Elijah O
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,118
- 916
Ungesoma kidogo kidogo uambulieamo
Mwenzio nachoka kusoma nyuzi ndefu ujue!! Huwezi samaraizi??? Aaraaaaahh....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenzio nachoka kusoma nyuzi ndefu ujue!! Huwezi samaraizi??? Aaraaaaahh....
fedha na dhahabu ni Mali ya Bwana Mungu umpa ampendae . sio siri. utajiri wa siri ni washetani hata shetani ni tajiri sana . je? wewe unaongelea utajiri gani? kweli utajiri wa shetani ni siri kubwa uwa mama au mtoto au watoto , kuvunja na kupora na kuua. wizi wa mali mbali mbali na ujambazi kisha ukawa tajiri ndio Maana matajiri wengi na utajiri ni siri kubwa wakikueleza unaweza kuzimia au kufa kabisa.
Ungesoma kidogo kidogo uambulieamo
Asante.
Amesema ni siri unataka atoe siri so atakua maskini.Mkuu hapa duniani Kuna mambo mengi Sanaa tumelishwa na mpaka leo yamekua kizungumkuti kwa fact hyo hiyo ya kusema "we amini hivo"...
Sasa na ww naomba usipite humo humo katika kuweka njia panda...unless ungeamua tu huu Uzi kubaki nao kichwani....lakini as long as umeamua kuleta elimu ya kututoa kwenye giza kutuleta kwnye mwanga then you must be at list a lillte bit open.......
Funguka hata kwa uchache tu au kwa juu juu tu.......tell us ni watu gani hao and how do they know our tomorrow's
wewe umefikiria siri za kupata utajiri ni siri . ila hujafikiria njia wanazopita Matajiri zikoje na kwanini ? ni siri kubwa nadhani mtoa Mada ni kijana bado mimi ni mzee miaka 64 sasa nyani mzee amekwepa Mishale Mingi. Pia nina Maisha Mazuri sana ila si tajiri . achana na siri ya Mtu tajiri . kwa Mungu hakuna siri . Mungu anampa ampendae utajiri sio kwa siri . hata wewe unae soma ujumbe huu Mungu akupe utajiri kwa Mapenzi yake . siri kwa siri Anae toa kwa siri ni shetani kwa sababu njia zake si halali
Mzee tununue kitabu tusome kuwa matajiri???
izo namba za simu hapo chini nizanini?Utajiri hausomwi kwenye vitabu, wewe uliona wapi siri zikawekwa vitabuni na kuuzwa
Umasikini pia hausomwi kwenye vitabu pia
Matjiri wala hawaongei sana kam wewe.Ndio haya maswali ya masikini yanavyokuwaga,
Wewe hata nikiwa tajiri unafikiri itakusaidia?
Nashukuru mfano bora umejitokeza, na wewe utakuwa Case Study humu Jamvini
Utajiri ni Siri,Wewe ni tajiri?
Tuanzie kwanza hapo.
Mkuu hii comment yako imekaa km unapita route za nyuma ya airport (mpalange)Mwenzio nachoka kusoma nyuzi ndefu ujue!! Huwezi samaraizi??? Aaraaaaahh....
Yeah nilikutana na jamaa mmoja ni tajiri sana ila yeye hapendi kabisa kuitwa hivyo, anasema yeye ni mtu aliyefanikiwa na si tajiri!Tajiri hawezi kujiita tajiri,
Utajiri hauna mdomo, una vitendo, nimeshaandika hapo.
Mkuu mbona unanitisha sana na hawa nduguKisa kingine,
Miaka ya nyuma, nlipata mchongo na wazungu flani.
Ilkua biashara ya kununua magogo Aina flani ya miti kutoka kusini
yanakusanywa, kontena likijaa nawataarifu
Wanakuja na mashine yao, wanayasaga saga mogogo yote yakua unga.
Kisha wanapaki kwenye viroba na KISHA WANANILIPA CHANGU kwa Kila kilo ya unga iliyopatikana Na kuyasafirisha kwenye ndege.
Nikaja nikamdokeza iyo fursa Binamu yangu mmoja Alkua anaishi maisha ya tabu sana.
Lengo lilikua tuunganishe Nguvu, niweze kukusanya mzigo wa kutosha FAIDA iwe kubwa.
Na nkajitolea siku moja naenda kuchukua mzigo nkaenda nae kabisa,
Siku nakabidhiwa malipo yangu, mchakato mzima anauonana KABISA.
Alichokifanya,
Akaanza kuhangaika kuomba omba mitaji kwa ndugu na watu wengine.
Nkashangaa kwny grup la familia,
Katibu wetu kaanzisha Uzi na anaomba wanafamilia wote wamchangie ndugu yetu afanikishe iyo project yake.
Siku sio nyingi nkaanza kuona watu wananifatilia,
Mara niamshwe usiku usiku, polisi wamekuja kunikagua nyumbani.
Nkiendesha usiku, Mara polisi wenye pikipiki wanisimamishe kunikagua.
Mara niitwe na
Nikakamatwa nikihisiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Polisi, ananihoji eti Kuna miti huwa nasaga nasafirisha unga unga.
Nimweleze uwo unga unakazi gani.
Nikakana Kila kitu,
Walinishikilia siku 3.
Yaani ilkua Ni usumbuf JUU usumbufu.
Baadae,
Kule nlikokua nanunua mzigo, wakaanza kunitilia mashaka Kila nkija kununua mzigo.
Mara waanze kunihoji hoji maswali hayana kichwa Wala miguu.
Siku sio nyingi,
Wale wazungu wakaja kuchukua mzigo Kama kawaida,
Baadae nkaja kuskia wamedakwa na polisi usiku airport wakipakia mzigo kwny ndege.
Taarifa zikaenea kua ule unga ulkua inachanganywa na vitu vingine kutengeneza Aina flani ya dawa za kulevya.
Nkaona isiwe tabu,
Nkahama ule mkoa haraka sana na NAMBA ya SIMU nkabadilisha kabisa.
Nkafunga mawasiliano na ndugu na wanafamilia wote.
Almost 2yrs,
Ule upepo ulipopoa ndo nkarejea kwny maisha ya kawaida.
NAJUTA KABISA.