Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe

Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe

Mm ninaomba mnisaidie tajiri hasa ni nani? Maana kila level utakayo ifikia bado utaitaji uongeze ili uingie nafas nyingine na kwa mwanadamu hawez limit matamanio yake hiyo ni nature, sasa masikini ni nani na tajiri ni nani?
 
Mkuu hapa duniani Kuna mambo mengi Sanaa tumelishwa na mpaka leo yamekua kizungumkuti kwa fact hyo hiyo ya kusema "we amini hivo"...

Sasa na ww naomba usipite humo humo katika kuweka njia panda...unless ungeamua tu huu Uzi kubaki nao kichwani....lakini as long as umeamua kuleta elimu ya kututoa kwenye giza kutuleta kwnye mwanga then you must be at list a lillte bit open.......

Funguka hata kwa uchache tu au kwa juu juu tu.......tell us ni watu gani hao and how do they know our tomorrow's
Kweli kabisa Mana kutuficha hakutusaidii kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapa duniani Kuna mambo mengi Sanaa tumelishwa na mpaka leo yamekua kizungumkuti kwa fact hyo hiyo ya kusema "we amini hivo"...

Sasa na ww naomba usipite humo humo katika kuweka njia panda...unless ungeamua tu huu Uzi kubaki nao kichwani....lakini as long as umeamua kuleta elimu ya kututoa kwenye giza kutuleta kwnye mwanga then you must be at list a lillte bit open.......

Funguka hata kwa uchache tu au kwa juu juu tu.......tell us ni watu gani hao and how do they know our tomorrow's
Ushaambiwa ni siri tena kubwa mno sio rahisi kuambiwa na kuna mambo watu wanayasema pale tu wanapokaribia kufa wanaojua husema huyu kabakiza muda mchache Hapa duniani.

Mfano kuna watu wanaacha kazi na anapata kazi ingine muda huo huo inafika pahali mtu anaweza kuiamrisha Dunia impe anachotaka na Dunia inamtii. Mtu anakuja ofisini kwenu kuomba kazi anaambiwa nafasi hakuna haipiti muda mtu anaachishwa ama anaacha kazi kwa kuamua alafu yeye anaitwa kazini.
Katika siri kuna siri KUU. Kitu ambacho unaweza kuwa hufahamu kujua siri haina manufaa kwako Kama huna uwezo wakuitumia ikakusaidia unakuwa huna tofauti na asiyefahamu. Siri ni uwezo,hali, kitu, Taarifa na Inawezekana mwenye siri akawa hajui Kama inapaswa kuwa siri ila inatokea tu haisemi na siku akitaka kuisema kadri anavozidi kuisema akili inamfunguka na kumpa mtetemo tofauti na kuacha kuisema inavotakikana Hapa namaanisha asili/Nature pia Inaweza kumzuia mtu asiseme siri fulani.

Because of time confusion let's me stop here
 
kuna watu hawana siri ni wawazi na wakweli na uwazi wao uliwapatia utajiri Mkubwa . kuna vitu vitatu ukitaka kufanikiwa maishani Uwe Mwaminifu sana, uwe kweli, uwe Msikivu na Mnyenyekevu. uwe na bidii na juhudi na Maarifa. Mtangulize Mungu kwa kila kitu .
Mbona vingi mkuu,ulisema vitu vitatu ?
 
Motivational Speakers inategemea ni yupi,,mfano marehemu mzee Mengi,Mzee Bakhresa hao wakiku motivate wasikilize because they mean it fully

Hata wao hawawez kukwambia kila kitu how they got where they are , watakwambia tu vitu basic ambavyo tumewah kuvisikia
 
Umeongea ukwel mtu, sasa mm naingia kweny izo sifa za utajir ila bdo kapuku. "Apo kwenyvkuongea na mtu mpk anaondoka sijui kavaa nguo ya rangi gani uyo ni mm mtupu aise" mpka nikahisigi nina kauzembe cha ku focuse au naweza onana na mtu ata mara mbili ila nisimkariri sura. Au mtu anaweza niuliza iv umeongea na mtu flan leo nikamjibu hpna baada ya muda namjibu ee nimeongea nae kumbe nishapoteza, nikiulizwa amesema dah apo sasa ndio mtihan km tulivyozungumza havikuwa na mantiki nitakumbuka viwili tu dah
 
Daaahh noma Sanaa hili darasa....ila hiyo paragraph ya nne unless uwe umemaanisha Mungu, lakini Kama umemaanisha Kuna binadamu wanajua mpaka kesho yetu Basi naomba ufafanue vizuri tena kwa umakini mkubwa mnoo
Yuko sahihi. Hela za utajiri mkubwa zina mikataba ambayo baadhi ya masharti yake ni kifo baada ya muda fulani au kuua kila baada ya muda fulani.
Kuna jamaa yangu alijaribu utajiri huo kwa kutaka kumwua nduguye. Kwa bahati mbaya siri ilivuja kwa kusemwa na mgonjwa baada ya kufanyiwa maombi. Hadi leo amebaki vilevile kama siyo kushuka kiuchumi. Dunia ina Siri nyingi.
 
Mkuu hapa duniani Kuna mambo mengi Sanaa tumelishwa na mpaka leo yamekua kizungumkuti kwa fact hyo hiyo ya kusema "we amini hivo"...

Sasa na ww naomba usipite humo humo katika kuweka njia panda...unless ungeamua tu huu Uzi kubaki nao kichwani....lakini as long as umeamua kuleta elimu ya kututoa kwenye giza kutuleta kwnye mwanga then you must be at list a lillte bit open.......

Funguka hata kwa uchache tu au kwa juu juu tu.......tell us ni watu gani hao and how do they know our tomorrow's
Naweza kumuunga mkono mweny hoja sababu mm nishawahi kufanya kaz kampuni flan iv ya boss wa kihindi baada ya kuondoka ndio nilikuja kufaham fununu za yule boss, kwamba ukija kabla ya kukuajir lazma akuangalie ung'aaji wa nyota yako kwa sangoma wake. Nilivyoambiwaa na mtu wake wa karb kuwa mm nilivyoenda pale nilionekana ni angavu sana tena akaambiwa awe makini na mm nikifanya mda mrefu pale kaz nitapendwa kupitwa ata yeye na naweza kuwa mkubwa kupita yeye kwahyo ikofikia iko kipindi asiniruhusu niondoke pale..kwahyo nikapigwa pini niwe mtu wa yes tuu nitumiwe. Popote nilipokuwaa naomba kaz sipati kuna sehm nilienda nikafaulu kila kitu mpka kesho natakiwa niitwe kazn waajiri wakasahau mpaka position yng ikapata mtu mwingne. Kwahyo hiv vitu kuwa mtu anajua kesho yako ni kwel aise dunia ina mambo mengi sana
 
UTAJIRI NI SIRI, NA SIRI NDIO UTAJIRI WENYEWE

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Kabla hujaanza kutafuta utajiri, basi kwanza kabisa jifunze kuwa na Siri. Huwezi kutafuta utajiri kama huna siri, na kamwe huwezi pata utajiri kama wewe sio mtu wa Siri.

Huwezi pewa nafasi nyeti, nafasi kubwa kama wewe sio mtu wa siri, Siri ndio utajiri wenyewe, siri ndio nguvu, uwezo, na kila kitu katika dunia ya mafanikio.

Huwezi kuwa nabii mkubwa, mchawi nguli, mganga aliyeshindikana, kama huna siri. Ili uwe katika Rank za juu kabisa zaa utajiri ni lazima uwe na siri kubwa, hata ukamatwe uchapwe, uminywe kende, uchomwe na kuchinjwa, bado usiwe mwepesi kuongea mambo yasiyostahili kusemwa.

Amin amin nakumbia, katika hii dunia kuna watu wanajua mpaka siku yako ya kufa lakini kamwe hawawezi kukuambia, kuna watu wanajua kabisa kesho utapata ajali ya Bodaboda lakini hawawezi kukuambia, amini kuna watu wanajua kabisa kesho unaenda kutusua mapesa wakati wewe hujui, lakini hawezi kukuambia.

Watu waliofanikiwa wote duniani kwa ngazi za juu ni watu wa siri, Manabii wote unaowajua na usiowajua wote walikuwa watu wa siri. Wachawi nguli, waganga wa level za juu kabisa ni watu wa siri, kamwe hawawezi kukwambia kitu.

Watu husema dunia haina siri, lakini nakuambia Dunia ina siri nyingi mno,, na siri hizo zinashikiliwa na watu wenye siri.

Utajiri ni Siri kwa sababu yeye aliyetajiri namba moja ambaye ni Mungu mwenyewe, Yeye ni SIRI, hakuna anayemjua na hataki ajulikane. Ila wenye siri amejifunua kwao.

Mungu hapendi mtu kiropo ropo, mtu asiye na Siri kamwe hawezi kuwa karibu na Mungu, kamwe hawezi kuwa Tajiri. Hii inatumika hata kwa Shetani, mtu asiye na siri kamwe hawezi kuwa karibu na Shetani, na huwezi kuwa karibu na hao alafu usiwe tajiri.

Mipango ya utajiri haisemwi na watu wenye siri, wao hutekeleza na inakuwa, lakini mipango inayosemwa kabla haijatekelezwa hiyo kwa asilimia kubwa zaidi ya 95% haiwezi kutekelezeka.

Utajiri ni siri, Utajiri umejificha, Utajiri hupenda watu wenye tabia ya kujifichaa, kutokujionyesha kutokupenda sifa za kijinga jinga.

Ukiona mtu anasema ni tajiri basi jua huyo sio Tajiri, utajiri hauna mdomo bali unavitendo.

Ukiona mtu anakuahidi sana jua hapo utekelezaji ni sifuri, utajiri hauna maneno bali mdomo.

Utajiri ummejificha
Madini na vito vya thamani vimejificha, huwezi ikuta imezagaa zagaa mtaani.

Hata kwenye serikali za dunia, kuna vitengo ndani ya nchi hutakiwa kupewa watu wenye siri sana.
Huwezi pewa wewe mwenzangu na miye kiropo ropo, kila kitu unataka watu wajue, kabla hujafanya unatangaza, ukifeli kukifanya unasingizia umelogwa wakati wewe ndio umejiloga.

Utajiri hauna mdomo, utajiri una vitendo tuu.

Utajiri sio imani, utajiri ni hulka, asili ya mtu, silika ya mtu. Huwezi ukawa tajiri kama huna hulka, asili na silika ya utajiri.

Utajiri sio bahati, utajiri ni jambo la lazima kwa watu wenye asili ya utajiri.
Kama ilivyo kwa umasikini
Umasikini hauji kwa bahati, umasikini ni jambo la lazima kwa watu wenye hulka na asili ya umasikini.

Utajiri unahitaji Usiri
Umasikini unahitaji uwazi
Utajiri unahitaji sheria nyingi
Umasikini unahitaji maisha ya hivi hivi, bila sheria

Utajiri unahitaji Mipango, na kujali kizazi kijacho
Umasikini hauhitaji mipango, haujali kizazi kijacho.

Utajiri una aibu ya kushindwa
Umasikini hauna aibu ya kushindwa
Utajiri hauna visingizio au lawama
Umasikini una Visingizio na lawama.

Utajiri haupendi marafiki wengi
Umasikini unapenda marafiki wengi.

Tajiri hapendi marafiki wengi na ikiwezekana matajiri wengi hawana marafiki bali jamaa tuu.
Lakini Masikini hupenda marafiki wengi, sio rahisi masikini akose rafiki.

Watu hujipendekeza kwa watu matajiri lakini matajiri huwachomolea mbali.
Lakini masikini ndio hujipendekeza kwa watu ili kupata marafiki wengi.

Mtu yeyote mwenye rafiki wengi ni ishara ya unafiki. Watu wenye unafiki ndio huwa na marafiki wengi.
Lakini sio rahisi kwa tajiri kuwa na marafiki wengi, matajiri wengi sio wanafiki, kama hakutaki atakuambia hakutaki, kama hataki kukusaidia atakuambia hataki kukusaidia.

Utajiri ni Siri, na siri ndio utajiri wenyewe.

Tajiri hapendi aonekane anapesa, au anamali hiyo ni moja ya sifa kuu ya tajiri, hata Mungu aliyetajiri namba moja hujifanya hana utajiri na mara nyingi hutenda katika dakika za mwisho.

Masikini hupenda aonekane naye yumo, naye anapesa, anamali, hivyo hujifanya anavaa vizuri ili aheshimike yaani anajidanganya kuwa ana pesa kumbe hana.

Ukiona unatabia ya kutaka kuonekana unapesa, unamali, una nguvu, una uwezo mbele za watu basi jua wewe ni masikini, unahaiba, huika na asili ya masikini.

Ndio maana kuna msemo wa masikini usemao " Mavazi huficha umasikini" Huo ni msemo wa watu masikini, tajiri hashughuliki na mavazi yako, masikini wenzako ndio watashughulika na mavazi yako. Tajiri hafuatilii maisha ya mtu,

Unaweza kukutana na tajiri mkazungumza hata masaa matatu alafu ukaondoka, asijue ulivaa nguo ya rangi gani, ukiona unatabia ya hivi ujue wewe una hulka ya utajiri. Lakini ukiona mtu anaongea na wewe hata dakika tano alafu ukaachana naye, akaja mwingine akakuuliza fulani alikuja hapa ulimuona, wewe ukajibu ndio,; tena nimeongea naye, alikuwa kavaa nguo za rangi hii, na viatu vya namna hii, na pembeni kumechanika, jua wewe upo kundi la masikini.

Masikini huangalia mambo madogo, tajiri hana muda huo;

Unataka kununua kiwanja, unasema, utasubiri sana.
Unataka kuoa au kuolewa unasema, Utasubiri sana
Unataka kuanzisha mradi, unasem, Utasubiri miaka nenda rudi.
Unatafuta kazi au kujiajiri, unasema, utasota mpaka ushangae
Unataka kununua gari, unasema, utatembea soli kama mdudu miaka nenda rudi.

Na kikawaida jamii masikini na watu masikini ndio huwa na tabia ya kusema au kuuliza maswali hayo.
Unakuta mtu hata hamna undugu, anakuuliza;
Vipi unaoa au unaolewa lini?
Utafikiri yeye ni mchungaji ndiye atafungisha.
Utasikia vipi hujapata kazi au ajira?
Utafikiri yeye anayo hiyo ajira, au anataka kukuajiri. Masikini ni wanafiki, wanachotafuta ni habari ya kusema.

Utasikia, vipi mumeo au mkeo hakusumbui?
Mjibu, njoo nikuoe wewe, ili usiwe unaniuliza maswali ya kipumbavu, hata kama ni mtu mzima mjibu hivyo ili akome umbeya.

Utasikia, mpaka sasa huna hata mtoto jamani?
Mjibu, njoo nikuzalishe, kenge wewe.

Sasa unakuta wapenda sifa wakiulizwa maswalli hayo ya kinafiki na watu wasio na msaada wowote kwao, kwa vile wanapenda sifa, nao wanajaa.
Utasikia ooh! Tayari nimeshanunua kiwanja, mwakani namwaga mawe ya msingi, alafu mwezi wa kumi nitaoa au kuolewa. Wewe ni mpumbavu.
Unamjibu yeye, kwani atakusaidia nini, au atachangia nini kama sio unatafuta kukwama.

Mwisho, utajiri wa jambo lolote ile ni siri, na siri ndio utajiri wenyewe.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
Mleta mada yupo sahihi kabisa, sina shaka na alichokisema , Matajiri sio watu wa kuzungumza zungumza ovyo, pia hufanya mambo yao kwa usiri sana . Hilo nimelishuhudia mwenyewe na nimelifanyia kazi pia.
 
Nashkuru kwa kunithibitishia mambo flan yalokua yananipa shida na kunikwamisha maana toka nianze kuwa msiri kwenye mikakati yangu basi naona Mungu anafungua njia.

Kwakwel 35% ya uloongea yana ukwel na yamenihusu.

Mengine sio halis sana au pengine hayajanihusu wala sijayakubali.

Ubarikiwe sana kwa nondo hii nzuri
 
Back
Top Bottom