Utajiri hauwezi kununua furaha je umaskini unanunua nini?

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,445
Reaction score
7,987
Watu wengi wanafikiri umaskini unatokana na udogo wa mshahara, lakini ukweli mchungu ni kwamba unatokana na mlolongo wa makosa ya kifedha unaoyafanya kila tarehe Mosi. Unapokea fedha, unalipia kila mtu mwingine kwanza, kisha unalia huna akiba pindi mwezi unapoisha.

Kama alivyowahi kusema bilionea na tajiri mzee Warren Buffett: "Usihifadhi kile kilichobaki baada ya kutumia, bali tumia kile kilichobaki baada ya kuhifadhi."

Sentensi hii moja ndiyo siri kuu inayotofautisha watu wanaojenga mafanikio ya kudumu na wale wanaobaki kwenye mtego wa kuishi kwa ajili ya kulipa bili kila mwezi:

Tabia ya kusema utaweka akiba au kuwekeza kile kitakachobaki mwisho wa mwezi ni mtego wa kisaikolojia. Hamna pesa inayowahi kubaki. Saikolojia ya mwanadamu inalazimisha matumizi kuongezeka ili kuenea kwenye kiasi chochote cha fedha kilichopo mkononi. Usipotenga akiba yako sekunde ile ile pesa inapoingia, utajikuta umeinunulia vitu visivyo na msingi, na mwisho wa mwezi utabaki ukiwa huna hata mia.

Mshahara au faida ya biashara ikingia, mtu wa kwanza anayepaswa kulipwa si mwenye nyumba, si duka la nguo, wala si mwenye baa ni baadaye yako. Tenga asilimia 10 hadi 20 ya kipato chako mara moja na uiipeleke kwenye uwekezaji au akaunti ya akiba kabla hujagusa senti moja kwa ajili ya matumizi mengine. Hiyo ndiyo pesa inayokufanyia kazi ya kukununulia uhuru wako wa baadaye.

Watu wengi wanatumia kanuni ya kimasikini: Kipato - Matumizi = Akiba.

Wanaofanikiwa wanatumia kanuni ya kitajiri: Kipato - Akiba = Matumizi.

Ukishaondoa fungu la uwekezaji kwanza, unalazimisha akili yako kuishi na kubana matumizi kwenye kile kiasi kilichobaki, bila kuhatarisha hatima yako ya kifedha.

Mafanikio hayajengwi na kiasi cha fedha unachotengeneza, bali unajengwa na nidhamu ya kiasi unachokilinda. Acha kuilisha dunia nzima huku ukijiacha mwenyewe ukiwa mikono tupu.

Anza kujilipa mwenyewe kwanza kuanzia leo!
 
Mambo ya the richest man in Babylon subiri watakuambia MAISHA hayana formula ni kweli ila yana kanuni.
 
Mkuu,

Ukisema "Usihifadhi kile kilichobaki baada ya kutumia, bali tumia kile kilichobaki baada ya kuhifadhi." una assume kwamba kuna kinachobaki katika matumizi.

Hii ni kauli ya mtu anayeweza kuwa na kinachobaki baada ya matumizi, anayefikiria kila mtu anacho cha kuhifadhi baada ya natunizi.

Ni kauki ya entitlement.

Unakariri maneno umya Warren Buffet Mmarekani bila kujua wenzako wana pesa za tangu enzi za utumwa huko.
 
Unanunua "mateso".
 
Suala umasikini hasa wa kipato lina sababu nyingi na chanzo chake kinatoka mbali.

Tunakubaliana kabisa kuweka akiba. Hatahivyo, kuna swali muhimu hapa, ambalo tunatakiwa kujibu: "mifumo yetu ya maisha inaruhusu kuweka akiba"?

Tuwahimize watu kuweka akiba that is right. Lakini kama watu makini tujiulize: kwanini watu hawawezi kuweka akiba?
 
Ni ushauri mzuri Tu unaoweza ku apply Kwa watu wengi Sana duniani...Akiba ni kitu cha msingi na muhimu kwenye maisha yetu. Kwa wale wenzangu na Mimi chini ya dola moja Kwa siku inabidi uongee juhudi Tu za kutafuta pesa kwasababu ukianza kupiga hizo asilimia za Akiba unaweza kujikuta unaishi kama MBWA MWITU MTAANI...but generally Akiba ni muhimu Kwa malengo ya baadae hivyo nidhamu ni muhimu Sana.
 
Mkuu,

Ukisema "Usihifadhi kile kilichobaki baada ya kutumia, bali tumia kile kilichobaki baada ya kuhifadhi." una assume kwamba kuna kinachobaki katika matumizi.

Hii ni kauli ya mtu anayeweza kuwa na kinachobaki baada ya matumizi, anayefikiria kila mtu anacho cha kuhifadhi baada ya natunizi.

Ni kauki ya entitlement.

Unakariri maneno umya Warren Buffet Mmarekani bila kujua wenzako wana pesa za tangu enzi za utumwa huko.
Unaweza ukawa sahihi mkuu Lakini mara nyingi ukiwa na kinachozidi na matumizi yanakuwa makubwa nidhamu inapotea kwahiyo hoja yangu bado Ina logic bila kujali nukuu ya Warren Buffett.
 
Hoja yako inatakiwa kupigiwa mstari hapo kwenye neno "ukiwa".

Ama sivyo unaweza kuingia kwenye mtego, mtu hana hata ugali kidogo ukamwambia kama hana ugali basi ale pilau. Wakati yeye anaposema hana hata ugali maana yake pilau hawezi kuimudu.

Kuna watu wengi hata wakiwa na nidhamu, waka save 100% ya wanachopata, waka invest, hiyo pesa bado ni ndogo tu wakipata dharula moja tu ya afya inamalizika.

Kwa hiyo hapo mambo mengine watu wanashindwa si kwa sababu ya kukosa nidhamu wao binafsi.

Wanashindwa kwa mifumo kutokuwa mizuri, uchumi kukosa uthabiti. Jamii kukosa safety net hata kwenye mambo kama afya.

Mtu anakuwa na nidhamu ya ku save kwa miezi sita, halafu anafukuzwa kazi kwa sababu za nje ya uwezo wake za uchuni qa nchi. Sasa hapo nidhamu ya ku save itamsaidiaje awndelee ku save?

Haya mambo ukitaka kuyatatua ni muhimu ku addeess matatizo ya kimfumo kwanza.

Huku kwenye kulaumu watu hawana nidhamu utawaonea wengi tu.

Kwa sababu nidhamu ya kutumia inataka uwe nazo za kutumia kwanza.

Sasa mtu ambaye hana za kutumia, ambao ndio wengi hao Tanzania, nidhamu ya kutumia itamsaidia nini?
 
Mkuu,

Ukisema "Usihifadhi kile kilichobaki baada ya kutumia, bali tumia kile kilichobaki baada ya kuhifadhi." una assume kwamba kuna kinachobaki katika matumizi.

Hii ni kauli ya mtu anayeweza kuwa na kinachobaki baada ya matumizi, anayefikiria kila mtu anacho cha kuhifadhi baada ya natunizi.

Ni kauki ya entitlement.

Unakariri maneno umya Warren Buffet Mmarekani bila kujua wenzako wana pesa za tangu enzi za utumwa huko.
Wana pesa tangu enzi za utumwa wao??
 
Wana pesa tangu enzi za utumwa wao??
Nawakumbusha Waafrika wanaotumia sana maneno ya matajiri wa Kimarekani, ambao wameishi maisha tofauti sana na Waafrika, kuwa hao matajiri wa Kimarekani sio wenzao, wengine ukichunguza utajiri wao, unakuta umetokea mbali tangu kwenye biashara ya utumwa.

Kwa hiyo, unapochukua maneno ambayo pengine Mmarekani kayatoa kwa hadhira ya Wamarekani wenzake wenye historia kama yake yeye, ni muhimu kuelewa muktadha mkubwa, usije kujikuta wewe Mmasai utajiri wenu ng'ombe, unaiga maisha ya Warren Buffet utajiri wake upo kwenye stock market na una historia ndefu mpaka kwenye enzi za utumwa huko, bila kuweka muktadha huo sawa.
 
Hakika
 
Back
Top Bottom