Utajiri ni rahisi kuupata ila masharti yake ni magumu

Utajiri ni rahisi kuupata ila masharti yake ni magumu

Siri kubwa ya utajiri ni kuheshimu pesa, nunua mahitaji ya muhimu tu. Huwezi kuweka heshima bar wakati wa utafutaji na ukawa tajiri.

Unapangisha nyumba Masaki kodi milioni 2 kwa mwezi na wewe unataka kuwa tajiri.

Unakwenda shopping Dubai, unanunua designer handbags na viatu, na wewe unataka uwe tajiri.
Nakubaliana nawe.
 
Mungu ndiye mmiliki wa vyote duniani, lakini hatoi utajiri kwa watu ambapo anajua utajiri ule utaipoteza roho yako.
Sijakuelewa.....unamaanisha kuwa hakuna utajiri unaotokana na mbarikiwe na MUNGU au?!
 
Kichwa cha habari ..kimebebs ujumbe mzito
Mada uozo mtupu

Mtoa mada kapimwe akili
 
Ukiona mtu katajiri jambo la kwanza utajiuliza mbona mimi nimeshindwa kuwa kama yeye.

Napo sema utajiri ni rahisi kuupata kwa sababu njia zake ni rahisi pale utakapo gundua unapatikanaje kama fursa,soko,bei na n.k

Matajiri wengi tunao waona na wengine wakubwa wamekuwa wakitupa njia za kutajirika hata kutuandikia vitabu vya mbinu na wengine kuwa wana hamasa mitandaoni huku wakituonesha ufahali na bata kibao.

Ila katika urahisi ambao hupo kwenye utajiri ni mgumu sana katika masharti yake.

Masharti yake ya kufanikiwa

* Kuwa mdhulumati
Ukiona watu wengi waliofanikiwa sehemu kubwa ni wazulumati kwenye biashara za watu kama malipo duni,mgao mdogo,ubinafsi wa kumiliki bila kuangalia wengine,utapeli,kulithi mali zisizo zake n.k

* Kuwa tapeli
Hii ya utapeli aina tofauti na uzulumati maana matajiri wengi utapeli watu na kupata pesa ya haraka mifano mingi tunayo na wengine walikuwa hapa JF,hata dada yetu mmoja alitamba insta kwa maisha mazuri.

* Biashara haramu
Hili suala watu wengi wametumia kama sehemu kubwa ya kupata utajiri kwa kasi kama kukwepa kodi,biashara za magendo,wizi,madawa,unyang'nyi ,kuhuza mwili na n.k

* Imani za kishirikina
Wasio amini uchawi hupo basi tambua hupo kwa sababu watu wanaingia kutoa maisha ya wapendwa wao,mazezeta,damu za watu na n.k ili kulinda na kuongeza mali zikuwe kwa njia wanazo jua wao.

* Roho mbaya
Ili kupata utajiri itakubidi kuwa na roho mbaya ili kufanikiwa hata ikibidi shetani kuwa karibu yako.

Ndio maana ule msemo :

Ni heli Ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri labda kwa uhuruma ya mungu.
Mkuu umeshashindwa maisha kabla ya kuyaanza.
 
Na wa Barrick ninao kunywa nao hawapo kishirikina kama unaokunywa nao!

huna unacho kijua na ujui unacho kifanya.na inaonyesha ni muajiliwa tu.biashara uzijui kaa kimya
 
Akina Ibrahim Ayubu na Suleman, hakuna aliyejua asili ya utajiri wao, labda walitubu mwisho na kumrudia Mungu. Hata mtu wa misukule akitubu anasamehewa. Mtoa hoja nakuunga mkono, hakuna utajiri halali. Ni maujanga ya ajabu, mengine ni aibu sema tu ni Siri ya mhusika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisha kata tamaa ww usipende kukatisha na wengne
 
Inaonekana jamaa ana mtazamo mfupi. Ukiangalia maelezo ya hoja yake, ameangalia kundi dogo sana la watu (a very narrow segment). Nadhani mtazamo wake ulikuwa juu ya matajiri wa nchini kwetu, hakuangalia nchi/mabara mengine.

Angeangalia na matajiri wa nchi nyingine za Ulaya au Marekani, nadhani asingekuja na conclusion hiyo.

Kwa utafiti wangu mdogo/mfupi, nimeona kuwa matajiri wengi ni professionals wa fani fulani, ambapo huzigeuza fani zao na kuzifanya ujasiriamali. Matajiri kama akina Bezos, Bil Gate, Ellon Musk, Mark Zukeberg, na wengine wengi; ni either wahandisi au programmers. Ila kibongobongo, ukimwambia mtu hivyo, hakuelewi, badala yake anakuambia lazima ushirikina uhusike.
 
Watu wanatafuta sababu rahisi rahisi za kujihalalishia kushindwa maisha.
maisha ni kama mtihani wa darasani unatakuwa mtu afaulu kuna sababu nyingi za mtu kufeli au kufaulu.... na kila mtu anaweza kufaula, kwa mfano watoto walipo shule za kulipia hawana tofauti za kibiologia na wa st. kayumba lakini utakuta wa st. junior wanafaulu mtihani darasa zima, kuwa tajir inawezekana kwa kila mtu.
 
Siri kubwa ya utajiri ni kuheshimu pesa, nunua mahitaji ya muhimu tu. Huwezi kuweka heshima bar wakati wa utafutaji na ukawa tajiri.

Unapangisha nyumba Masaki kodi milioni 2 kwa mwezi na wewe unataka kuwa tajiri.

Unakwenda shopping Dubai, unanunua designer handbags na viatu, na wewe unataka uwe tajiri.
Hakuna maskini anaepangisha nyumba kodi mil 2 na apate chenji ya kwenda shopping 🛍 DUBAI... labda maskini JEURI
 
Back
Top Bottom