na wake. Ahsante
 
Mtazamo wangu; kuungana EAC ni bora na Faida zaidi kuliko hasara!

Mtazamo wako; sio bora wala sio lazima, miungano ipo mingi!

Kila mmoja abaki na wake. Ahsante
Sasa nikitaka kukueleza kuwa "EAC" sio bora na haina "Faida zaidi" utaona nimeingilia mawazo yako?
Ingekuwa hivyo basi ungekaa nayo mawazo yako hayo na usiyaweke hapa.
Ukishaweka hapa ukumbini, maana yake ni kwamba unakaribisha mawazo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na yale yanayopingana na yako.
 
..ninavyoelewa mimi engine inarahisha kazi, badala ya kufanya kazi ziwe ngumu zaidi.

..sasa kama Tz ni engine ya eac basi tulitakiwa tuonyeshe njia kwa wenzetu, tuwe chachu na siyo kikwazo ktk jumuiya.

..yako mambo mengi ambayo yanatokea ktk jumuiya na reaction ya serikali na wananchi wetu ni kama vile tumeshtukizwa.

..serikali yetu inajua nini kinachokuja mbeleni ktk masuala ya integration lakini wananchi hawaandaliwi ku-take advantage au kukabiliana na hali hiyo.

..Labda nikupe mfano mdogo...Tanzania tuna population kubwa kuliko majirani zetu, kwa hiyo sisi ndio wenye labour force kubwa zaidi. Je, tumefanya marekebisho na maboresho yoyote ktk mfumo wetu wa elimu ili vijana wa Tz wawe in high demand kujaza soko la ajira la Afrika Mashariki?

..Unaposema EA inaihitaji Tz kuliko Tz inavyoihitaji EA una maana gani? Nchi za EA zinahitaji waalimu toka Tz? Zinahitaji Engineers toka Tz? Zinahitaji bidhaa za viwandani toka Tz?

..Wenzetu watuhitaji "Watanzania", au wanaihitaji "Tanzania"? Na kwanini?

sijui kama umenielewa au mawazo unachojua ndicho nilitaka ukielewe ila tayari unakijua ila kwa namna tofauti kidogo.

niliposema ni engene sio kwa maana ya kwamba tayari tunaendesha EAC,hapana.ni kwamba sisi ndio hot cace ya muunganiko huo.ndio maana tunaposita kutia miguu yote,muungano wote unakosa mashiko.rejea UK na EURO.

hiyo pop ndio backup no 2 ukiondoa ardhi,sisi tunayoitegemea kiuchumi,rejea china na uchumi wake.ina jitoshereza kwa soko la ndani kibiashara na viwanda.kuhusu kujiandaa kuwa na workforce hilo lisikutishe,ndio sababu vyuo na shule zinajengwa kila siku,ukiacha miaundombinu.

ninaposema EA inaihitaji TZ namaanisha hapo juu,kwa maana kujibu swali lako TZ haihitaji eng kutoka nchi nyingine hapa tz,wala dr,wala mtaalamu yeyote.

wenzetu wanahitaji TZ sio watz,ndipo kigugumizi cha tz kilipo.so for now wacha kila mtu ashinde mechi zake tu.
 
wenzetu wanahitaji TZ sio watz,ndipo kigugumizi cha tz kilipo.so for now wacha kila mtu ashinde mechi zake tu.

..asante.

..mimi nadhani na sisi inabidi tujiongeze ili wenzetu watuhitaji "watanzania."

..Ni kweli tuna ardhi kubwa kuliko wenzetu, na ninaunga mkono kuilinda kwa ajili ya waTz.

..lakini hali itaendelea hivyo kwa muda gani kabla hatujaanza kubanana wenyewe kwa wenyewe?

..Tukumbuke kwamba ardhi haiongezeki, kwa hiyo tujiandae kwa EA ambapo ardhi ni ndogo hata kwa Watanzania wenyewe.
 
Hatuna tofauti ya kiutamaduni yeyote makabila ni yaleyale. Arusha huku na Nairobi hakuna tofauti , wa pwani hawana tofauti nk hatuna tofauti ya kiutamaduni maana hatuna utamaduni wa nchi bali utamaduni wetu ni makabila.

Pili mawazo yangu sio ya kunufaisha nchi mmoja mfano tukiwgiza dawa pamoja gharama zitapungua lakini zikifika hapa kila nchi inachukua kiasi walicho agiza ni sawa na ku share container lakini hata bei itashuka. Kuhusu ndege mfano ni share sasa kuna shida gani kama tutapata ulicho wekeza.

Elimu mbona hao viongozi wetu wamesoma nje? Kwanini tusiwe na system ina fanana ili isiwe kila siku tunaambiwa elimu ya nchi mmoja iko chini? Sasa hapo kuna ukenya na Utanzania upi?

Mnao shinda kuogopa Kenya bado sielewi ni wapi watanufaika zaidi yetu maana mawazo yangu bado kila mmoja ana haki sawa
Kenya sio kama tunawaogopa ishu ni ndumi la kuwili hatuhitaji ushirikiano nao
 
Kenya sio kama tunawaogopa ishu ni ndumi la kuwili hatuhitaji ushirikiano nao

Watanzania tuna utamaduni wa kujidanganya na kujiaminisha uongo. Mfano sio wazo baya kuammua kwamba kama nchi hatutafanya lock down ya Corona kwa sababu za kiuchumi lakini hiwezi kuwa na akili zako ukafikiri corona haipo kabisa au inaishia kwenye mipaka Lakini kwasababu tunapenda kujidanganya tunatumika kwa faida binafsi. Hivyo ni ngumu kujadili mambo kama watu wameamua kuamini uongo. Mengi tunayo amini kuhusu jirani zetu ni uongo.
 
Sasa nikitaka kukueleza kuwa "EAC" sio bora na haina "Faida zaidi" utaona nimeingilia mawazo yako?
Ingekuwa hivyo basi ungekaa nayo mawazo yako hayo na usiyaweke hapa.
Ukishaweka hapa ukumbini, maana yake ni kwamba unakaribisha mawazo mbali mbali, ikiwa ni pamoja na yale yanayopingana na yako.

Chief mimi na wewe wote wachangiaji na kwenye kuchangia mada kila mmoja ako na opinions zake!

Narudia tena maoni yangu muungano wa nchi za Africa mashariki na Africa kwa ujumla unafaida nyingi zaidi ya utengano, na kile ukionacho kibovu kwako kwa wengine kina thamani na kinyume chake!
 
Back
Top Bottom