Utajiri ni Siri, na Siri ndio Utajiri wenyewe


Hata shetani humpa amtakaye, kwani wangapi wanaamini uchawi na uganga na bado ni masikini

Utajiri ni Siri, Ukiwa kiropo ropo hata usali mara elfu kwa Mungu hawezi kukupa utajiri kwa ukiropo ropo wako.

Mungu huwapa watu wenye siri, sio utajiri tuu hata akili, maarifa, ubunifu n.k
 
Ungesoma kidogo kidogo uambulieamo

Nimemuambia hata shuleni kuna walioishia darasa la pili, wala asijali, kila mmoja anakula urefu wa kamba yake.

Yeye asitake kwa vile kaishia la pili basi akadhani watu wote wanataka waishie la pili kama yeye
 
wewe umefikiria siri za kupata utajiri ni siri . ila hujafikiria njia wanazopita Matajiri zikoje na kwanini ? ni siri kubwa nadhani mtoa Mada ni kijana bado mimi ni mzee miaka 64 sasa nyani mzee amekwepa Mishale Mingi. Pia nina Maisha Mazuri sana ila si tajiri . achana na siri ya Mtu tajiri . kwa Mungu hakuna siri . Mungu anampa ampendae utajiri sio kwa siri . hata wewe unae soma ujumbe huu Mungu akupe utajiri kwa Mapenzi yake . siri kwa siri Anae toa kwa siri ni shetani kwa sababu njia zake si halali
 
Amesema ni siri unataka atoe siri so atakua maskini.
 

Kwa Mungu hakuna Siri? Mzee wangu unajua hata maana ya Mungu?
Unapoambiwa Mungu aliyesirini unaelewa nini/

Unasema hakuna siri kwa Mungu,
Unajua kwa nini mpaka sasa hakuna aliyewahi kumuona Mungu?
Unasema hakuna Siri kwa Mungu, mzee acha hizo bhana.

Unajua siku yako ya kufa?
Unajua siku ya mtu kufanikiwa au kuanguka?

Unajua kwa nini Mungu ameficha mawazo ya mtu na mtu, yaani wewe ukifikiria mimi sijui, nami nikifikiria nawe hujui? Unajua maana yake hivyo?

Unasema hakuna siri kwa Mungu kana kwamba kesho unaijua,

Kesho ni muhimu kwa sababu hatuijui, kesho ni siri na walio nayo ni wale wenye siri hiyo.

Kwa Mungu kuna siri nyingi kuliko kwa shetani,
Mungu bila siri hawezi kuwa Mungu,
Kusema kwa Mungu hakuna siri tafsiri yake ni kuwa Mungu hana thamani tena
 
kuna watu hawana siri ni wawazi na wakweli na uwazi wao uliwapatia utajiri Mkubwa . kuna vitu vitatu ukitaka kufanikiwa maishani Uwe Mwaminifu sana, uwe kweli, uwe Msikivu na Mnyenyekevu. uwe na bidii na juhudi na Maarifa. Mtangulize Mungu kwa kila kitu .
 
vijana wa hizi wao wanajua kila kitu , sisi wanaona tumechelewa wao wamewahi , mnakopita tulipita long time mi nasaidia tu kutoa maoni yangu ukiona yanafaa yachukue ila ukiona ni hayafai ya tupe kapuni.[emoji120]
 
Ndio haya maswali ya masikini yanavyokuwaga,

Wewe hata nikiwa tajiri unafikiri itakusaidia?

Nashukuru mfano bora umejitokeza, na wewe utakuwa Case Study humu Jamvini
Matjiri wala hawaongei sana kam wewe.
Vilevile sio kweli kuwa matajiri hawana marafiki wengi,akina Ginimbi si uliwaona wewe!
 
Bandiko bora kabisa kwa huu mwaka, mimi niko tofauti sana na viropo ropo..

Hapa kuna ndugu yangu tayari nimemuweka kando, nilimpa mchongo matokeo yake akaanza kutangaza kwa kila mtu mpka watu ambao kwa vyovyote hawawezi fanya hiyo issue, nikaona hapa hamna mtu saiz namchukulia kama jamaa tu!
 
Mkuu mbona unanitisha sana na hawa ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…