Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe

Nimelipenda bandiko lako mtoa mada,yapo mengi nakubaliana nayo.
 
Siku vijana wa jf wakiijua siri ya utajiri watakwenda kukojoa getini Ikulu ya Chamwino.
Pesa mbaya sana

Hahahha!

Ikiwa kijana akipata tuu milioni 10
anaona amepata pesa anaanza kudharau waru, kulewa hovyo, kunya na kukojoa hovyoo, kunyamba na kutema mate hovyo, unafikiri hiyo milioni 10 zitakubali hayo?
 
Kabisa siri ndo utajiri wenyewe.
 
Kisa kingine,
Miaka ya nyuma, nlipata mchongo na wazungu flani.
Ilkua biashara ya kununua magogo Aina flani ya miti kutoka kusini

yanakusanywa, kontena likijaa nawataarifu

Wanakuja na mashine yao, wanayasaga saga mogogo yote yakua unga.

Kisha wanapaki kwenye viroba na KISHA WANANILIPA CHANGU kwa Kila kilo ya unga iliyopatikana Na kuyasafirisha kwenye ndege.

Nikaja nikamdokeza iyo fursa Binamu yangu mmoja Alkua anaishi maisha ya tabu sana.
Lengo lilikua tuunganishe Nguvu, niweze kukusanya mzigo wa kutosha FAIDA iwe kubwa.

Na nkajitolea siku moja naenda kuchukua mzigo nkaenda nae kabisa,
Siku nakabidhiwa malipo yangu, mchakato mzima anauonana KABISA.

Alichokifanya,
Akaanza kuhangaika kuomba omba mitaji kwa ndugu na watu wengine.

Nkashangaa kwny grup la familia,
Katibu wetu kaanzisha Uzi na anaomba wanafamilia wote wamchangie ndugu yetu afanikishe iyo project yake.

Siku sio nyingi nkaanza kuona watu wananifatilia,

Mara niamshwe usiku usiku, polisi wamekuja kunikagua nyumbani.

Nkiendesha usiku, Mara polisi wenye pikipiki wanisimamishe kunikagua.

Mara niitwe na

Nikakamatwa nikihisiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.

Polisi, ananihoji eti Kuna miti huwa nasaga nasafirisha unga unga.
Nimweleze uwo unga unakazi gani.

Nikakana Kila kitu,
Walinishikilia siku 3.

Yaani ilkua Ni usumbuf JUU usumbufu.

Baadae,
Kule nlikokua nanunua mzigo, wakaanza kunitilia mashaka Kila nkija kununua mzigo.

Mara waanze kunihoji hoji maswali hayana kichwa Wala miguu.

Siku sio nyingi,
Wale wazungu wakaja kuchukua mzigo Kama kawaida,

Baadae nkaja kuskia wamedakwa na polisi usiku airport wakipakia mzigo kwny ndege.

Taarifa zikaenea kua ule unga ulkua inachanganywa na vitu vingine kutengeneza Aina flani ya dawa za kulevya.

Nkaona isiwe tabu,
Nkahama ule mkoa haraka sana na NAMBA ya SIMU nkabadilisha kabisa.

Nkafunga mawasiliano na ndugu na wanafamilia wote.

Almost 2yrs,
Ule upepo ulipopoa ndo nkarejea kwny maisha ya kawaida.

NAJUTA KABISA.
 
 


Hahahhaha
 
uliku mti gani uo au kam kuna picha ingependeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…