HB.com
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 608
- 639
kasajili tigo shopMpe Tigo yako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kasajili tigo shopMpe Tigo yako
kasajili tigo shop
Kama ni kwa manufaa huu umefwata nini hapa?kwan ni manufaa yake au ya nchi??
=Kirobausiwe unacomment uku umeshika kiloba
kumbe n ww vzr umejitambulishaHahahahahahahaa au we ndo yule gwash alikuwa anahojiwa clouds TV nn??
Nimegundua wengi wanaobishia utajiri wa diamond ni vijana wa umri wake ambao wengi wao bado wanaishi kwao ambao ikatokea siku akapata milioni mtaa mzima utajua.Acha hasira, maana unaongea kama vile kakulazimisha uamini wakati yeye kaulizwa swali akalijibu, sasa wewe uwe umeamini au hujaamini hayo ni matatizo yako sisi hayatuhusu.
Sijaelewa hapa milioni moja?Maneno makali ndo yapi??
Huyo mnaemuita domo hana ujanja wa kuwa hata na mil 1
Labda izo bilioni 8.6 za kuchapisha tandale
Point mkuu ukiwa mchakalikaji milioni elfu moja nindogo sanaDIAMOND kumbe bado hajui kuwekeza kwa mtu kama mimi ningeshaingia kwenye orodha ya Forbes kwa jinsi ya pesa anazozipata,angekuwa kwenye bilioni 50 au 60 kumbe yupo hapa hapa. Kumbukeni bilioni 1 = milioni 1,000 kwahiyo kama wewe ni mchakalikaji basi hivi ni vihela vya supu tu.
Pengine anauza madawa ya kulevya...kuna mada zinaendelea hapa jukwaan kuhusu utajir wa mwanamuziki Diamond ni Tshs bil 8. Sina nia ya kupinga ila tujadili kwa facts kama Great Thinker.
...........
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.
Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.
Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.
Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.
Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.
Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
............
baadhi ya michango ya wadau
1.Kuna watu wanadhani billioni ni kitu rahisi sana kuwa nacho achana na hiyo billion 8 wanayodanganya nayo....Show moja Diamond akiwa nje ya nchi analipwa Million 50.. Tufanye anafanya show nje ya nchi week zote 52 za mwaka, hiyo ni Billion 2.5 kwa mwaka, tufanye kafanya hizo show miaka miwili mfululizo inatupa Billion 5..
Anasema Vodacom walimpa Million 800, DSTV nao tufanye Million 100, Uber Million 100, Tomato Million 100, Caller tunes Billion 1.. Hapo Jumla tunapata Billion 7.1.. Na hapo hatujaweka matumizi yoyote.. Sasa hizo billion 8.6 katolea wapi.. Billion kuimiliki msifikiri mchezo.. Angekuwa anamiliki Billion 8 asingetembelea kile kigari kwa miaka mitatu sasa
2.Sio kila mtu anayekupinga anakuchukia.. Mjifunze hilo kwanza, Billion 8 bakini mkiziongelea ila hiyo pesa huyo dogo hana.. Billion 8 angekaa kwenye nyumba kama ile uko porini?? Umeona nyumba na magari wanayopush yule dogo mnaija wa 5 star music?? Mtu ana ki BMW hajakibadilisha mwaka wa tatu huu na nyumba ya kawaida kabisa inaitwa Ikulu alafu mnadanganya ana Billion 8.
3.Kwa asie jua pesa ana dhani billion ni pesa ya masihara lkn swali linakuja je, mziki unalipa kiasi hicho? ana assets zipi japo za billion 2?
4 kama mziki unalipa kwa nn kuna utofauti Mkubwa sana wa kimapato kati yake na wanamziki wengine?maana hakuna mwanamziki mwingine aliyefikisha bil 2.
5. kwa pesa hizo asingekaa huko porini Madale angetafuta mjengo masaki, mikocheni, mbezi beach au sinza( hapa naongelea msanii)
....Wadau kutiririke
Hapo umeongea point...tsh 8billion nisawa na 400m za kenya..hio pesa unaeza kununua magari matatu makubwa...mbona jaguar anamiliki kampuni ya kuuza magari na pia anamiliki ndege...jaguar ndo mwanabiashara halisi katika wasanii east africa...kama diamond anamiliki hio pesa na anatumia gari moja miaka mitano basi hajui kuekeza...Hizo million za endorsement mnazosema kalipwa mna uhakika amelipwa hizo pesa?? Na kama amelipwa mbona hakuna fair price mnasema tu zaidi ya kiasi fulani?? Na kama amelipwa unafikiri kodi inachukuliwa ngapi hapo?? Mbona miamala yake ya kodi TRA sio kwa mapato hayo ya hizo pesa mnazodanganyana kwenye mitandao.. Akilipwa na Uber Million 60 unazosema unafikiri zote zinaingia mfukoni mwake?? Hiyo 60 million anaweza kwenye account akaingiza 30 au 35 pekee hizo zingine zikaishia kwenye kodi na malipo kwa mameneja wake..
Na sidhani kama ni kweli Diamond ana hizo nyumba nyingi mnazosema, huo ni uzushi, Diamond sio msiri kiasi hicho ashindwe kuonyesha au kutangaza hizo nyumba nyingi mnazosema wakati endorsement huwa anawatangazia pesa alizolipwa.. Miaka kadhaa iliyopita alipewa Prado na boss mmoja akalitangaza ni la kwake mpaka alipokuja kunyang'anywa, alinunua nyumba Salasala akatangaza na kuiweka kwenye mitandao kila mtu akajua, hivi kweli mnafikiri Diamond anaweza kumiliki kitu watu wakashindwa kujua?? Kama mpaka kitanda cha mtoto wake na chumba chake kila Mtanzania anakijua kilivyo ndio anailiki majumba mengi asiyatangaze??
Jamani hizo pesa endeleeni kuzitaja tu kama ni rahisi kuzipata, na ni dhahiri mtu mwenye Billion 8 hawezi kuishi kwenye kama ile nyumba Diamond anayokaa tena ukizingatia ni Celeb mkubwa Africa yule, Mtu mwenye Billion 8 hawezi kushare gari na mpenzi wake tena BMW second hand..