shida iliyopo ni wivu wa pesa anazopata thats it. haishangazi hata hivyo ni kweli pia wapo hata wachungaji wengine watakuwa wanamwonea wivu kwa utajiri wake. lakini ni ngumu kwao kuwa na ushahidi wa mabaya afanyayo.
kama ni dhambi basi wanasiasa ndio watakao kuhukumiwa kwa ahadi hewa na kuzungumza uongo kwa ujanja mbele za wananchi wakiwapa matumaini feki, huku wao wakitajirika kwa jasho la wananchi na kuwaacha wananchi wakiwa choka mbaya na matumaini hewa.
na wanasiasa kama marais, wabunge, watunzi wa vitabu, wanamuziki, wanatengeneza fedha nyingi sana kwa kukusanya watu wengi na kuuza maneno kwa watu tena mengine yasiyo na mantiki wala maadili yoyote kwa jamii, na wengi wamejikuta wakiwa mamilionea kwa usanii wao, japo jamii inawaona kama wanaofaa na wakuigwa, je si bora huyu anayekusanya watu na kuwafundisha watu kuacha wizi, shirki, na kuwaasa watu kumcha mungu huku anatengeneza pesa ndefu kupitia kazi yake?
Believe me, umaskini wa nchi hii chanzo chake ni wanasiasa wasiojali maslahi ya taifa na kujali maslahi yao binafsi, na ndiyo wenye ushawishi mkubwa sana kwa jamii.