DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
Hanna watu wabaya Kama ndugu, HATA kufungiana rizki na kurogana.Mkuu mbona unanitisha sana na hawa ndugu
Utakuta miongoni mwa ndugu yako ndo anakulostisha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hanna watu wabaya Kama ndugu, HATA kufungiana rizki na kurogana.Mkuu mbona unanitisha sana na hawa ndugu
[emoji110][emoji109][emoji106] well saidKwa Mungu hakuna Siri? Mzee wangu unajua hata maana ya Mungu?
Unapoambiwa Mungu aliyesirini unaelewa nini/
Unasema hakuna siri kwa Mungu,
Unajua kwa nini mpaka sasa hakuna aliyewahi kumuona Mungu?
Unasema hakuna Siri kwa Mungu, mzee acha hizo bhana.
Unajua siku yako ya kufa?
Unajua siku ya mtu kufanikiwa au kuanguka?
Unajua kwa nini Mungu ameficha mawazo ya mtu na mtu, yaani wewe ukifikiria mimi sijui, nami nikifikiria nawe hujui? Unajua maana yake hivyo?
Unasema hakuna siri kwa Mungu kana kwamba kesho unaijua,
Kesho ni muhimu kwa sababu hatuijui, kesho ni siri na walio nayo ni wale wenye siri hiyo.
Kwa Mungu kuna siri nyingi kuliko kwa shetani,
Mungu bila siri hawezi kuwa Mungu,
Kusema kwa Mungu hakuna siri tafsiri yake ni kuwa Mungu hana thamani tena
Mmmh mpaka nimeogopa sana mkuu!Hanna watu wabaya Kama ndugu, HATA kufungiana rizki na kurogana.
Utakuta miongoni mwa ndugu yako ndo anakulostisha.
Kwani mpumbavu Ni lugha mbaya ? Upumbavu Ni level ya chini kabisa ukipita ujinga. Nimemkumbusha atoke huko kwenye upumbavu aje kwenye ujinga halafu awe mwerevu.Huwezi kutumia lugha nzuri mpaka umuite mpumbavu?
Kasema ana miaka 64 kwanini huna heshima[emoji848]
Bado sijakariri mkuu.Utajiri ni Siri,
Umesahau mara hii,?
'Matjiri wala hawaongei sana kam wewe.'Matjiri wala hawaongei sana kam wewe.
Vilevile sio kweli kuwa matajiri hawana marafiki wengi,akina Ginimbi si uliwaona wewe!
Kabisa kabisa ndio maana mimi baadhi ya mambo huwa sisemi lakini ninayo mfano watu wengi wanaonifahamu wanajua nina watoto 2 tu wanaowajua lakini kiukweli nina utajiri wa watoto 5 sasa na watu Hawajui mimi kimya watakuja nakushangaa tu hapo baadae mimi nakula matunda ya kuzaa...Yes ndio watoto nao ni utajiri asiyetaka alale mbere kwanza maendeleo hayana vyama...UTAJIRI NI SIRI, NA SIRI NDIO UTAJIRI WENYEWE
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Kabla hujaanza kutafuta utajiri, basi kwanza kabisa jifunze kuwa na Siri. Huwezi kutafuta utajiri kama huna siri, na kamwe huwezi pata utajiri kama wewe sio mtu wa Siri.
Huwezi pewa nafasi nyeti, nafasi kubwa kama wewe sio mtu wa siri, Siri ndio utajiri wenyewe, siri ndio nguvu, uwezo, na kila kitu katika dunia ya mafanikio.
Huwezi kuwa nabii mkubwa, mchawi nguli, mganga aliyeshindikana, kama huna siri. Ili uwe katika Rank za juu kabisa zaa utajiri ni lazima uwe na siri kubwa, hata ukamatwe uchapwe, uminywe kende, uchomwe na kuchinjwa, bado usiwe mwepesi kuongea mambo yasiyostahili kusemwa.
Amin amin nakumbia, katika hii dunia kuna watu wanajua mpaka siku yako ya kufa lakini kamwe hawawezi kukuambia, kuna watu wanajua kabisa kesho utapata ajali ya Bodaboda lakini hawawezi kukuambia, amini kuna watu wanajua kabisa kesho unaenda kutusua mapesa wakati wewe hujui, lakini hawezi kukuambia.
Watu waliofanikiwa wote duniani kwa ngazi za juu ni watu wa siri, Manabii wote unaowajua na usiowajua wote walikuwa watu wa siri. Wachawi nguli, waganga wa level za juu kabisa ni watu wa siri, kamwe hawawezi kukwambia kitu.
Watu husema dunia haina siri, lakini nakuambia Dunia ina siri nyingi mno,, na siri hizo zinashikiliwa na watu wenye siri.
Utajiri ni Siri kwa sababu yeye aliyetajiri namba moja ambaye ni Mungu mwenyewe, Yeye ni SIRI, hakuna anayemjua na hataki ajulikane. Ila wenye siri amejifunua kwao.
Mungu hapendi mtu kiropo ropo, mtu asiye na Siri kamwe hawezi kuwa karibu na Mungu, kamwe hawezi kuwa Tajiri. Hii inatumika hata kwa Shetani, mtu asiye na siri kamwe hawezi kuwa karibu na Shetani, na huwezi kuwa karibu na hao alafu usiwe tajiri.
Mipango ya utajiri haisemwi na watu wenye siri, wao hutekeleza na inakuwa, lakini mipango inayosemwa kabla haijatekelezwa hiyo kwa asilimia kubwa zaidi ya 95% haiwezi kutekelezeka.
Utajiri ni siri, Utajiri umejificha, Utajiri hupenda watu wenye tabia ya kujifichaa, kutokujionyesha kutokupenda sifa za kijinga jinga.
Ukiona mtu anasema ni tajiri basi jua huyo sio Tajiri, utajiri hauna mdomo bali unavitendo.
Ukiona mtu anakuahidi sana jua hapo utekelezaji ni sifuri, utajiri hauna maneno bali mdomo.
Utajiri ummejificha
Madini na vito vya thamani vimejificha, huwezi ikuta imezagaa zagaa mtaani.
Hata kwenye serikali za dunia, kuna vitengo ndani ya nchi hutakiwa kupewa watu wenye siri sana.
Huwezi pewa wewe mwenzangu na miye kiropo ropo, kila kitu unataka watu wajue, kabla hujafanya unatangaza, ukifeli kukifanya unasingizia umelogwa wakati wewe ndio umejiloga.
Utajiri hauna mdomo, utajiri una vitendo tuu.
Utajiri sio imani, utajiri ni hulka, asili ya mtu, silika ya mtu. Huwezi ukawa tajiri kama huna hulka, asili na silika ya utajiri.
Utajiri sio bahati, utajiri ni jambo la lazima kwa watu wenye asili ya utajiri.
Kama ilivyo kwa umasikini
Umasikini hauji kwa bahati, umasikini ni jambo la lazima kwa watu wenye hulka na asili ya umasikini.
Utajiri unahitaji Usiri
Umasikini unahitaji uwazi
Utajiri unahitaji sheria nyingi
Umasikini unahitaji maisha ya hivi hivi, bila sheria
Utajiri unahitaji Mipango, na kujali kizazi kijacho
Umasikini hauhitaji mipango, haujali kizazi kijacho.
Utajiri una aibu ya kushindwa
Umasikini hauna aibu ya kushindwa
Utajiri hauna visingizio au lawama
Umasikini una Visingizio na lawama.
Utajiri haupendi marafiki wengi
Umasikini unapenda marafiki wengi.
Tajiri hapendi marafiki wengi na ikiwezekana matajiri wengi hawana marafiki bali jamaa tuu.
Lakini Masikini hupenda marafiki wengi, sio rahisi masikini akose rafiki.
Watu hujipendekeza kwa watu matajiri lakini matajiri huwachomolea mbali.
Lakini masikini ndio hujipendekeza kwa watu ili kupata marafiki wengi.
Mtu yeyote mwenye rafiki wengi ni ishara ya unafiki. Watu wenye unafiki ndio huwa na marafiki wengi.
Lakini sio rahisi kwa tajiri kuwa na marafiki wengi, matajiri wengi sio wanafiki, kama hakutaki atakuambia hakutaki, kama hataki kukusaidia atakuambia hataki kukusaidia.
Utajiri ni Siri, na siri ndio utajiri wenyewe.
Tajiri hapendi aonekane anapesa, au anamali hiyo ni moja ya sifa kuu ya tajiri, hata Mungu aliyetajiri namba moja hujifanya hana utajiri na mara nyingi hutenda katika dakika za mwisho.
Masikini hupenda aonekane naye yumo, naye anapesa, anamali, hivyo hujifanya anavaa vizuri ili aheshimike yaani anajidanganya kuwa ana pesa kumbe hana.
Ukiona unatabia ya kutaka kuonekana unapesa, unamali, una nguvu, una uwezo mbele za watu basi jua wewe ni masikini, unahaiba, huika na asili ya masikini.
Ndio maana kuna msemo wa masikini usemao " Mavazi huficha umasikini" Huo ni msemo wa watu masikini, tajiri hashughuliki na mavazi yako, masikini wenzako ndio watashughulika na mavazi yako. Tajiri hafuatilii maisha ya mtu,
Unaweza kukutana na tajiri mkazungumza hata masaa matatu alafu ukaondoka, asijue ulivaa nguo ya rangi gani, ukiona unatabia ya hivi ujue wewe una hulka ya utajiri. Lakini ukiona mtu anaongea na wewe hata dakika tano alafu ukaachana naye, akaja mwingine akakuuliza fulani alikuja hapa ulimuona, wewe ukajibu ndio,; tena nimeongea naye, alikuwa kavaa nguo za rangi hii, na viatu vya namna hii, na pembeni kumechanika, jua wewe upo kundi la masikini.
Masikini huangalia mambo madogo, tajiri hana muda huo;
Unataka kununua kiwanja, unasema, utasubiri sana.
Unataka kuoa au kuolewa unasema, Utasubiri sana
Unataka kuanzisha mradi, unasem, Utasubiri miaka nenda rudi.
Unatafuta kazi au kujiajiri, unasema, utasota mpaka ushangae
Unataka kununua gari, unasema, utatembea soli kama mdudu miaka nenda rudi.
Na kikawaida jamii masikini na watu masikini ndio huwa na tabia ya kusema au kuuliza maswali hayo.
Unakuta mtu hata hamna undugu, anakuuliza;
Vipi unaoa au unaolewa lini?
Utafikiri yeye ni mchungaji ndiye atafungisha.
Utasikia vipi hujapata kazi au ajira?
Utafikiri yeye anayo hiyo ajira, au anataka kukuajiri. Masikini ni wanafiki, wanachotafuta ni habari ya kusema.
Utasikia, vipi mumeo au mkeo hakusumbui?
Mjibu, njoo nikuoe wewe, ili usiwe unaniuliza maswali ya kipumbavu, hata kama ni mtu mzima mjibu hivyo ili akome umbeya.
Utasikia, mpaka sasa huna hata mtoto jamani?
Mjibu, njoo nikuzalishe, kenge wewe.
Sasa unakuta wapenda sifa wakiulizwa maswalli hayo ya kinafiki na watu wasio na msaada wowote kwao, kwa vile wanapenda sifa, nao wanajaa.
Utasikia ooh! Tayari nimeshanunua kiwanja, mwakani namwaga mawe ya msingi, alafu mwezi wa kumi nitaoa au kuolewa. Wewe ni mpumbavu.
Unamjibu yeye, kwani atakusaidia nini, au atachangia nini kama sio unatafuta kukwama.
Mwisho, utajiri wa jambo lolote ile ni siri, na siri ndio utajiri wenyewe.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
Motivational Speakers inategemea ni yupi,,mfano marehemu mzee Mengi,Mzee Bakhresa hao wakiku motivate wasikilize because they mean it fullyMaskini hawezi kunishauri bwn Mdogo.
Motivational Speaker ni shiiiiiiiida.
Huruma unamuonea mtu yuko na vita vya kiafya,kiakili au tuseme ana personal issues zinam face ambazo zinaweza kumpelekea akawa weak au aka demise kabisa.Lakini kwenye every aspect ambazo zina involve competition kama business,kazi hapo kuna creativity kazini,promotion na vitu kama hizo zinahusu chapaa,rizki,ngawila huwa ni siri ndio maana matajiri hawatoi siri.Ntachangia kwa mfano hai,
Kuna jamaa angu, Tunafanya biashara eneo moja.
alnifata kuniomba nimsaidie chimbo la bidhaa flani maana kwa bei anayonunua (sh.850) na Bei ya kuuzia sokoni (sh1000) hamlipi kabisa.
Nkamuonea huruma nkampa chimbo la kununua sh. Sh.220 ili akauze ile ile sh.1000
Baada ya wiki
Mteja anauliza Bei gan hii, unamwambia Elfu moja.
Anakujibu, Mbona flani pale anauza jero jero.
Mfanyabiashara mwenzang mwingine akaja ananiuliza,
Aisee Jamaa anapata wapi mzigo, Pale kwake anauza jero jero rejareja.
Dah!
Nkajua tayar picha ishaungua.
Baada ya hapo,
Ile FAIDA kubwa nliokua naipata kwenye ile bidhaa ikapotea ivyo kabisa na mauzo yakashuka.
NLIJUTA SANA!
Nowdays,
NIMEKUA BANDIDU KABISA,
Kuna baadhi ya machimbo ya hela Hadi mke wangu wa ndoa au Ndugu wa damu sitaki ajue kabisa.
NAUNGA MKONO HOJA, uko sahii Sana mtoa mada
Umetoa tena siri aisee Sisi watu weusi tuna matatizo sanaKisa kingine,
Miaka ya nyuma, nlipata mchongo na wazungu flani.
Ilkua biashara ya kununua magogo Aina flani ya miti kutoka kusini
yanakusanywa, kontena likijaa nawataarifu
Wanakuja na mashine yao, wanayasaga saga mogogo yote yakua unga.
Kisha wanapaki kwenye viroba na KISHA WANANILIPA CHANGU kwa Kila kilo ya unga iliyopatikana Na kuyasafirisha kwenye ndege.
Nikaja nikamdokeza iyo fursa Binamu yangu mmoja Alkua anaishi maisha ya tabu sana.
Lengo lilikua tuunganishe Nguvu, niweze kukusanya mzigo wa kutosha FAIDA iwe kubwa.
Na nkajitolea siku moja naenda kuchukua mzigo nkaenda nae kabisa,
Siku nakabidhiwa malipo yangu, mchakato mzima anauonana KABISA.
Alichokifanya,
Akaanza kuhangaika kuomba omba mitaji kwa ndugu na watu wengine.
Nkashangaa kwny grup la familia,
Katibu wetu kaanzisha Uzi na anaomba wanafamilia wote wamchangie ndugu yetu afanikishe iyo project yake.
Siku sio nyingi nkaanza kuona watu wananifatilia,
Mara niamshwe usiku usiku, polisi wamekuja kunikagua nyumbani.
Nkiendesha usiku, Mara polisi wenye pikipiki wanisimamishe kunikagua.
Mara niitwe na
Nikakamatwa nikihisiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Polisi, ananihoji eti Kuna miti huwa nasaga nasafirisha unga unga.
Nimweleze uwo unga unakazi gani.
Nikakana Kila kitu,
Walinishikilia siku 3.
Yaani ilkua Ni usumbuf JUU usumbufu.
Baadae,
Kule nlikokua nanunua mzigo, wakaanza kunitilia mashaka Kila nkija kununua mzigo.
Mara waanze kunihoji hoji maswali hayana kichwa Wala miguu.
Siku sio nyingi,
Wale wazungu wakaja kuchukua mzigo Kama kawaida,
Baadae nkaja kuskia wamedakwa na polisi usiku airport wakipakia mzigo kwny ndege.
Taarifa zikaenea kua ule unga ulkua inachanganywa na vitu vingine kutengeneza Aina flani ya dawa za kulevya.
Nkaona isiwe tabu,
Nkahama ule mkoa haraka sana na NAMBA ya SIMU nkabadilisha kabisa.
Nkafunga mawasiliano na ndugu na wanafamilia wote.
Almost 2yrs,
Ule upepo ulipopoa ndo nkarejea kwny maisha ya kawaida.
NAJUTA KABISA.
Duh safi sana sio kwa sifa hizi aiseeHv we jamaa mpuuz unajua nakusoma SANA wewe. Keep it up, endelea kutuandikiwa Mkuu. Jinga SANA wewe
Mkuu kuna siri ambazo Mungu baba anajua lakini Yesu hajui.mfano siku ya kiama ,Yesu hajui ni liniHakuna siri ya utajiri au kuwa Msiri ndio utajiri . utajiri wa siri unatoka kwa shetani. Neno la Mungu linasema Mungu ndie akupae utajiri . soma kumbukumbu 8:18 Mungu ndiye atupae nguvu ya kupata utajiri Mungu akikupa hakuna cha siri . Matajiri wenye siri utajiri wengi wameupata kwa njia zisizo halali, wizi , dhuruma, kupora , kuua watu, ruswa na ufisadi. ndio maana utajiri wao ni siri. ila tajiri alie pewa na Mungu hakuna usiri soma kina Ibrahimu na selemani, na Ayubu ktk vitabu vya Mungu hakuna siri ktk utajiri wao.
Kwa iyo ana sound kama anapakuliwa sio?Mkuu hii comment yako imekaa km unapita route za nyuma ya airport (mpalange)
Hao nitawasikiliza mzee baba,ila shida nao wale hata muda wa kutoa ushauri walikua hawana.Motivational Speakers inategemea ni yupi,,mfano marehemu mzee Mengi,Mzee Bakhresa hao wakiku motivate wasikilize because they mean it fully
Basi si na wewe uache upumbavu na ujinga wako wa kudhania dhania na watu huwajui.Habithi mmoja.Kwani mpumbavu Ni lugha mbaya ? Upumbavu Ni level ya chini kabisa ukipita ujinga. Nimemkumbusha atoke huko kwenye upumbavu aje kwenye ujinga halafu awe mwerevu.
Hapa tunatumia anonymous account hatujuani umri, by the way unajuaje na Mimi Nina miaka zaidi ya 60 ?
Daah pole sna mkuu....ndugu noma sana hata me nataka niwe bandidu yahn mwakan hapo niwakatae kabisa!Kisa kingine,
Miaka ya nyuma, nlipata mchongo na wazungu flani.
Ilkua biashara ya kununua magogo Aina flani ya miti kutoka kusini
yanakusanywa, kontena likijaa nawataarifu
Wanakuja na mashine yao, wanayasaga saga mogogo yote yakua unga.
Kisha wanapaki kwenye viroba na KISHA WANANILIPA CHANGU kwa Kila kilo ya unga iliyopatikana Na kuyasafirisha kwenye ndege.
Nikaja nikamdokeza iyo fursa Binamu yangu mmoja Alkua anaishi maisha ya tabu sana.
Lengo lilikua tuunganishe Nguvu, niweze kukusanya mzigo wa kutosha FAIDA iwe kubwa.
Na nkajitolea siku moja naenda kuchukua mzigo nkaenda nae kabisa,
Siku nakabidhiwa malipo yangu, mchakato mzima anauonana KABISA.
Alichokifanya,
Akaanza kuhangaika kuomba omba mitaji kwa ndugu na watu wengine.
Nkashangaa kwny grup la familia,
Katibu wetu kaanzisha Uzi na anaomba wanafamilia wote wamchangie ndugu yetu afanikishe iyo project yake.
Siku sio nyingi nkaanza kuona watu wananifatilia,
Mara niamshwe usiku usiku, polisi wamekuja kunikagua nyumbani.
Nkiendesha usiku, Mara polisi wenye pikipiki wanisimamishe kunikagua.
Mara niitwe na
Nikakamatwa nikihisiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Polisi, ananihoji eti Kuna miti huwa nasaga nasafirisha unga unga.
Nimweleze uwo unga unakazi gani.
Nikakana Kila kitu,
Walinishikilia siku 3.
Yaani ilkua Ni usumbuf JUU usumbufu.
Baadae,
Kule nlikokua nanunua mzigo, wakaanza kunitilia mashaka Kila nkija kununua mzigo.
Mara waanze kunihoji hoji maswali hayana kichwa Wala miguu.
Siku sio nyingi,
Wale wazungu wakaja kuchukua mzigo Kama kawaida,
Baadae nkaja kuskia wamedakwa na polisi usiku airport wakipakia mzigo kwny ndege.
Taarifa zikaenea kua ule unga ulkua inachanganywa na vitu vingine kutengeneza Aina flani ya dawa za kulevya.
Nkaona isiwe tabu,
Nkahama ule mkoa haraka sana na NAMBA ya SIMU nkabadilisha kabisa.
Nkafunga mawasiliano na ndugu na wanafamilia wote.
Almost 2yrs,
Ule upepo ulipopoa ndo nkarejea kwny maisha ya kawaida.
NAJUTA KABISA.
Yale yale..... hata ukujua itakusaidia nini????Wewe ni tajiri?
Tuanzie kwanza hapo.